Faida Za Kuswali Qiyaamul-Layl
1-WANAOSWALI QIYAAMUL-LAYL WAMEANDALIWA PEPO
Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala)
}}تَتَجَافَى جُنُوبُهُمْ عَنِ الْمَضَاجِعِ يَدْعُونَ رَبَّهُمْ خَوْفًا وَطَمَعًا وَمِمَّا رَزَقْنَاهُمْ يُنفِقُونَ{{
}}فَلَا تَعْلَمُ نَفْسٌ مَّا أُخْفِيَ لَهُم مِّن قُرَّةِ أَعْيُنٍ جَزَاء بِمَا كَانُوا يَعْمَلُون {{
{{Mbavu zao zinaachana na vitanda kwa kumwomba Mola wao Mlezi kwa khofu na kutumaini, na hutoa kutokana na Tulivyowaruzuku}}
{{Nafsi yoyote haijui waliyofichiwa katika hayo yanayo furahisha macho - ni malipo ya yale waliokuwa wakiyatenda}} [As-Sajdah 16-17]
Aayah
hizi zinambashiria Pepo Muislamu mwenye kuhangaika na
kujitahidi kusimama kuswali usiku na mwenye kutoa mali yake kwa ajili
ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) zinambashiria Pepo ambayo imejaa
mazuri Aliyoyaficha Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) kwa ajili yao, mazuri
ya kupendeza yatakayodumu milele ambayo hajapata mtu kuyaona kwa sababu
ya vitendo vyao vizuri walivyovifanya vilifichika na Allaah (Subhaanahu
wa Ta'ala) Anaficha thawabu zao.
ففي صحيح البخاري وغيره عن أبي هريرة رضي الله عنه أن النبي صلى الله عليه وسلم قال)): قال الله تعالى:
أعددت لعبادي الصالحين ما لا عين رأت، ولا أذن سمعت، ولا خطر على قلب بشر، فاقرؤوا إن شئتم
فَلاَ تَعْلَمُ نَفْسٌ مَّا أُخْفِيَ لَهُم مِّن قُرَّةِ أَعْيُنٍ جَزَاء بِمَا كَانُوا يَعْمَلُونَ ((
Al-Bukhaariy
na wengineo wamesimulia kwamba Abu Hurayrah (Radhiya Allahu 'anhu)
amesema kwamba, Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)
amesema:
(("Allaah
(Subhaanahu wa Ta'ala) Amesema, Nimewatayarishia waja Wangu wema
yale ambayo macho hayajapata kuona, wala masikio hayajapata kusikia, na
wala hayajapata kupita katika akili ya mtu, kwa hiyo someni mkipenda
فَلاَ تَعْلَمُ نَفْسٌ مَّا أُخْفِيَ لَهُم مِّن قُرَّةِ أَعْيُنٍ جَزَاء بِمَا كَانُوا يَعْمَلُونَ
Nafsi yoyote haijui waliyo fichiwa katika hayo yanayo furahisha macho - ni malipo ya yale waliyo kuwa wakiyatenda)) [As-Sajdah 16-17]
Vile
vile Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Ametaja Wacha Mungu watakaokuwa
Peponi na yale waliokuwa wakiyafanya, na mojawapo ni kukesha usiku kwa
kufanya ibada,
}}إِنَّ الْمُتَّقِينَ فِي جَنَّاتٍ وَعُيُونٍ{{
}}آخِذِينَ مَا آتَاهُمْ رَبُّهُمْ إِنَّهُمْ كَانُوا قَبْلَ ذَلِكَ مُحْسِنِينَ{{
}}كَانُوا قَلِيلًا مِّنَ اللَّيْلِ مَا يَهْجَعُونَ{{
}}وَبِالْأَسْحَارِ هُمْ يَسْتَغْفِرُون{{
}}وَفِي أَمْوَالِهِمْ حَقٌّ لِّلسَّائِلِ وَالْمَحْرُومِ{{
{{Hakika Wacha Mungu watakuwa katika Mabustani na chemchem}}
{{Wanapokea aliyowapa Mola wao Mlezi. Kwa hakika hao walikuwa kabla ya haya wakifanya mema}}
{{Walikuwa wakilala kidogo tu usiku}}
{{Na katika mali yao ipo haki ya mwenye kuomba na asiyeomba}} [Adh-Dhaariyaat: 15-19]
2- NI KATIKA SIFA ZA WAJA WA AR-RAHMAAN
}}وَعِبَادُ الرَّحْمَنِ الَّذِينَ يَمْشُونَ عَلَى الْأَرْضِ هَوْنًا وَإِذَا خَاطَبَهُمُ الْجَاهِلُونَ قَالُوا سَلَامًا {{
}} وَالَّذِينَ يَبِيتُونَ لِرَبِّهِمْ سُجَّدًا وَقِيَامًا{{
{{Na waja wa Ar-Rahmaaan Mwingi wa Rehma ni wale wanaotembea ulimwenguni kwa staha, na wajinga wakiwasemeza hujibu: Salama!}}
{{Na wale wanaokesha kwa ajili ya Mola wao Mlezi kwa kusujudu na kusimama}} [Al-Furqaan: 63-64]
3- HUWA SIO SAWA NA WENGINE
}}لَيْسُواْ سَوَاء مِّنْ أَهْلِ الْكِتَابِ أُمَّةٌ قَآئِمَةٌ يَتْلُونَ آيَاتِ اللّهِ آنَاء اللَّيْلِ وَهُمْ يَسْجُدُونَ{{
{{Wote
hao si sawa sawa. Miongoni mwa Watu wa Kitabu wamo watu waliosimama
barabara, wanasoma Aya za Mwenyezi Mungu nyakati za usiku, na pia
wanasujudu}} [Al-'Imraan: 113]
}}أَمَّنْ هُوَ قَانِتٌ آنَاء اللَّيْلِ سَاجِدًا وَقَائِمًا يَحْذَرُ الْآخِرَةَ وَيَرْجُو رَحْمَةَ رَبِّهِ قُلْ هَلْ يَسْتَوِي الَّذِينَ يَعْلَمُونَ
وَالَّذِينَ لَا يَعْلَمُونَ إِنَّمَا يَتَذَكَّرُ أُوْلُوا الْأَلْبَابِ{{
{{Je!
Afanyae ibada nyakati za usiku kwa kusujudu na kusimama akitahadhari na
Akhera, na akitaraji rehema za Mola wake Mlezi...Sema: Eti watakuwa
sawa wale wanaojua na wale wasiojua? Hakika wanaokumbuka ni watu wenye
akili}} [Az-Zumar: 9]
4- NI NYAKATI ZA KUGHUFURIWA DHAMBI
Kama Anavyosema Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala):
}}الصَّابِرِينَ وَالصَّادِقِينَ وَالْقَانِتِينَ وَالْمُنفِقِينَ وَالْمُسْتَغْفِرِينَ بِالأَسْحَارِ{{
{{Wanaosubiri, wanaosema kweli, na watiifu, na wanaotoa sadaka, na wanaoomba maghfira kabla ya alfajiri}} [Al-'Imraan 17]
Vile vile:
((عن أبي هريرة رضي الله عنه أن رسول الله صلى الله عليه وسلم قال: ينزل ربنا تبارك وتعالى كل ليلة إلى السماء الدنيا حين يبقى ثلث الليل الآخر فيقول: من يدعوني فأستجيب له؟ من يسألني فأعطيه؟ من يستغفرني فأغفر له)) رواه الجماعة.
((Imetoka kwa Abu Hurayra (Radhiya Allahu 'anhu) kwamba Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) Amesema:
Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Huteremka kila siku katika mbingu ya
dunia (mbingu ya kwanza) inapobakia thuluthi ya mwisho ya usiku na
Husema: Nani ananiomba Nimtakabalie? Nani Ana shida nimtekelezee? Nani
ananiomba maghfira Nimghufurie?)) [Imesimuliwa na kundi la wapokezi wa Hadiyth]
5- MWENYE KUSWALI QIYAAMUL-LAYL HUPATA SIHA KATIKA MWILI
((عليكم بقيام الليل فإنه دأب الصالحين قبلكم، وقربة إلى الله تعالى، ومكفرة للسيئات، ومنهاة عن الإثم، ومطردة للداء عن الجسد )) رواه أحمد والترمذي وصححه الألباني
((Shikamaneni
na kusimama (kuswali) usiku kwani ni tabia/adabu za waja wema kabla
yenu, na kujikurubisha kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) na ni kafara
ya maovu, na ni kinga ya dhambi, na ni kiondosho cha maradhi katika
mwili)) [Ahmad na At-Tirmidhiy na kaisahihisha Shaykh Al-Albaaniy]
6- NYAKATI ZA KUKUBALIWA DU'AA
Amesema Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)
((ان في الليل لساعة لا يوافقها رجل مسلم يسأل الله تعالي خيرا من امر الدنيا و الاخرة، الا اعطاه اياه، وذلك كل ليلة)) رواه مسلم
((Hakika
katika usiku kuna saa ambayo mja anapomuomba Allaah (Subhaanahu wa
Ta'ala) kheri katika mambo ya dunia au Akhera ila (Allaah) Humpa kheri
hizo, na hivyo ni kila usiku)) Muslim
7- USHARIFU (UTUKUFU) WA MUUMIN
Kama alivyosema Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)
((أتاني جبريل فقال: يا محمد، عش ما شئت فإنك ميت، وأحبب من شئت فإنك مفارقه، واعمل ما شئت فإنك مجزي به، واعلم أن شرف المؤمن قيامه بالليل، وعزه استغناؤه عن الناس)) رواه الحاكم والبيهقي وحسنه المنذري والألباني
((Amenijia
Jibriyl akasema: Ewe Muhammad ishi upendavyo bila shaka wewe ni maiti
(utakufa), na mpende umtakaye bila shaka utafarikiana naye, na tenda
unavyopenda lakini ujue utalipwa kwa vitendo hivyo, na tambua kwamba
utukufu wa Muumin ni Qiyaamul-Llayl, na heshima yake ni kujitosheleza Na
watu)) [Al Haakim na Al Bayhaqiy, na Al Mundhiriy na Al-Abaaniy wamesema ni Hadiyth Hasan]
8- NI KUPATA HUSNUL-KHAATIMAH (MWISHO MWEMA)
((من قام بعشر آيات لم يُكتب من الغافلين، ومن قام بمائة آية كتب من القانتين، ومن قام بألف آية كتب من المقنطرين )) رواه أبو داود وصححه الألباني (والمقنطرون هم الذين لهم قنطار من الأجر)
((Atakayesimama
(usiku) na aya kumi hatoandikiwa katika miongoni mwa walioghafilika, na
atakayesimama kwa aya mia ataandikiwa ni miongoni mwa wanyenyekevu, na
atakayesimama kwa aya Alfu ataandikwa miongoni mwa wenye mirundi)) [Abu Dawuud na amesahihisha Shaykh Al-Albaaniy] (Maana ya mirundi ni wale walio na mrundi wa thawabu).
9 - USO HUNG'ARA KWA NURU
يقول الحسن البصري رحمه الله : " لم أجد من العبادة شيئا أشد من الصلاة في جوف الليل" فقيل له : ما بال المجتهدين من أحسن الناس وجوها فقال: "لأنهم خلوا بالرحمن فألبسهم من نوره"
Anasema Hasan Al-Baswry Mwenyeezi Mungu Amrehemu: "Sijapata kuona ibada iliyo nzito kama Swalah katika kiza cha usiku". Akaulizwa, Vipi wale watu wajitahidio wenye nyuso nzuri kabisa? Akajibu, "kwa sababu wamejitenga (wamejifaraghisha na) Na Ar-Rahmaan, basi Naye Akawavisha Nuru Yake."
SABABU ZA KUKUWEZESHA KUAMKA QIYAAMUL-LAYL
1- Usile na kunywa hadi ukashiba sana usiku.
2- Usijitaabishe sana mchana kwa yasiyo na faida.
3- Usiache 'Qaylulah' (kulala kidogo mchana) kwani inasaidia kuamka usiku.
4- Usifanye maasi kwani yanamzuia mtu kuamka Qiyaamul- layl.
5- Safisha moyo wako kutokana na uhasidi, chuki na waislamu wenzako.
6- Fikiria mauti na usiwe na matumaini ya kuishi sana.
7- Tambua fadhila zake.
No comments:
Post a Comment