Assalaamu 'Alaykum wa RahmatuLlaah wa Barakaatuh, Ndugu wapenzi,
Kwa
Munaasabah huu wa furaha wa siku hii tukufu ya ‘Iyd Al-Fitwr tunapenda
kuchukua fursa hii kuwawasilishia salaam zetu za siku hii na du'aa njema
kwenu wote, tukimuomba Allaah (Subhaanahu Wa Ta'ala) Atutaqabalie
'amali zetu na zenu ‘TAQABBALA ALLAAHU MINNA WA MINKUM’ (Hivi ndivyo
Maswahaba watukufu walivyokuwa wakiambiana pindi wanapokutana
katika siku ya 'Iyd).
Na
tunamuomba Yeye Aliyetukuka na Mweza, Awajaalie furaha, amani, mapenzi,
siha na Iymaan pamoja na karama na utukufu katika masiku yote ya uhai
wetu. Mwisho, bila kuwasahau wenzetu katika du'aa zetu leo na kila siku.
Ndugu zetu Waislam walio katika dhiki za ukandamizwaji, vita, njaa na
machafuko huko Burma, Syria, na palipokuwa Qiblah cha kwanza cha Uislam,
na Msikiti wa tatu kwa utukufu na hadhi, Palestina, na pote walipo
Waislamu ulimwenguni.
Tunamuomba Allaah (Subhaanahu Wa Ta'ala) Atutakabalie du'aa zetu na za Waislam wote duniani, Aamiyn
Tafadhali bonyeza kwenye picha ifuatayo upate Takbiyrah ya 'Iyd
No comments:
Post a Comment