Social Icons

rss feed facebook twitter google plus linkedin youtube email

Friday, August 31, 2012

ALOZIKWA BUTIAMA


1: NI MINGI SASA MIAKA, TANGU ALIPOONDOKA
    ONDOKA KAMA DHIHAKA, DUNIANI KAFUTIKA
    FUTIKA NA ZAKE TAKA, ZIMEBAKI TWATESEKA
    ALOZIKWA BUTIAMA..............................

2: ALICHOFANYA HAKUNA, TUBAKI KUJIVUNIA
    KUJIVUNIA LA MAANA, URITHI KWA TANZANIA
    TANZANIA TUJE NENA, BABO ALOTUCHIA
    ALOZIKWA BUTIAMA......................

3: AZIMIO ALIUNDA, MALI AKATAIFISHA
   TAIFISHA NA VIWANDA, NA NYUMBA JIMILIKISHA
   JIMILIKISHA NA UKANDA, WA PWANA AKAUFISHA
   ALOZIKWA BUTIAMA.................................

4: ALITUKUZA UDINI, AKAENZI UBAGUZI
   UBAGUZI KWETU PWANI, AKAHUJUMU MAKAZI
   MAKAZI YA VIJIJINI, UJAMAA UKAWINI
   ALOZIKWA BUTIAMA..........................

5: LEO MNAMWITA BABA, SEMENI KWA MKE GANI?
    MKE GANI WA HAIBA, AWE MAMA TAIFANI?
    TAIFANI TUJE SHIBA, ATUOPOE TOPENI?
    ALOZIKWA BUTIAMA.........................

6: LAU LAPIGWA KABURI, NINGELIPIGA LA KWAKE
   LA KWAKE KWA ZAKE SHARI, VIBAYA VITENDO VYAKE
   VYAKE VYA WAZI NA SIRI, ALOFANYA ASIFIKE
   ALOZIKWA BUTIAMA.................................

7: TWAMUOMBA SUBHANA, ATUEPUSHA NA DHAHAMA
    DHAHAMA ZA HUYU BWANA, ALOZIKWA BUTIAMA
    BUTIAMA NANONG'ONA SIJAONA WAKE WEMA
    ALOZIKWA BUTIAMA.......................

8: ALOZIKWA BUTIAMA, SIJAONA WAKE WEMA
    WEMA ULITUAMA, UBAYA UKAUZIMA
    UKAUZIMA DAIMA, USIPATE LA KUSEMA
    ALOZIKWA BUTIAMA............................

Thursday, August 30, 2012

Malawi yajiondoa kwenye Paralympics

Malawi imejiondoa kutoka mashindano ya Olimpiki ya walemavu yaliyoanza rasmi mjini London.
Hii ingekuwa mara ya kwanza kwa taifa hilo kushiriki katika michezo hiyo lakini inadaiwa kuwa ukosefu wa fedha umeilazimisha kujiondoa.
Wanariadha vipofu Chisomo Jeremani na Janet Shedani pamoja na wasaidizi wao wawili na maafisa wanne wa michezo ndio waliotarajiwa kusafiri London kwa ajili ya michezo hiyo.
Kamati ya michezo ya olimipiki ya walemavu nchini humo, imelaumu serikali pamoja na makampuni ya kibinafsi kwa kukosa kuwafadhili.
Kamati ya kimataifa ya Paralimpics huenda ikapendekeza hatua kuchukuliwa dhidi ya Malawi.
Waandalizi wa michezo hiyo nchini Uingereza, Locog tayari walikuwa wametoa ufadhili kusaidia katika safari ya wachezaji hao kuelekea London,lakini kulingana na maafisa nchini Malawi, pesa hizo hazikutosha kutuma kikosi chote hicho ikiwemo wanariadha na wasaidizi wao.
Mwandishi wa BBC nchini Malawi, Frank Kandu amesema kuwa changamoto zinazokabili kamati ya michezo ya paralympics ya Malawi, zilisababishwa na matatizo ya kiuchumi yanayoikabili nchi hiyo ya kusini mwa Afrika.
Mnamo mwezi Mei, rais mpya wa nchi hiyo Joyce Banda, alishusha thamani ya sarafu ya nchi hiyo kwa asilimia 33 kama sehemu ya mpango wa serikali kutaka jamii ya kimataifa kuanza tena kuipatia msaada.

NANI ALIYE MUUWA SHEIKH ABOUD ROGO..????


p1d Riots in Mombasa after killing of Muslim cleric
MOMBASA: The daughter of Muslim Leader Aboud Rogo cries out as Rogo’s father holds the slumped and bloodstained body of his son in the vehicle where Rogo was shot dead near the Jomo Kenyatta.

haya ndio yaliyofuatia baada ya kuuliwa Sheikh aboud Rogo nchini pwani si kenya.

pwani si kenya mambo si shwari

mombasa yachafuka

mtaa kwa mtaa mamwera wakumwanga baba sio mchezo pwani si kenya

mpaka juu ya magorofa askari wamemwagwa duu mombasa iko chini ya ulizi wa machogo

sheikh Aboud Rogo wakati wa uhai wake kabla hajauliwa

silaha kubwa kubwa ndio kuleta amani au kuchafuwa amani..?

TCRA yahitaji 6bn/ kuweka anuani Dar es Salaam



Na Kunze Mswanyama,DAR ES SALAAM
MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) inahitaji zaidi ya shilingi bilioni 6 ili kuweka anuwani za makazi kwa mkoa wa Dar es salaam pekee ikiwa ni gharama za ununuzi wa vitendea kazi, usafiri na mahitaji mengine ya lazima.

Hata hivyo,TCRA imeomba wananchi kuchangia zoezi hilo kwani kutokana na kupanda kwa gharama za bidhaa, mahitaji yanazidi kuongezeka na kwamba imepangwa kufanyika harambee maalum.

Katibu Mkuu wa wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Dk.Florens Turuka alipokuwa akitoa taarifa ya mradi huo mbele ya wandishi wa habari waliojumuika kwa pamoja na wabunge wote wa Dar es salaam.

Alisema, kwa kutambua umuhimu wa mradi huo viongozi wa jiji walikubaliana kwa pamoja kuandaa chakula cha hisani cha kuweza kuchangisha na kupata fedha za kuchangia utekelezaji kwa ufanisi na kwa muda uliopangwa.


“Serikali kwa kupitia TCRA imefungua akaunti maalumu kwa ajili ya uchangiaji mradi huo ili kutekeleza mfumo wa anwani za makazi katika mkoa wa Dar es salaam. Akaunti hiyo inaitwa TCRA-Postcode Project 0150315694502 iliyofunguliwa katika benki ya CRDB tawi la Mlimani City”,alisema Dk.Turuka.

Mradi huo uliozinduliwa na aliyekuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye kwa sasa ni Rais wa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar mwaka 2009, tayari umekwisha fanyiwa majaribio mikoa ya Arusha na Dodoma ambapo ulionesha mafaniko makubwa.

Akizungumzia changamoto zinazowakabili, Mkurugenzi Mkuu wa TCRA Prof.John Nkoma alisema ni pamoja na uhaba wa fedha na baadhi ya watu wasiokuwa waaminifu kuiba miundombinu ya anuwani hizo ikiwemo vibao vya kuonesha mitaa.

Nkoma alisema gharama za mradi huo mkubwa na unaoongeza ajira kupitia utalii, tayari umekwisha peleka kikosi kazi nchini Afrika Kusini ili kujifunza namna ya kuweka anuwani za makazi kwenye makazi yasiyopimwa.

Kwa upande wake Meya wa Jiji la Dar es salaam,Dk.Didas Masaburi alisema jiji lina zaidi ya 70% ya maeneo ambayo hayajapimwa jambo linalofanya kazi kuwa kubwa zaidi huku muda zaidi ukihitajika kutengwa ili kuhakikisha kila nyumba inapatiwa namba yake.

Wajumbe wengine ni wizara ya Miundombinu na Mawasiliano ya Zanzibar, Ardhi, Makaazi, Maji na Nishati ya SMZ, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa-Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa pamoja na wizara ya Fedha.

Aidha,wajumbe wengine wa kamati hii ni viongozi wa juu wa taasisi zifuatazo.Mkurugenzi Mkuu TCRA,Posta Masta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC),Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Vitambulisho vya Taida (NIDA) na Mkurugenzi Mkuu Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS).

Prof.Nkoma pia aliwatoa wasiwasi wananchi kuwa anuwani hizo hazimzuii mtu yeyote kuhama kutoka eneo moja hadi jingine kutokana na kuwa na mfumo unaowezesha kubadilisha anuwani kama ilivyo kwa kadi za benki ambapo mteja huweza kubadilisha namba ya siri muda wowote apendapo.

CRA yahitaji 6bn/ kuweka anuani Dar es Salaam



Na Kunze Mswanyama,DAR ES SALAAM
MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) inahitaji zaidi ya shilingi bilioni 6 ili kuweka anuwani za makazi kwa mkoa wa Dar es salaam pekee ikiwa ni gharama za ununuzi wa vitendea kazi, usafiri na mahitaji mengine ya lazima.

Hata hivyo,TCRA imeomba wananchi kuchangia zoezi hilo kwani kutokana na kupanda kwa gharama za bidhaa, mahitaji yanazidi kuongezeka na kwamba imepangwa kufanyika harambee maalum.

Katibu Mkuu wa wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Dk.Florens Turuka alipokuwa akitoa taarifa ya mradi huo mbele ya wandishi wa habari waliojumuika kwa pamoja na wabunge wote wa Dar es salaam.

Alisema, kwa kutambua umuhimu wa mradi huo viongozi wa jiji walikubaliana kwa pamoja kuandaa chakula cha hisani cha kuweza kuchangisha na kupata fedha za kuchangia utekelezaji kwa ufanisi na kwa muda uliopangwa.

“Serikali kwa kupitia TCRA imefungua akaunti maalumu kwa ajili ya uchangiaji mradi huo ili kutekeleza mfumo wa anwani za makazi katika mkoa wa Dar es salaam. Akaunti hiyo inaitwa TCRA-Postcode Project 0150315694502 iliyofunguliwa katika benki ya CRDB tawi la Mlimani City”,alisema Dk.Turuka.

Mradi huo uliozinduliwa na aliyekuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye kwa sasa ni Rais wa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar mwaka 2009, tayari umekwisha fanyiwa majaribio mikoa ya Arusha na Dodoma ambapo ulionesha mafaniko makubwa.

Akizungumzia changamoto zinazowakabili, Mkurugenzi Mkuu wa TCRA Prof.John Nkoma alisema ni pamoja na uhaba wa fedha na baadhi ya watu wasiokuwa waaminifu kuiba miundombinu ya anuwani hizo ikiwemo vibao vya kuonesha mitaa.

Nkoma alisema gharama za mradi huo mkubwa na unaoongeza ajira kupitia utalii, tayari umekwisha peleka kikosi kazi nchini Afrika Kusini ili kujifunza namna ya kuweka anuwani za makazi kwenye makazi yasiyopimwa.

Kwa upande wake Meya wa Jiji la Dar es salaam,Dk.Didas Masaburi alisema jiji lina zaidi ya 70% ya maeneo ambayo hayajapimwa jambo linalofanya kazi kuwa kubwa zaidi huku muda zaidi ukihitajika kutengwa ili kuhakikisha kila nyumba inapatiwa namba yake.

Wajumbe wengine ni wizara ya Miundombinu na Mawasiliano ya Zanzibar, Ardhi, Makaazi, Maji na Nishati ya SMZ, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa-Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa pamoja na wizara ya Fedha.

Aidha,wajumbe wengine wa kamati hii ni viongozi wa juu wa taasisi zifuatazo.Mkurugenzi Mkuu TCRA,Posta Masta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC),Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Vitambulisho vya Taida (NIDA) na Mkurugenzi Mkuu Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS).

Prof.Nkoma pia aliwatoa wasiwasi wananchi kuwa anuwani hizo hazimzuii mtu yeyote kuhama kutoka eneo moja hadi jingine kutokana na kuwa na mfumo unaowezesha kubadilisha anuwani kama ilivyo kwa kadi za benki ambapo mteja huweza kubadilisha namba ya siri muda wowote apendapo.

MCT yakipongeza Chuo cha habari Zanzibar

Na Husna Mohammed
BARAZA la Habari Tanzania (MCT), limekipongeza Chuo cha Uandishi wa Habari Zanzibar (ZJMMC), kutokana na kiwango chake cha elimu inachokitoa chuoni hapo.

Katibu Mkuu wa Baraza hilo, Kajubi Mukajanga, aliyasema hayo jana alipofungua mafunzo ya kuwajengea uwezo wa kitaaluma walimu wa Chuo cha Uandishi wa Habari Zanzibar, yaliyofanyika ofisi za Baraza la Habari Zanzibar tawi la Zanzibar hapo Mlandege mjini hapa.

Alisema chuo cha ZJMMC, kinatoa taaluma ya ushindani wa soko la ushindani katika tasnia ya habari ikilinganishwa na vyuo vya habari vinavyochipukia hasa upande wa Tanzania bara.

"Kwa kuwa tasnia hii unaweza kufanya kazi popote ni dhahiri waandishi wanaopata taaluma hiyo wanaweza kuingia katika ushindani mkubwa na si kwa Tanzania bara, nchi jirani lakini pia wanaweza kufanya kazi nchi yoyote na mashirika makubwa ya habari", alisema.

Kajubi, alisema pamoja na mambo mengine, walimu hao wanaopatiwa mafunzo ya siku nne kwa kiasi kikubwa yatawawezesha kutoa elimu ya ubora zaidi inayohitajika NACTE ili kuwawezesha wanafunzi wanaomaliza masomo yao kutambulikana zaidi.

Aidha alisema mafunzo hayo yatawawezesha kwenda sambamba na mitaala inayotakiwa na NACTE, jambo ambalo litawapa upeo mkubwa wa ufundishaji walimu.

"Lengo letu ni kutaka kuona tunawaandaa waandishi kuweza kufanya kazi zao vizuri wanapomaliza masomo yao", alisema.

Nae Mkuu wa Chuo cha Uandishi wa Habari Zanzibar, Saleh Yussuf Mnemo, alisema kwa kiasi kikubwa mafunzo hayo yataweza kuwajengea uwezo walimu wanaofundisha chuoni hapo, sambamba na kuelekea katika usajili wa NACTE kwa chuo hicho.

"Ni wazi kuwa sasa tunaelekea katika mchakato wa kupata usajili wa NACTE hasa ikizingatiwa kuwa mitaala hii inaendana hasa na kile wanachokitaka", alisema.

Mafunzo hayo yameandaliwa na Baraza la Habari Tanzania na kusimamiwa na kuratibiwa na Baraza la Taifa na viwango vya Elimu Tanzania (NACTE).

Wednesday, August 29, 2012

Uamsho ni rehema ilioteremshiwa ASP na CCM–Zanzibar Kwanini waipiga mabomu?

sheikh farid hadi Na Laila Abdullah,
Ni ukweli usiokanushika wa Historia ya miaka 48 ya Mapinduzi na Muungano, kwamba Chama cha Afro-Shirazi Party (ASP) na baadae CCM –Tawi la Zanzibar, pamoja na viongozi wake wote walioshika hatamu tangu 1964, ndio wenye JUKUMU la Msiba ulioiangukia Zanzibar. ASP kamwe haiwezi wala haipaswi kuvitupia lawama vyama vyengine vya kisiasa kuhusu kusababisha msiba huo.
ASP na baadae CCM (Zanzibar) na Viongozi wake wote walishika hatamu na mpini kuamua hatima ya Zanzibar, ndio walioshika mpini chini ya biramu la “MAPINDUZI DAIMA”. Hatamu na Mpini huo hawakutaka kuziachia au kuwaponyoka tena kwa kila hali hadi hii leo.
Msiba gani huo?
Ni Msiba wa Zanzibar kupoteza Uhuru wake na Mamlaka yake (Soveregnity) kwa Tanganyika iliojibatiza jina la Tanzania . Matokeo yake kuanzia April 26,1964 , ni kuona historia ya miaka 2000 ya dola la Zenj kuanzia (City State)ikianza kuzikwa kabisa hatua kwa hatua.Mjadala wa sasa wa Katiba mpya ambao awali ulikataza maoni juu ya Muungano “mtakatifu”, unalenga kuizika kabisa dola ya Zanzibar hapo 2014.

Ni chini ya usimamizi wa Afro-Shirazi Party ndipo:
a) Zanzibar ilipoteza KITI chake Katika Umoja wa Mataifa 1964-
b) Zanzibar imepoteza Umashuhuri wake katika ramani ya dunia-
c)Zumari leo likipulizwa Zanzibar,hakuna tena achezae mrima-
d)Zanzibar,haiwezi kufunga Mikataba ya Mikopo na wafadhili wa Kimataifa bila ya ruhusa ya Dodoma-
e)Zanzibar ilibidi kujitoa Jumuiya ya Nchi za Kiislamu (OIC) licha ya kuwa ndio iliokuwa Mecca ya Afrika ya Mashariki katika kueneza uislamu-
f)Hata hodi-hodi za Zanzibar kujiunga na Shirikisho la mpira Ulimwenguni (FIFA), hazikufua dafu.
g) Marais wa Zanzibar wanachaguliwa na kuidhinishwa DODOMA kama tulivyoona kisa cha Dr.Amani Karume na Dr.Gharib Bilal.

Kwa ufupi, ni dhahiri-shahiri kuwa,chini ya UONGOZI wa ASP na baadae CCM-Zanzibar, visiwa vyetu vimepoteza SAUTI yake ndani na nje ya Zanzibar .Hali hii ya kufadhahisha, yafaa kuungama hatahivyo, haikuridhiwa na viongozi wote wa afro-shirazi party na baadae wa CCM-Zanzibar .Walipotanabahi na kun’gamua madhambi walioifanyia nchi yao, walijaribu kurekebisha au kugeuza mkondo,lakini bila ya mafanikio.
Mzee Karume alijaribu wakati wa utawala wake wa miaka 8 ulioanzia Januari 12,1964 hadi kuuwawa kwake April 7, 1972 kuikwamua Zanzibar kutoka makucha ya “MUUNGANO-KOTI”bila kudiriki kulivua.Rais Jumbe,mfuasi wake madarakani, nae alijaribu 1984 na kuangushwa Dodoma-lilikochimbwa KABURI la kuizika dola ya Zanzibar na hata viongozi wake.
Commandoo Dr.Salmin Amour,alitumbua macho huku nae KIBIRITI chake KIKITIKISWA alipolazimishwa kujitoa OIC (Jumuiya ya Nchi za Kiislamu). Mwalimu Nyerere aliukomea mlango wa nyuma na wa mbele wa OIC mpaka hii leo wakati nchi ambayo inapinga UDINI,ni rukhsa kuwa na usuhuba wa kibalozi na VATICAN na hata kulitambua dola la Wakristo wa Nigeria ya Mashariki (BIAFRA) walilojaribu kuunda miaka ya 1970.
Seif Shariff na wenzake wakiwa ndani ya CCM walipotaka kufuata NYAYO za Rais Jumbe, na kutetea masilahi ya Zanzbar,walikiona kilichomtoa kanga manyoya walipotimuliwa nje ya CCM Dodoma.
Matokeo yake : Yeyote Yule anaebisha sera za CCM-DODOMA, mfano walivyofanya hivi punde akina Mzee Hassan Nasoro Moyo na Mansouri Himidi kuiweka nchi yao ya Zanzibar kwanza na sera za chama nyuma, SAUTI ZA “MASULTANI WA DODOMA NA MABALOZI WAO waliopo VISIWANI ZANZIBAR NA PEMBA”, zinamkemea. Eti wanakiuka sera ya chama ya serikali 2 kwendea moja ? Ni dhahiri uwepo wa serikali 3 unazuwia sera ya serikali mbili kwendea moja. USIA ULIOACHIWA CCM NA BABA WA TAIFA. Ndipo Mwalimu alipowakemea akina Kikwete na wenzake G-55 walipodai serikali ya Tanganyika.
Hatua walizochukua viongozi hao wote wa Afro-Shirazi party au CCM –Zanzibar, kumvika paka kengele, hazijaiokoa Zanzibar .Na wapi viongozi wa sasa wa CCM walioshika mpini na hatamu katika serikali ya umoja wa kitaifa- akina Sheni na Balozi Seif Idi, wanakoikokota Zanzibar huku wakitetea sera ya chama ya serikali 2 , ni siri yao wenyewe. Mzalendo yeyote wa Zanzibar anaekula kiapo huku ameshika msahafu kuitetea na kuilinda Zanzibar,hawezi kamwe kuchangia mazishi yake makaburini dodoma.
Ni jambo la wazi kabisa viongozi hawa wa CCM , bila ya ridhaa ya Dodoma, wasingeshika hatamu tangu chamani hata serikalini.Vilio vya hivi punde za kuwaajibisha akina Mzee Moyo na kijana Mansouri, ni ushahidi wa hayo.Idhini ya wazanzibari, yadhihirika hawaihitaji na ndio maana wahafidhina ndani ya CCM –Zanzibar na bara ,wanatetea sera za chama na sio nchi yao (Zanzibar).Kuibuka kwa jumuiya ya kiislamu ya muamsho na kudai haki na mamlaka ya Zanzibar,kwa hivyo, ni neema ilioteremshiwa viongozi wa sasa na wa zamani wa ASP-CCM (Zanzibar) na mwenye enzi Mungu.
Ni jahazi la safina walioletewa kulipanda kuwavusha salama na dharuba za kisiwa cha chumbe na mwishoe kujikosha na laana za kuja kulitosa kabisa dola la Zanzibar.kwamba kwani historia itakuja kuandika kuwa (ASP) ndicho chama kilichoiongoza Zanzibar chini ya biramu la “mapinduzi daima” kutoweka katika ramani ya dunia.
Viongozi wa jumuiya ya UAMSHO- akina Amir Msellem;farid na zan ,wamenadi hadharani,tena dhahiri-shahiri kuwa , hawataki madaraka! .
Watakacho ni kuwarejeshea VIONGOZI wa Zanzibar hadhi yao,kuirejeshea Zanzibar na WaZanzibari UHURU wao na MAMLAKA yao na kuwafanya waZanzibari wote wa Zanzibar na Pemba wapumuwe.

Kwanini basi wanapigwa mabomu hata misikitini?
Kile viongozi wa CCM-ZANZIBAR isipokuwa wachache kama Mzee Moyo na Mansour , wasichothubutu kudai kwa nchi yao ya Zanzibar,UAMSHO wanakidai,tena bila ya hofu,woga na kutetereka. wamejitoa mhanga kusafisha madhambi ya miaka 48 ya viongozi wa ASP na CCM-Zanzibar, waliofanya ama kwa kupenda au kwa kulazimishwa .
Kwanini basi neema hii ilioteremshiwa ASP na CCM-Zanzibar na mwenye enzi mungu,hawaipokei mikono miwili na badala yake waipiga mabomu ? je, chama bora kuliko Zanzibar ?

Monday, August 27, 2012

KUJA KWA JIBRIIL عليه السلام KUWAFUNDISHA WAISLAMU MAMBO YA DINI YAO

الحديث الثاني
"مجىء جبريل ليعلم المسلمين أمر دينهم"
 عَن عُمَر رضي اللهُ عنه أَيْضاً قال:   بَيْنَما نَحْنُ جُلْوسٌ عِنْدَ رسُولِ الله صلى الله عليه وسلم ذات يَوْم  إذْ طَلَعَ عَلَيْنَا رَجُلٌ شَدِيدُ بَياضِ الثِّيَاِبِ شَديدُ سَوَادِ الشَّعْرِ، لا يُرَى عليه أَثَرُ السَّفَرِ ولا يَعْرِفُهُ مِنَّا أَحَدٌ، حَتى جَلَسَ إلى النَّبِّي صلى الله عليه وسلم، فأسْنَدَ رُكْبَتَيْهِ إلى رُكْبَتَيْهِ ووَضَعَ كَفَّيْهِ على فَخِذَيْهِ، وقال: يا محمَّدُ أَخْبرني عَن الإسلامِ، فقالَ رسُولُ الله صلى الله عليه وسلم:(( الإسلامُ أَنْ تَشْهَدَ أَنْ لا إلهَ إلا اللهُ وأَنَّ محمِّداً رسولُ الله، وتُقِيمَ الصَّلاةَ، وتُؤتيَ الزَّكاةَ، وتَصُومَ رَمَضان، وتَحُجَّ الْبَيْتَ إن اسْتَطَعتَ إليه سَبيلاً)). قالَ صَدَقْتَ. فَعَجِبْنا لهُ يَسْأَلُهُ ويُصَدِّقُهُ، قال : فَأَخْبرني عن الإِيمان. قال: ((أَن تُؤمِنَ باللهِ، وملائِكَتِهِ وكُتُبِهِ، ورسُلِهِ، واليَوْمِ الآخِرِ، وتُؤمِنَ بالْقَدَرِ خَيْرِهِ وشَرِّهِ)) قال صدقت. قال : فأخْبرني عَنِ الإحْسانِ. قال:(( أنْ تَعْبُدَ الله كَأَنَّكَ تَرَاهُ فإنْ لَمْ تَكُنْ تَرَاهُ فإنَّهُ يَرَاك)). قال: فأَخبرني عَنِ السَّاعةِ، قال: ((ما المَسْؤولُ عنها بأَعْلَمَ مِنَ السَّائِلِ )). قال: فأخبرني عَنْ أَمَارَتِها، قال:(( أن تَلِدَ الأمَةُ رَبَّتَها، وأَنْ تَرَى الحُفاةَ العَُراةَ العالَةَ رِعاءَ الشَّاءِ يَتَطَاوَلُونَ في الْبُنْيانِ )) ثُمَّ انْطَلَقَ، فَلَبِثْتُ مَلِيّاً، ثُمَّ قال : ((يا عُمَرُ، أَتَدْرِي مَنِ السَّائِلُ؟)) قُلْتُ: اللهُ ورسُولُهُ أَعلَمُ . قال:(( فإِنَّهُ جِبْرِيلُ أَتاكُمْ يُعَلِّمُكُمْ دِينَكُمْ))   
رَوَاهُ مُسْلِمٌ

  
HADITHI YA 2
KUJA KWA JIBRIIL عليه السلام KUWAFUNDISHA WAISLAMU MAMBO YA DINI YAO  
  
Kutoka kwa 'Umar رضى الله عنه ambaye amesema: Siku moja tulikuwa tumekaa na Mtume صلى الله عليه وسلم  , hapo alitokea  mtu ambaye  nguo zake zilikuwa nyeupe pepe na nywele zake zilikuwa nyeusi sana; hakuwa na alama  ya machofu ya safari na wala hapakuwa na hata mmoja katika sisi aliyemtambua. Alienda akakaa karibu na Mtumeصلى الله عليه وسلم akaweka magoti yake karibu na magoti yake (Mtume) na akaweka viganja vyake juu ya mapaja yake kisha akasema; Ewe Muhammad! Niambie kuhusu Uislamu.  Mjumbe wa Allaah  صلى الله عليه وسلمalisema:  Uislamu ni kukiri kuwa hakuna mola isipokuwa  Allaah na Muhammad ni Mjumbe wake, kusimamisha Swalah, kutoa Zakaah, kufunga Ramadhaan na kwenda kuhiji (Makkah) ukiweza.  

(Akasema yule mtu yaani Jibriyl) Umesema kweli. Tulipigwa na mshangao kwa kumuuliza kwake Mtume na kumsadikisha.  Na akasema tena: Niambie  kuhusu Iymaan.  Akasema (Mtume صلى الله عليه وسلم) Ni kumwamini Mwenyeezi-Mungu, Malaika Wake, Vitabu Vyake, Mitume Yake na siku ya Qiyaama, na  kuamini ya kuwa kheri na shari zinatoka Kwake (Allaah سبحانه وتعالى  ). (Akasema Jibriyl): Umesema kweli, akasema hebu nielezee kuhusu Ihsaan.  Akasema Mtume صلى الله عليه وسلم   Ni kumuabudu Allaah سبحانه وتعالى   kama vile unamuona na kama humuoni basi Yeye Anakuona.  Akasema (Jibriyl):  Niambie    kuhusu Qiyaama.  Akajibu (Mtume  صلى الله عليه وسلم : Muulizwaji si mjuzi kama asivyo vilevile Muulizaji. Kisha akamwambia: Nijulishe alama zake: Akajibu (Mtume صلى الله عليه وسلم): Kijakazi atazaa bibi yake, na utaona wachunga wenda miguu chini, wenda uchi (wasio na uwezo wa kumiliki hata mavazi), mafukara (wasiokuwa hata na sehemu ya kuishi kwa umaskini) wakishindana kujenga majumba ya fahari. Kisha akaondoka (Jibriyl) na nilitulia kidogo (nikitafakari). Kisha akasema Mtume صلى الله عليه وسلم : "Ewe 'Umar! Je, unamjua ni nani yule aliyekuwa akiuliza? Nikasema: Allaah na Mjumbe wake wanajua zaidi.  Akasema Mtume   صلى الله عليه وسلم: Ni Jibriyl, alikuja kuwafundisha dini yenu.
Imesimuliwa na Muslim

TOBA (TAUBA)

Salaam zangu natuma, ziwafike Afrika,
Mungu Awape hekima, mzidi kuneemeka,
Naomba Zake rehema, zivuke zote mipaka,
Omba Toba kwa haraka, madhambi unapotenda.

Madhambi unapotenda, omba toba kwa haraka,
Mungu sana Anapenda, Aombwe kila dakika,
Hujuwi unapokwenda, lini roho itatoka,
Omba Toba kwa haraka, madhambi unapotenda.

Yupo macho Maulana, Halali na Kuzeeka,
Kila kitu Anaona, yote yanayotendeka,
Si usiku si mchana, Yupo macho Mtukuka,
Omba Toba kwa haraka, madhambi unapotenda.

Yupo karibu na sisi, dua Kwake zinafika,
Ili zifike upesi, tuzidi Kumkumbuka,
Tuache yote maasi, ili Apate ridhika,
Omba Toba kwa haraka, madhambi unapotenda.

Wakati unatoroka, tupo kwenye hekaheka,
Mauti yatatufika, ghafla tutaanguka,
Hapo tunapodondoka, toba imeshafungika,
Omba Toba kwa haraka, madhambi unapotenda.

Shetani yupo mbioni, humuoni akichoka,
Hutupambia machoni, baya sawa huliweka,
Atutie mtegoni, halafu anatucheka,
Omba Toba kwa haraka, madhambi unapotenda.

Alipokua peponi, Adamu kahadaika,
Kadanganywa na shetani, balaa ikamfika,
Akatubu Kwa Manani, mwishowe akaokoka,
Omba Toba kwa haraka, madhambi unapotenda.

Kuomba toba ni nzuri, kosa linapofanyika,
Unajiweka tayari, ajali inapofika,
Kumbuka mbele kaburi, na moto usozimika,
Omba Toba kwa haraka, madhambi unapotenda.

Omba toba kila mara, huku ukisikitika,
Omba sana maghfira, toa kidogo sadaka,
Kumbuka sana akhera, na siku ya kufufuka,
Omba Toba kwa haraka, madhambi unapotenda.

Mungu Atupe uzima, hapa mwisho kuandika,
Atupe nguvu na hima, radhi Zake tunataka,
Atupe nzuri hatima, na madhambi kufutika,
Omba Toba kwa haraka, madhambi unapotenda.

Allaah Awanusuru Syria Na Myanmar (Burma)


Kwa jina Lake Mwenyezi, Mola wetu Subhana,
Nawasalimu Wapenzi, Awalinde Maulana,
Yeye ndie Mkombozi, Peke Yake hana mwana,
Mungu Awaangamize, Manusayri makafiri.

Manusayri makafiri, Syria wanapigana,
Mashia hawa hatari, hawajui uungwana,
Wao wanapenda shari, wanapenda kuuana,
Mungu Awaangamize, Manusayri makafiri.

Ni maadui wa Sunni, yote yanaonekana,
Huwachinja Waumini, kwa silaha kila aina,
Silaha toka Irani, na Urusi na Uchina,
Mungu Awaangamize, Manusayri makafiri.

Waumini siku hizi, Syria wana shida sana,
Wamekuwa Wakimbizi, hata chakula hawana,
Wengine hawajiwezi, wanakufa tunaona,
Mungu Awaangamize, Manusayri makafiri.

Manusayri mashetani, makafiri wajalana,
Hawafungi Ramadhani, wala Kuhiji hapana,
Dini yao sio dini, na Pagani hufanana,
Mungu Awaangamize, Manusayri makafiri.

Allah Awape subira, watoto wanalizana,
Wanarusha makombora, kwa marefu na mapana,
Mabinti hutekwa nyara, nashindwa hata kunena,
Mungu Awaangamize, Manusayri makafiri.


                       

Kwingine ni Myanmari, wanapigwa Waumini,
Tunakuomba Qahari, Rudisha kwao amani,
Watoe kwenye hatari, wamo kwenye mtihani,
Mungu Awaangamize, Mabudha wa Myanmari.

Mabudha wa Myanmari, Burma jina la zamani,
Watose kwenye bahari, kama vile Fira’auni,
Uvunje yao kiburi, na vichwa virudi chini,
Mungu Awaangamize, Mabudha wa Myanmari.

Na tena bila futari, walifunga Ramadhani,
Na Wewe ndio Jabari, Unawaona Machoni,
Faraji wanasubiri, kutoka Kwako mbinguni,
Mungu Awaangamize, Mabudha wa Myanmari.

Umoja wa Mataifa, wananyamaza kwa nini?
Sababu wanaokufa, ni Waislamu yakini,
Twazijua zao sifa, na chuki kwa yetu dini,
Mungu Awaangamize, Mabudha wa Myanmari.

Tuamke Waislamu, na macho yafumbueni,
Imani iwe timamu, masikio zibueni,
Walimu na Maimamu, watoto wazindueni,
Mungu Awaangamize, Mabudha wa Myanmari.

Kweli nina wasiwasi, ndugu wapo hatarini,
Ninamuomba Mkwasi, Awalinde masikini,
Ombeni duaa upesi, kwenye Swalah ziombeni,
Mungu Awaangamize, Mabudha wa Myanmari.

Sunday, August 26, 2012

MUENZI MKE WAKO

Kwa kuoa huchukui tu mke, Bali unachukua ulimwengu wako mzima. Kuanzia hapo mpaka maisha yako yote mke wako atakuwa mwenzio, mwandani wako, na rafiki yako mpenzi.
Atashiriki katika nyakati zako nzuri, siku zako, na miaka yako. Atakuwa pamoja nawe katika furaha na shida, katika mafanikio na tabu, katika ndoto zako na katika wakati wa hofu. Ukiumwa, atakupa huduma bora kabisa. Wakati unapohitaji msaada atafanya vyovyote awezavyo kwa ajili yako. Wakati una siri, ataitunza siri yako, wakati unahitaji ushauri, atakupa ushauri mzuri kabisa.
Atakuwa na wewe utakapoamka asubuhi kitu cha kwanza ambacho macho yako yataona ni macho yake. Wakati wa mchana, atakuwa na wewe, kama kuna wakati mchache hatokuwa na wewe kwa kimwili, atakuwa anakufikiria wewe, anakuombea dua kwa moyo wake wote, akili yake yote, na roho yake nyote. Ukienda kulala usiku, kitu cha mwisho macho yako kuona itakuwa ni yeye, na ukilala bado utakuwa unamuona katika ndoto zako. Kwa kifupi atakuwa ni ulimwengu wako mzima na wewe utakuwa ulimwengu wake mzima.  
Kielezo bora kabisa ambacho mimi binafsi nishawahi kusoma kinafafanua ukaribu wa wanandoa juu ya wao kwa wao na kielezo hicho kipo katika aya ya Qur-aan ambayo inasema:
((Wao ni vazi kwenu, na nyinyi ni vazi kwao)) [Al-Baqarah 2:187].
Na Kweli, wanandoa ni kama vazi juu ya wao kwa wao kwa sababu wanapeana ulinzi, liwazo, kinga (stara), msaada (tegemeo), na mapambo ambayo vazi linampa mtu. Hebu jaribu kufikiri msafara wakati wa siku za baridi kwenda sehemu kama vile Alaska bila ya kuwa na nguo! Wanandoa wetu wanatupa kiwango kile kile cha faraja (liwazo), ulinzi, na msaada  katika msafara wa maisha yetu katika dunia hii kama vile nguo itakavyofanya katika msafara wa Alaska.
Mahusiano baina ya wanandoa ni ya kustaajabisha kabisa katika mahusiano yote ya kibinaadamu: Idadi ya mapenzi na mahaba, undani na ukaribu, huruma na imani, amani na utulivu ambao unajaza nyoyo za wanandoa ni jambo lisiloelezeka kwa wepesi. Ufafanuzi pekee wa mantiki ambao unaweza kuelezeka juu ya haya mastaajabu makubwa katika hisia zote za kibinaadamu ni kwamba: Ni kitendo cha Allah Subhanahu wa Ta'ala, ((Na Allaah Amekuumbieni wake [na wenza katika jinsi yenu])) [An-Nahl 16:72]
Mola wetu tu Allaah Subhanahu wa Ta'ala katika katika Utawala Wake usio na upeo wa huruma Yake  isiyo na mipaka  na Hekima Yake adhimu Anaweza kujenga na kuzididimiza katika akili hizi hisia za kustaajabisha na za kubarikiwa katika nyoyo za wanandoa. Kwa kweli Allah Subhanahu wa Ta'aala Anawakumbusha wale ambao wanatafuta ishara Zake katika ulimwengu huu kwamba hisia hizi katika moyo wa wanandoa ni katika ishara Zake ambazo zinatakiwa zimuongoze mwanaadamu katika kuwepo Kwake kama Alivyosema katika Qur-aan, (Na katika Ishara Zake ni kuwa Amekuumbieni wake zenu kutokana na nafsi zenu ili mpate utulivu kwao. Naye Amejaalia mapenzi na huruma baina yenu. Hakika katika haya bila ya shaka zipo ishara kwa watu wanaofikiri." [Ar-Ruum 30:21]
Lakini Allaah Subhanahu Wa Ta’aala Anajua kwamba moyo wa binaadamu sio kitu ambacho kiko tuli, wakati mwengine huwa dhaifu na wakati mwengine huwa na nguvu. Hisia zinaweza kubadilika na hubadilika pindi wakati unavyosogea. Mapenzi yanaweza kufifia na kupayuka mbalini. Mshikamano wa ndoa unaweza kuwa dhaifu kama haujahudumiwa vizuri. Furaha katika ndoa haiwezi kudharauliwa; furaha ya kuendelea inahitaji utowaji wa daima kutoka pande zote. Ili mti wa mapenzi ya ndoa ubaki hai na kuendelea kuishi, udongo lazima udumishwe, uhifadhiwe, umwagiwe maji na ulelewe.
Kumbuka kwamba Mtume wetu Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alipata nafasi ya kwenda kwenye majangwa na kushindana mbio na mke wake Bibi 'Aaishah. Bibi 'Aaishah alimshinda Mtume lakini baadae aliponenepa, Mtume alimshinda Bibi 'Aaishah. Kumbuka kwamba Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alimchukua mkewe kwenda kuwatazama vijana wa Ki-Ethiopia wakicheza michezo ya utamaduni wao. Maonyesho ya hisia yanahitajika kuweza kuufanya mshikamano wa ndoa usifanye kutu na kuoza. Kumbuka kwamba utapata thawabu kutoka kwa Allah (Subhanahu wa Ta'aala) kwa hisia zozote unazomuonyesha mkeo kama Mtume   (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alivyosema: ((Mmoja wenu atapata thawabu kwa chochote ambacho atafanya ili kutafuta radhi za Allaah hata kwa tonge analomlisha mkewe))
Kamwe usidharau umuhimu wa vitu vidogo vidogo kama vile kuweka chakula kwenye mdomo wa mkeo, kumfungulia mlango wa gari, na hali kadhalika. Kumbuka kwamba Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa anasogeza goti lake kwa mkewe amkanyage kuweza kumpanda ngamia.
Jaribu kutafuta wakati ili nyote wawili muweze kuswali pamoja. Kuuimarisha uhusiano kati yenu na Allaah (Subhanahu wa Ta'aala) ni hakikisho kubwa kuwa uhusiano wenu wa kindoa utabaki madhubuti. Kuwa na amani kati yenu na Allah (Subhanahu wa Ta'ala)  daima kutapelekea ndani mwenu kuwa na amani zaidi.
Kumbuka kwamba Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) aliwapa habari nzuri (aliwabashiria) wanandoa wanaoamka usiku kuswali pamoja. Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) anamsisitiza mwanandoa anayeamka mwanzo amuamshe mwenzake, japo kummwagia maji katika uso wake. 
Daima jaribu uwezavyo kuwa mtu mzuri kwa mkeo kwa njia ya maneno na vitendo. Ongea nae, mchekee, tafuta ushauri wake, muulize juu ya mawazo yake, tumia wakati maalum na yeye na daima kumbuka kwamba Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alisema: ((Wabora katika nyinyi ni wale ambao ni wabora kwa wake zao))
Mwishowe, ni kawaida kwa wanandoa kuahidi kuwapenda na kuwaheshimu wanandoa wenziwe mpaka mauti yawatenganishe. Naamini kwamba ahadi hii ni nzuri au ni bora kabisa, lakini haitoshi! Haitoshi kumpenda mkeo tu. Lazima upende anachokipenda pia. amilia yake, anaowapenda yeye uwapende pia. Usiwe kama mwenzangu mmoja ambaye hakufurahiwa kuja kwa wazazi wa mke wake kukaa kwa wiki chache. Alimwambia wazi mkewe “Mimi siwapendi wazazi wako”. Bila ya kusita mkewe alimtazama machoni kwa hasira na kusema, “Na wako pia siwapendi”.
Mapenzi yasiishe na pia tunaamini kuna maisha baada ya mauti ambapo wale ambao walifanya wema katika dunia hii wataungana na wanandoa wenzio ((Ingieni Peponi, nyinyi na wake zenu; mtafurahishwa humo)) [Az-Zukhruf 43:70] Pia wataungana na watoto wao.
Na mfano bora katika mintarafu hii itakuwa ni Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ambaye mapenzi yake kwa Bibi Khadiyjah, mkewe aliyeishi naye kwa miaka 25 yalisogea mpaka kwa wale aliowapenda Khadiyjah; mapenzi yake haya yaliendelea hata baada ya kufa Bibi Khadiyjah. Ilikuwa miaka mingi baada ya kifo cha Bibi Khadiyjah na Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) hakumsahau na kila panapochinjwa mbuzi katika nyumba yake basi hutuma kifurushi kwa familia ya Bibi Khadiyjah na marafiki zake na kila akihisi kuwa mgeni  anayegonga mlango ni Dada ya Khadiyjah aitwaye Hala, Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)  alikuwa akiomba huku akisema, "Ee Allaah Jaalia awe ni  Hala."

Mawaridi Kumi Ya Kupata Mapenzi Ya Allaah سبحانه وتعالى Na Mtume صلى الله عليه وآله وسلم




 



WARIDI LA: 1

Omba Tawbah sana kwa Allaah سبحانه وتعالى   Na  jiweke katika Twaharah daima
}}...إِنَّ اللّهَ يُحِبُّ التَّوَّابِينَ وَيُحِبُّ الْمُتَطَهِّرِينَ{{
{{…… Hakika Mwenyezi Mungu huwapenda wanao tubu na huwapenda wanao jisafisha}}
Al-Baqarah:222 


WARIDI LA:  2 
 Mfuate Mtume صلى الله عليهو آله  وسلم   kwa kutimiza Sunnah zake na fuata tabia na mwendo wake  ili  uthibitishe  mapenzi yako kwa Allaah سبحانه وتعالى

}}قُلْ إِن كُنتُمْ تُحِبُّونَ اللّهَ فَاتَّبِعُونِي يُحْبِبْكُمُ اللّهُ وَيَغْفِرْ لَكُمْ ذُنُوبَكُمْ وَاللّهُ غَفُورٌ رَّحِيمٌ    {{
{{Sema: Ikiwa nyinyi mnampenda Mwenyezi Mungu basi nifuateni mimi, Mwenyezi Mungu atakupendeni na atakufutieni madhambi yenu. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kufuta madhambi na Mwenye kurehemu}}
Al-Imraan:31

Vile vile  fuata  Sunnah za Makhalifa Wanne waliongoka, Abubakar, 'Umar, 'Uthmaan na 'Aliy
عنهما  رضي الله

WARIDI LA : 3
Timiza Fardhi yako kwanza vizuri, kisha ongeza na Sunnah zaidi za Swalah, kutoa sadaqa, kwenda Umra, kufanya kila aina ya wema kwa wazazi na Waislamu wenzako
((‏عن ‏ ‏أبي هريرة رضي الله عنه ‏ ‏قال ‏
‏قال رسول الله ‏ ‏صلى الله عليه وآله وسلم ‏ ‏إن الله قال ‏ ‏من عادى لي وليا فقد ‏‏ آذنته ‏‏ بالحرب وما تقرب إلي عبدي بشيء أحب إلي مما افترضت عليه وما يزال عبدي يتقرب إلي بالنوافل حتى أحبه فإذا أحببته كنت سمعه الذي يسمع به وبصره الذي يبصر به ويده التي يبطش بها ورجله التي يمشي بها وإن سألني لأعطينه ولئن استعاذني لأعيذنه وما ترددت عن شيء أنا فاعله ترددي عن نفس المؤمن يكره الموت وأنا أكره مساءته))

((Inatoka kwa Abu Hurayrah رضي الله عنه ambaye alisema: Mtume ‏صلى الله عليه وآله وسلم  amesema: Yeyote yule afanyae uadui kwa walii (rafiki) wangu nitatangaza vita dhidi yake.  Mja wangu hanikaribii na kitu chochote ninachokipenda kama amali nilizomuwajibisha, na mja wangu huzidi kunikaribia kwa amali njema za Sunnah ili nimpende. Ninapompenda huwa (Mimi ni) masikio yake anayosikilizia, macho yake anayoonea, mikono yake anayopigania, miguu yake anayokwendea, lau angeniomba kitu bila shaka ningempa, lau angeniomba himaya bila shaka ningempa, sisiti juu ya kitu chochote kama ninavyosita  (kuichukua) roho ya mja wangu muumin.  Anachukia mauti nami nachukia kumuumiza.))

(Al-Bukhariy)


WARIDI LA:  4

Fanya mema mengi Allaah Aridhike na wewe na wewe uridhike na uwe tayari kuondoka duniani hali ya kupenda kwenda kuonana naye.

((عن ‏ ‏أبي بردة ‏ ‏عن ‏ ‏أبي موسى ‏
‏عن النبي ‏ ‏صلى الله عليه وآله وسلم ‏ ‏قال ‏ ‏من أحب لقاء الله أحب الله لقاءه ومن كره لقاء الله كره الله لقاءه))
((Kutoka kwa Abu Musa kwamba Mtume صلى الله عليه وآله وسلم  kasema:  Atakayependa kuonana na Allaah basi Allaah Naye Atapenda kuonana naye, na atakayechukia kuonana na Allaah, basi Naye Allaah Atachukia kuonana naye))
 (Muslim)


WARDI LA:   5

Ukipendwa na Allaah سبحانه وتعالى basi utapendwa na Jibriyl na wakaazi wa mbinguni na watu wa duniani pia

((عن ‏ ‏أبي هريرة ‏
‏عن النبي ‏ ‏صلى الله عليه وآله وسلم ‏ ‏قال ‏ ‏إذا أحب الله العبد نادى ‏ ‏جبريل ‏ ‏إن الله يحب فلانا فأحببه فيحبه ‏ ‏جبريل ‏ ‏فينادي ‏ ‏جبريل ‏ ‏في أهل السماء إن الله يحب فلانا فأحبوه فيحبه أهل السماء ثم يوضع له القبول في الأرض))
((Imetoka kwa Abu Hurayrah kwamba Mtume صلى الله عليه وآله وسلم  amesema: Mwenyeezi Mungu Akimpenda mja (wake) Humuita Jibriyl na Husema: Nampenda fulani kwa hivyo (nawe) mpende.  Kisha Jibriyl humpenda.  Kisha Jibriyl huwaita wakaazi  wa mbinguni: Hakika Allaah Anampenda fulani basi na nyinyi mpendeni.  Basi hupendwa na wakaazi  wa mbinguni, kisha kupendwa kwake hujengwa duniani))
(Al-Bukhariy)


WARIDI LA:  6

Fanya wema, toa sadaka, jizuie na ghadhabu, wasamehe wenzako wanapokukosea  upate daraja ya Muhsiniyn na upendwe na Allaah سبحانه وتعالى    
}}الَّذِينَ يُنفِقُونَ فِي السَّرَّاء وَالضَّرَّاء وَالْكَاظِمِينَ الْغَيْظَ وَالْعَافِينَ عَنِ النَّاسِ وَاللّهُ يُحِبُّ الْمُحْسِنِينَ{{
{{Ambao hutoa wanapo kuwa na wasaa na wanapo kuwa na dhiki, na wanajizuia ghadhabu, na wasamehevu kwa watu; na Mwenyezi Mungu huwapenda wafanyao wema}}

(Al-'Imraan 134)


WARDI LA: 7

 Penda kusoma Suratul-Ikhlaas upate mapenzi ya Allaah سبحانه وتعالى 

((عن ‏ ‏أنس ‏أن رجلا قال والله إني لأحب هذه السورة ‏ ‏قل هو الله أحد ‏ ‏فقال رسول الله ‏صلى الله عليه وآله وسلم ‏‏ حبك إياها أدخلك الجنة
الترمذي وصححه الألباني

Imetoka kwa Anas ambaye alisema: Mtu mmoja alimwambia Mtume صلى الله عليه وآله وسلم "Mimi naipenda sura hii  قُلْ هُوَ اللَّهُ أَحَد akasema Mtume صلى الله عليه وآله وسلم  “Mapenzi yako kwayo yatakuingiza peponi”

At-Tirmidhiy na  Imesahihishwa na Albaaniy
(Hapa tufahamu kuwa Suratu Ikhlaas ni sehemu ya Qur’an, na ni vizuri kuisoma Qur’an yote na usitosheke na Surah moja au baadhi na ukaacha zingine kwa kuichukua hadiyth hiyo peke yake bila kutazama na zingine).


WARIDI LA: 8
  Mpende Allaah سبحانه وتعالى  , Mtume صلى الله عليه وآله وسلم  na Makhalifa wake wote Wanne Abubakar, 'Umar, 'Uthmaan na ‘Aliy رضي الله عنهما  upate kuwa nao.

((عن ‏ ‏أنس ‏ ‏رضي الله عنه ‏
‏أن رجلا سأل النبي ‏ ‏صلى الله عليه وآله وسلم ‏ ‏عن الساعة فقال متى الساعة قال وماذا أعددت لها قال لا شيء إلا أني أحب الله ورسوله ‏ ‏صلى الله عليه وسلم ‏ ‏فقال ‏ ‏أنت مع من أحببت قال ‏ ‏أنس ‏ ‏فما فرحنا بشيء فرحنا بقول النبي ‏ ‏صلى الله عليه وسلم ‏ ‏أنت مع من أحببت
‏قال ‏ ‏أنس ‏ ‏فأنا أحب النبي ‏ ‏صلى الله عليه وسلم ‏ ‏وأبا بكر ‏ ‏وعمر ‏ ‏وأرجو أن أكون معهم بحبي إياهم وإن لم أعمل بمثل))
((Imetoka kwa Anas ‏رضي الله عنه ambaye alisema:
Alikuja mtu mmoja akamuuliza Mtume صلى الله عليه وآله وسلم  kuhusu saa (Qiyaamah) akauliza: Lini Qiyaamah? Akamuulize je, Kwani umekitayarishia nini?  Akasema: sikutayarisha kitu isipokuwa mimi nampenda Allaah na Mtume wake صلى الله عليه وسلم
Akasema: basi wewe uko pamoja na unayempenda.  Anas akasema: Hatukufurahiwa na jambo kama tulivyofurahiwa na usemi huu wa Mtume صلى الله عليه وآله وسلم "wewe uko pamoja na unayempenda" Akasema Anas: "Basi mimi nampenda Mtume صلى الله عليه وآله وسلم na Abubakar, na 'Umar na natumai niwe pamoja nao kwa mapenzi yangu juu yao japo kama sikufanya kama walivyofanya wao"))

(Al Bukhariy)


WARIDI LA: 9

Kuwa na Tawakkul katika mambo yako yote, umuweke Allaah سبحانه وتعالى   mbele ya kila jambo, na unapotaka kufanya jambo, kwanza tafuta ushauri kwa watu wema, kisha swali istikhaara, kisha Tawakkal kwa Allaah سبحانه وتعالى   

}}شَاوِرْهُمْ فِي الأَمْرِ فَإِذَا عَزَمْتَ فَتَوَكَّلْ عَلَى اللّهِ إِنَّ اللّهَ يُحِبُّ الْمُتَوَكِّلِينَ{{

{{ Shauriana nao katika mambo. Na ukisha kata shauri basi mtegemee Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu huwapenda wanao mtegemea}}

Al-Imraan: 159


WARIDI LA: 10

Kuwa na tabia njema na watu kama, upole, ukarimu, heshima, ucheshi, adabu nzuri upate kuwa karibu na Mtume صلى الله عليه وآله وسلم siku ya Qiyaamah.
  (( عن أبي جده ‏أنه سمع النبي ‏ ‏صلى الله عليه وآله وسلم ‏ ‏يقول ‏ ‏ألا أخبركم بأحبكم إلي وأقربكم مني مجلسا يوم القيامة فسكت القوم فأعادها مرتين ‏ ‏أو ثلاثا ‏ ‏قال القوم نعم يا رسول الله قال أحسنكم خلقا))
(احمد) 
((Imetoka kwa Abi Jidduh   kwamba amemsikia Mtume صلى الله عليه وآله وسلم akisema:  Je, nikujulisheni nani kipenzi kwangu na nani atakayekuwa karibu yangu siku ya Qiyaama?  Wakanyamaza watu wote, akarudia mara mbili au tatu, wakasema watu: "ndio ewe Mtume صلى الله عليه وآله وسلم akasema: mwenye tabia njema katika nyinyi))
(Ahmad)