Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR
limetahadharisha juu ya hali mbaya inayowakabili Waislamu wa Myanmar.
Taarifa ya UNHCR imeeleza kuwa, karibu Waislamu elfu sabini na tano
wanaishi katika mazingira hatarishi kwenye kambi za muda nchini humo.
Waislamu hao wameamua kuhama makaazi yao na kukimbilia kwenye maeneo ya
amani, baada ya Mabuda wenye misimamo ya kufurutu mipaka wakiungwa mkono
na vikosi vya serikali ya nchi hiyo kuwasaka na kuwaua kwa halaiki.
Taarifa zinaeleza kuwa, Waislamu hao wanakabiliwa na hali mbaya sana ya
kiafya na lishe duni kwenye kambi zao za muda zilizoko umbali wa
kilomita 500 kutoka mji mkuu wa nchi hiyo. Hata hivyo vitisho vingali
bado vinaendelea vya watu wanaobeba silaha dhidi ya Waislamu laki nane
walioko katika eneo la kaskazini mwa Myanmar. Watu hao wanaobeba silaha
waliwaua kwa halaiki Waislamu wapatao 90 kutoka katika vijiji mbalimbali
yapata miezi minne iliyopita.
Sunday, September 30, 2012
Kamanda wa waasi Syria auawa na wafuasi wake
Kamanda wa waasi wa Syria wanaoungwa mkono wa madola ya kigeni
ameuawa na wafuasi wake wenye silaha waliomgeuka katika mji wa Dara'a.
Rabea Swaidan aliuawa kwenye mji huo kusini mwa Damascus hapo jana na
wafuasi wake wakati walipokuwa wakigombania kugawana vitu walivyopora na
fedha walizopokea kutoka nje ya nchi kwa ajili ya kuendeleza shughuli
zao haramu.
Wakati hayo yakiripotiwa vikosi vya serikali ya Syria vimedhibiti maeneo
zaidi katika mji wa Aleppo yaliyokuwa yakikaliwa na magenge yenye
silaha yanayoungwa mkono na madola ya nje, huku waasi 180 wakiuawa na
wengine 30 kukamatwa. Maeneo hayo yamedhibitiwa katika operesheni kubwa
ya kijeshi ya serikali dhidi ya waasi wanaopigana dhidi ya serikali ya
Rais Bashar al Assad wa Syria.
Walibya wakabidhi mamia ya silaha kwa jeshi
Saturday, September 29, 2012
Ikhwan: Hakuna mwafaka kati ya Israel na Misri
Katibu Mkuu wa Harakati ya Ikhwaanul Muslimiin nchini Misri amesema kuwa, Rais Muhammad Mursi wa nchi hiyo hatakutana na kufanya mazungumzo na kiongozi yeyote wa utawala wa Kizayuni wa Israel. Mahmoud Hussein amesema kuwa, Rais Mursi hatakutana na kiongozi yeyote wa utawala wa Israel hata kama ikiwa ni kuufanyia marekebisho mkataba wa amani wa Camp David. Mahmoud Hussein amesisitiza juu ya kukomeshwa uchokozi unaofanywa na utawala huo ghasibu dhidi ya wananchi wa Palestina wa eneo la Ukanda wa Gaza, sanjari na kusimamishwa kikamilifu ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni katika eneo la Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan. Katibu Mkuu wa Ikhwaanul Muslimiin amesema, hakuna kiongozi yeyote wa Misri atakayefanya mazungumzo na kiongozi wa Israel hadi pale zitakapodhaminiwa haki za wananchi wa Palestina.
Waislamu Ethiopia waandamana dhidi ya serikali
Maelfu ya Waislamu wa Ethiopia wamefanya maandamano makubwa kwenye miji mbalimbali ya nchi hiyo wakipinga siasa za serikali ya Adiss Ababa. Waislamu wa Ethiopia wanaituhumu serikali ya nchi hiyo kwa kuingilia kati masuala ya dini hiyo na hali kadhalika ikifanya njama za kuwashinikiza Waislamu wafuate mikikati iliyopangwa na serikali. Malalamiko ya Waislamu dhidi ya siasa na sera za serikali ya nchi hiyo yameanza tokea miezi tisa iliyopita. Waandamanaji walilaani vikali mipango ilyoratibiwa na serikali ya kuwachagulia viongozi wa kidini kinyume na irada na matakwa ya Waislamu walio wengi nchini humo. Hali kadhalika waandamanaji wametaka waachiliwe huru vingozi wao wanaoshikiliwa na vyombo vya dola nchini humo.
UAMSHO YABAINISHA SABABU ZA MASHEHE KUSHIRIKI KUDAI UHURU WA ZANZIBAR
waislamu na waznzibar kote nchini wametakiwa kufuata mfumo aliouweka Allah kwa waja wake kwa lengo la kupata mafanikio mema hapa duniani na kujiepusha na adhabu huko akhera
wito huo umetolewa leo na shekh Khalfan Nassor katika mhadhara uliofanyika katika viwanja vya masjid salami magogon wilaya ya maghrib unguja. Aidha amewasihi viongozi walioko madarakan kutumia madaraka yao kwa uadilifu na kulinda haki za wale wanaowaongoza na kusisitiza kuwa mashehe hawana nia ya kuwaondosha madarakani katika nyadhifa zao bali ni jukumu lao kufikisha ujumbe wa allah kwa waumin wote wakiwemo na
Tuesday, September 25, 2012
Mahakama ya Misri yawahukumu kifo magaidi 14
Mahakama ya Misri imewahukumu kifo magaidi 14 na wengine wanne
kifungo cha maisha jela kwa kosa la kushambulia jeshi na maafisa wa
polisi katika rasi ya Sinai.
Watu hao ni wafuasi wa kundi moja la wanamgambo ambao wamepatikana na hatia ya kuwaua maafisa watatu wa polisi, mwanajeshi mmoja na raia katika mashambulizi yaliyofanywa mwezi Juni na Julai mwaka 2011.
Eneo la Sinai la Misri kwa muda mrefu limekuwa likikabiliwa na matatizo ya kiuslama. Mwezi Agosti mwaka huu jeshi la Misri lilianzisha operesheni kali ya kuimarisha usalama kwenye eneo hilo baada ya watu wasiojulikana kuuwa askari 16 wa mpakani wa Misri.

Kufunguliwa mpaka kati ya Kodivaa na Ghana
Monday, September 24, 2012
MAALIM SEIF ONYA VIONGOZI WANAOVURUGA AMANI
KATIBU Mkuu wa Chama cha wananchi (CUF) Maalim
Seif Sharif Hamad, amesema kuna baadhi ya viongozi ndani ya Zanzibar,
hawafurahishwi na hali ya amani na utulivu iliyoko katika Visiwa hivyo.
Amesema kiongozi anayesajiisha wananchi kukataa umoja na
mashirikiano ya wananchi, anakusudia kuirejesha Zanzibar katika matatizo
na wananchi wake kuishi kwa uhasama na ugomvi kila siku.
Maalim Seif, alieleza hayo katika mkutano mkubwa wa hadhara wa CUF
uliyofanyika jana jioni katika Jimbo la Bububu, nje ya mji wa Zanzibar.
Maalim Seif, alikuwa nje ya Zanzibar, wakati wa kampeni za uchaguzi wa
Jimbo hilo.
Akifafanua hotuba yake Maalim Seif, alisema kuna viongozi ambao
wanawaambia wananchi wakatae mashirikiano ya chini na mashirikiano
yabaki kwa viongozi wa juu, “vipi anawaambia watu kauli hiyo,”? alihoji
Maalim Seif:
“Sikuwepo katika kampeni lakini nimeona kapitia facebook na kila
kitu nakiona lakini niliporudi nikaletewa CD moja kampeni ya ufunguzi wa
kampeni ya CCM na CUF na kuangalia nataka niseme,” alisema na kuongeza:
Al Shabab yakiri kumuua mbunge wa Somalia
Wanamgambo wa kundi la al Shabab wa Somalia wamesema kuwa wao ndio
waliomfyatulia risasi na kumuua mbunge wa Somalia hapo jana na kutishia
kumuua kila mbunge wa nchi hiyo. Watu waliokuwa na silaha jana walimuua
kwa kumfyatulia risasi Mustafa Haji Mohamed nje ya nyumba yake baada ya
sala ya Ijumaa. Sheikh Abdiasis Abu Musab msemaji wa oparesheni za
kijeshi wa kundi la wanamgambo wa al Shabab amesema kwa kuhoji kuwa ni
mara ngapi wamewaonya Wasomalia kujiunga na serikali ya kikafiri?
Msemaji wa al Shabab amesema wamemuua mbunge Mustafa na kwamba watawaua
wabunge wote na maafisa wa Somalia. Augustine Mahiga Mjumbe Maalumu wa
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia ameyaelezea mauaji ya
mbunge huyo yaliyofanywa na al Shabab kuwa ni kitendo cha woga
kinachokumbusha changamoto zinazozikabili taasisi mpya na uongozi wa
nchi hiyo.
Sunday, September 23, 2012
Wanigeria waandamana kumtetea Mtume SAW
Makumi ya maelefu ya watu wamefanya maandamano makubwa katika mji
wa pili kwa ukubwa Nigeria wa Kano kulaani vitendo vya kumvunjia
heshima Mtume Muhammad SAW.
Waandamanaji wametoa nara kama vile ‘Mauti kwa Marekani’, ‘Mauti kwa Israel’ na ‘Mauti kwa Maadui wa Uislamu’. Mmoja kati ya viongozi wa Harakati ya Kiislamu iliyoandaa maandamano hayo Sheikh Mohammad Turi amesema Waislamu wa Nigeria wamejitokeza kubainisha upinzani wao kwa filamu na vijikatuni vilivyomvunjia heshima Mtume Muhammad SAW.
Nchini Ufaransa jeshi la polisi limewazuia Waislamu kuandamana kupinga kuvunjiwa heshima matukufu ya Kiislamu. Nchi hiyo ya Ulaya sasa imegeuka na kuwa kitovu cha chuki dhidi ya Uislamu.
Wakati huo huo Waziri wa Reli nchini Pakistan Ghulam Ahmad Bilour amesema atatoa zawadi ya dola $ laki moja kwa yeyote atakayemuua mtengenezaji wa filamu ya hivi karibuni inayomvunjia heshima Mtume SAW.

Saturday, September 22, 2012
Waislamu TZ walaani filamu inayomtusi Mtume SAW
Maelfu ya Waislamu katika mji wa Dar
es Salaam, Tanzania wameandamana kulaani filamu inayomtusi na kumvunjia
heshima Mtume saw. Waislamu hao waliokuwa wakipiga nara dhidi ya
Marekani waliandamana hapo jana na kutoa tamko dhidi ya wanaoshambulia
na kuudhalilisha Uislamu. Akitoa tamko la Waislamu mwishoni mwa
maandamano hayo, Sheikh Ponda Issa Ponda, Katibu Mkuu wa Shura ya
Maimamu Tanzania, ameitaka serikali ya Tanzania kuzuia mitandao ya
intaneti, DVD na mianya mingine kuonyesha filamu hiyo ya kumvunjia
heshima Mtume, sambamba na kutaka kufungwa ubalozi wa Marekani nchini
humo. Aidha Sheikh Ponda Issa Ponda amesema kuwa, tamko hilo ni la
Waislamu wote wanaompigania Mtume na kwamba, kuanzia sasa Waislamu
wanagomea bidhaa zote zinazotengenezwa na Marekani pamoja na utawala wa
Kizayuni wa Israel. Ameongeza kwamba, ubalozi wa Marekani nchini
Tanzania unapaswa kufungwa mara moja, la sivyo Waislamu wa nchi hiyo
watachukua hatua kali zaidi.
Friday, September 21, 2012
Sudan mbili zakubaliana kubadilishana wafungwa
Sudan na Sudan Kusini zimekubaliana juu ya hatua ya
ubadilishanaji wafungwa wa nchi mbili. Hayo yamesemwa na Waziri wa Mambo
ya Ndani wa Sudan Ibrahim Mahmood Hamid alipokutana na kamishna wa
Sudan Kusini katika masuala ya ujenzi mpya na miundo mbinu mjini
Khartoum. Viongozi hao wawili wamekubaliana kubadilishana wafungwa na
kuwarejesha nchini mwao sambamba na kuhukumiwa kwa mujibu wa hukumu za
nchi hiyo. Katika kikao hicho pia walijadili kuondolewa vizuizi
vilivyopo kwa ajili ya kuwarejesha raia wa Sudan Kusini kutoka nchini
Sudan. Katika kipindi cha kujitenga Sudan Kusini kutoka Sudan kaskazini
tarehe tisa mwezi Juni 2011, zilianza harakati za kuwahamisha raia wa
nchi mbili katika maeneo yao ya asili, suala lililopelekea maelfu ya
raia wa nchi mbili hizo kurejea makwao.
Ujerumani na Tanzania zasaini mkataba wa mashirikiano usafiri wa anga
Thursday, September 20, 2012
Kauli ya UAMSHO dhidi ya film
ADHABU YA ALLAH INAMSTAHILIA ALOMTUKANA MTUME (S.A.W) KAMA ZINAVYOMSTAHILIA MWENYE KUUWA WASIOKUWA NA HATIA
Kila sifa njema zinamstahikia Allah (S.W.) Muumba Mbingu na Ardhi Mfalme wa wafalme asiyeshindwa na kitu; sala na salamu zimuendee kipenzi cha Umma, Mtume Muhammad (s.a.w). Aliyeletwa kuwa ni Rehma kwa walimwengu wote na aliyekuwa kasifiwa na Mola wetu kuwa ameshikamana na sifa nzuri na vitendo vizuri kabisa.Kwa utukufu alopewa Mtume (s.a.w) ni muujiza wa kutosha kwa mwenye kuzingatia kiasi ambacho hauathiriki utukufu wake kwa maneno ya wajinga bali hudhalilika msemaji na kuzidi kutukuka mtukufu wa daraja Mtume (s.a.w) na kwanini asitukuke wakati ametukuzwa na yeye Allah (S.W.) utukufu usio kifani pale alipomwambia:
“..Kwa hakika wewe Muhammad una Tabiya ADHIYM..”
Ndugu wa Kiislaam,
Inasikitisha sana kuona kuwa kuna baadhi ya Waislaam ambao ni watu wepesi kiasi cha kuweza kuchokozwa na wajinga wasio na thamani wakajiingiza katika mitego na vitendo vyao vikawashirikisha pia Waislam wasiokubaliana na vitendo vyao viovu. Daima Mwislamu anatakiwa awe katika haki; asimuasi Mwenyezi Mungu ili kuepukana na ghadhabu zake Allah (S.W.).
Uislaam ni dini ilokamilika kwa kumdhaminia mwanaadamu ufumbuzi na miongozo ya mambo yote katika maisha yake ya Dunia na ndio maana Allah (S.W.) kakitukuza Kitabu chake kwa kusema:
“…hatujaacha kitu katika kitabu hichi…”
Tukizingatia tutaona kuwa watu waovu kuibuka kila baada ya muda na kumtukana Mtume (s.a.w) au kuutukana Uislaam si jambo geni ni ukafiri wa wazi na uadui ulioanza tokea siku ya mwanzo ya kupewa Utume na kuanza kuufikisha kwa watu wake yeye mwenyewe Mtume (s.a.w) na kwa bahati, aliyeanza hujuma na dharau hizo alikuwa mtu wa karibu wa damu kabisa na Mtume (s.a.w) na haikuwa kumkanusha tu bali alifikia hadi kumuombea maangamizo kwa maneno mashhuri aliposema Abuulahab:
“..maangamizo yakufike, hili ndio ulotukusanyia…!”
Mbali ya kupigwa mawe na mengine mengi tu, la umuhimu ni kujifunza kutoka kwake (s.a.w.) na vile vile maandiko ya Qur-aan.
Ni sahihi kabisa kuwa amelaanika na kuangamia yule mwenye kumtusi Mtume (s.a.w.) ndio tukaona hakusalimika jamaa yake Mtume (s.a.w) wa damu, bwana Abuulahab, Allah akashusha sura nzima ya maangamizo akaanza kwa kusema:
“Imeangamia mikono ya Abulahab na kuangamia na yeye mwenyewe…”
Lakini je! ni sahihi kuuwawa maquraysh wa makka kwa kosa lake? Jawabu: aya hazikushuka kuwalaani Makuraysh wote, si wa ndani hapo Makka, seuze waliokuweko nje seuze wale ambao wamo katika dhimma na hifadhi za Waislamu; ikiwa kosa la Abulahab hakuadhibiwa mwengine basi ni wazi kuwa hakuna uhalali wa Waislamu kwa kosa la watu kumkejeli Mtume (s.a.w) kuwahujumu wasiohusika na wasiokuwa na hatia.
Kuvamia Ubalozi wa Marekani hukoBenghazi nchini Libya ni kosa kwa pande nyingi tu kwani Allah (S.W.) anasema:
“…wala hatobeba mkosaji dhambi ya mwengine…”
Kosa la kumkejeli Mtume (s.a.w) haijawa halali kufanya ndio sababu ya kutenda vitendo vya uadui.
Allah (S.W.) ametufunza hayo ndani ya Qur-aani kwa kusema:
“… wala makosa ya watu ya kukuzuiyeni msiingie masjidi ‘lharami yasikufanyeni mkatenda uadui na kuchupa mipaka…”
Ubaya mkubwa zaidi ni kuhatarisha roho za watu ambao wako chini ya dhimma zetu kwani kila balozi na wafanya kazi wake huwa katika hifadhi ya nchi waliokuweko. Hivo leo tutafurahia kusikia balozi wa Libya nae anavamiwa na kuuwawa na familia yake nchi yoyote aliko?
TUNALAANI TUNALAANI NA KUKEMEA KWA NGUVU ZOTE KWA KEJELI DHIDI YA MTUME MUHAMMAD S.A.W. ILOFANYWA NA MAKUNDI YANAYOTAKA KUPANDIKIZA MBEGU ZA FITNA NA UCHOCHEZI WA VITA, PIA TUNAKEMEA KITENDO CHA KUULIWA BALOZI NA WATENDAJI WAKE WASIO NA HATIA, NA PAMOJA NA MATENDO YOTE YA UHARIBIFU YANAYOFANYWA DUNIANI KOTE KISHA KUNASIBISHWA NA UISLAMU AMBAO UKO MBALI NA DHULMA NA UADUI HUO.
Pia tunamuomba Allah (s.w) awaangamize na kuwadhalilisha wale wote walochangia kwa njia moja au nyengine kutengeneza Fitna hiyo.
Hakika Mtume (s.a.w) ni Rehma ilioletwa hapa ulimwenguni akishushiwa ndani ya Qur-ani:
“…na hatukukupeleka wewe Muhammad illa uwe ni rehma kwa walimwengu…”
Rehma hii ni mafunzo alotuachia Mtume (s.a.w) yatakayowavutia wasiokuwa Waislamu kutaka kuujuwa Uislamu wala hatutokuwa rehma kwa matendo maovu acha mauwaji. Tufuate sira yake Mtume ya kuwa na sifa nzuri na vitendo vizuri.
Tunamshukuru Mola kwa neema Zake na ulinzi Wake.
Sh. FARID HADI AHMED
MSEMAJI MKUU WA UMOJA WA JUMUIYA
NA TAASISI ZA KIISLAMU ZANZIBAR 18/9/2012

Al Azhar yalaani kuvunjiwa heshima Mtume SAW
Shekhe Mkuu wa Al Azhar, Ahmed al-Tayyeb amelaani vikali hatua ya
jarida moja la Ufaransa kuchapisha tena vijikatuni vinavyomdhalilisha
na kumtusi Nabii Muhammad SAW.
Vijikatuni hivyo vimechapishwa katika jarida la kila wiki la Charlie Hebdo la Ufaransa. Wakati huo huo Jumuiya ya Nchi za Kiarabu imetoa wito kwa Waislamu kote duniani kufanya maandamano makubwa ya amani ya kulaani uchapishaji wa vijikatuni hivyo.
Jarida hilo la Ufaransa limethubutu kufanya kitendo hicho kichafu huku Waislamu wakiendelea kuandamana kote duniani kulaani utengenezaji wa filamu inayomvunjia heshima Mtume SAW huko Marekani.

Sudan mbili kukamilisha mazungumzo Ethiopia
Rais Omar Hassan al-Bashir wa Sudan anatarajiwa kufanya
mazungumzo ya ana kwa ana na mwenzake wa Sudan Kusini Salva Kiir siku ya
Jumapili wakati wa kikao cha mwisho cha pande mbili ambacho kimechukua
muda wa majuma mawili. Kikao hicho kilichowashirikisha wawakilishi
kutoka Juba na Khartoum kililenga kutatua mivutano kati ya serikali
mbili hizo kuanzia suala la ugawanaji sawa wa pato la mafuta hadi kadhia
ya usalama wa mipakani. Mkuu wa timu ya Mazungumzo ya Sudan Kusini,
Pagan Amum amethibitisha kuwa kikao hicho kitafanyika mjini Addis Ababa.
Mjumbe maalum wa Norway huko Sudan na Sudan Kusini, Endre Stiansen
amesema jamii ya kimataifa imefurahishwa na jinsi mazungumzo ya pande
mbili yalivyokwenda ndani ya majuma mawili yaliyopita na kwamba Umoja wa
Mataifa una matumaini ya kusainiwa makubaliano ya kudumu kati ya Sudan
na Sudan Kusini kuhusu usalama wa mpakani wakati wa mkutano wa Jumapili
kati ya Marais Omar al-Bashir na Salva Kiir.
Monday, September 17, 2012
OIC kukabiliana na dharau dhidi ya Mtume (saw)
Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi wanachama katika Jumuiya ya
Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) watajadili njia za kukabiliana na vitendo
vya dharau na kumvunjia heshima Mtume Muhammad (saw).
Balozi na mwakilishi wa Iran katika Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) Hamid Reza Dahqani amesema kuwa mawaziri hao watajadili njia za kukabiliana na dharau na vitendo vya kuyavunjia heshima matukufu ya Kiislamu katika mkutano wao wa 39 utakaofanyika nchini Djibouti na ule utakaofanyika katika Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York.
Ameashiria mikono ya nyuma ya pazia iliyohusika katika kuvunjia heshima matukufu ya Kiislamu na kusema kuwa, Wamagharibi daima wamekuwa wakidai kuwa masuala hayo yanatokana na uhuru wa kusema na kujieleza katika katiba za nchi zao. Dahqani ameongeza kuwa taasisi za kimataifa zinasisitiza juu ya udharura wa kuheshimiwa dini za mbinguni, thamani na itikadi za mataifa mbalimbali lakini inasikitisha kuwa hadi sasa juhudi za jumuiya za kutetea haki za binadamu na jumuiya za kimataifa ikiwemo OIC hazijafanikiwa kuwakinaisha Wamagharibi kuhusun ukweli kwamba uhuru hauna maana ya kuvunjia heshima matukufu ya itikadi za watu wengine.

Watu 45 wauawa katika mapigano nchini Somalia
Watu wasiopungua 45 wameuawa na wengine zaidi ya 60 kujeruhiwa
katika mapigano yaliyotokea kusini mwa kijiji cha Bibi kati ya majeshi
ya Kenya na Somalia kwa upande mmoja dhidi ya wapiganaji wa kundi la al
Shabaab.
Mapigano hayo yametajwa kuwa ndiyo makali zaidi kutokea huko kusini mwa Somalia tangu majeshi ya Kenya yaingie nchini humo mwezi Oktoba mwaka jana.
Mapigano baina ya pande hizo mbili yalishadidi zaidi baada ya jaribio la majeshi ya Kenya na Somalia la kutaka kuingia katika ngome za kundi la al Shabaab karibu na kijiji cha Bibi.
Hadi sasa hakujatolewa habari kamili kuhusu idadi kamili ya watu waliouwa katika mapigano hayo kutoka pande zote mbili lakini vyombo vya kuaminika vinasema makumi ya watu wameuawa.
Duru za kundi la al Shabaab zinasema kuwa ndege za kijeshi za Kenya zinashiriki katika mapigani hayo makali.

Sunday, September 16, 2012
SHEH AZZAN AMEWATAKA WAZANZIBAR KUSHIKAMANA NA MAFUNZO YA UISLAMU KATIKA UKOMBOZI WA ZANZIBAR..
Jumuiya ya uamsho na mihadhara ya kiislamu Zanzibar imeendelea na harakati zake za kuitakia mema nchi ya zanzibar ili iweze kuwa na uhuru wa kujiamulia mambo wanayotaka.
Hayo yameeelezwa katika mhadhara uliofanyika magogoni katika msikiti wa msumbiji. kwa upande wake naibu amiri wa jumuiya hiyo sh Azzan bin khalid amesema ni wajibu wa kila muislamu kutekeleza wajibu wa kuletwa duniani ili kuweza kufanikiwa siku ya malipo.
Amewataka wazanzibar kuwa na mshikamano na kuwacha sera za vyama vyao ili kuweza kuondoa dhulma inayofanywa na serikali ya muungano wa tanzania.
Aidha naibu amiri wa jumuiya hiyo amebainisha kuwa muda wa kuikomboa zanzibar kupitia mafunzo ya kiislamu umefika hivyo wazanzibar wanatakiwa wasiogope mbinu na vitisho ambavyo vanatolewa na serikali.
Katika mhadhara huo sh Azzan amelaani vakali vitendo ambavyo vimefanywa na maadui wa uislamu duniani vya kumdhalilisha Mtume Muhammad S.A.W vinavyoongozwa na Marekani na Israel.
Akizungumzia juhudi za Jumuiya katika suala zima la kuitetea Zanzibar amesema ni kumuandikia barua ya wazi yenye kurasa 14 Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt Jakaya Mrisho Kikwete inayoelezea mustakbali wa Zanzibar.
Nae sh Mselem amesema kwa walipofikia wazanzibar kwasasa ni vigumu kurudi nyuma katika kudai hadhi ya nchi yao hivyo amesisitiza kwamba juhudi za kuitafutia heshima zanzibar zitaendelea..
Wakati huo huo kumejitokeza kikundi cha watu wasiojuilikana na kuchoma moto maskani ya ccm iliopo kariakoo inayojuilikana kwa jina la Kachorora. wanamaskani hiyo wamehusisha tukio hilo na harakati za jumuiya ya uamsho kwa kuwa tukio hilo limetokea wakati wa kurudi katika mhadhara wao lakin sh mselem kwa niaba ya jumuiya amekanusha dai hilo licha ya kwamba kuna baadhi ya vyombo vya habar haraka vimeihusisha uamsho katika tukio hilo.hivyo ameliomba jeshi la polisi kufanya uchunguzi ili Kuweza kuwachukulia hatua za kisheria wale wote waliohusika na tukio hilo.
Watu wasiojulikana Wameitia Moto Maskani ya Kachorora.
Askari wa Kikosi za Zimamoto Zanzibar wakiwa katika zoezi la kuuzima
moto uliokuwa wakiwaka katika maskani ya Kachorora Rahaleo unaosadikiwa
kutiwa na watu wasiojulikana usiku wa jana katika maskani hiyo na
kusababisha hasara ya mali ya moja ya duka la kutengeneza makochi katika
maskani hiyo.
Wananchi wakishughudia moto uliokuwa ukiunguza mali katika maskani ya Kachorora juzi usiku.
Mabaki ya Duka la kutengeneza makochi katika maskani hiyo kama inavyoonekana pichani.
Moja ya Uharibifu uliotokea katika maskani hiyo
Saturday, September 15, 2012
Hizbullah: Yaitisha maandamano makubwa Lebanon
Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon
imeitisha maandamano makubwa zaidi nchini humo kulaani hatua ya
kuvunjiwa matukufu ya dini ya Kiislamu.
Maandamano hayo yenye lengo la kutetea matukufu ya Kiislamu yanatarajiwa kufanyika Jumatatu ijayo mjini Bairut, Lebanon. Hivi karibuni pia Waislamu mjini Bairut walifanya maandamano makubwa wakilaani filamu iliyomtusi mtukufu Mtume Muhammad (sww) na kuutaka ulimwengu wa Kiislamu uchukue hatua kali za kukabiliana na njama za Marekani. Aidha hapo jana raia mmoja wa Lebanon aliuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa baada ya waandamanaji waliokuwa wamejawa na hasira kali kutaka kuvamia hoteli moja ya Kimarekani nchini humo. Mbali na Lebanon nchi nyingine za Kiislamu kamavile Misri, Libya, Bahrain, Tunisia, Yemen, Iran, Indonesia na Palestina zilishuhudia maandamano makubwa huku idadi ya watu wakiuawa na kujeruhiwa vibaya.

Wanajeshi wa Marekani wawasili San'aa, Yemen
Duru moja ya kuaminika imeripoti kuwa, wanajeshi wa Marekani
wamewasili huko San'aa mji mkuu wa Yemen. Duru hiyo imeripoti kuwa,
wanajeshi 150 wa kikosi cha majini wa Marekani wamewasili katika uwanja
wa ndege wa San'aa wa nchi hiyo na ndege moja ya kijeshi ya Marekani.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo, wanajeshi hao wa Marekani wamewasili huko
San'aa Yemen ili kuulinda ubalozi wa nchi yao na kulinda maslahi ya
Washington nchini humo. Mitaa minne inayoelekea katika ubalozi wa
Marekani mjini San'aa jana ilishuhudia maandamano makubwa ya Wayemeni
dhidi ya Marekani, na baadae maandamano hayo yaligeuka na kuwa ghasia
baada ya vikosi vya usalama vya Yemen kuingilia kati na kusababisha raia
wanne kuuawa na wengine zaidi ya 30 kujeruhiwa.
Maandamano hayo yalifanyika kufuatia kutengenezwa filamu huko Marekani inayomvinjia heshima Mtume Muhammad s.a.w. Watu walioshuhudia wameleza kuwa, wanajeshi wa Marekani waliwafyatulia risasi raia wa Yemen kutokea ndani ya ubalozi na kuwauwa. Mji wa Taiz pia huko Yemen leo umeshuhudia maandamano makubwa ya wananchi dhidi ya filamu hiyo ya udhalilishaji ya Marekani iliyotengenezwa na Sam Bacile.

UN yatahadharisha kuhusu umaskini barani Afrika
Umoja wa Mataifa umetahadharisha kuhusu umasikini
katika nchi za kusini mwa jangwa kubwa la Afrika. David Gressly Mratibu
wa Masuala ya Haki za Binadamu wa nchi za kandokando mwa jangwa la
Sahara wa umoja wa Mataifa ameripoti kuwa, maisha ya watu milioni 50
yako hatarini kutokana na uwezekano wa kupungua mazao ya kilimo mwakani.
Gressly ameongeza kuwa kunyesha mvua katika nchi za
kandokando mwa jangwa la Sahara ni ishara ya kuwepo mazao mazuri mwaka
ujao hata hivyo kupungua kwa mazao na pia kupanda kwa bei za vyakula
kutayaweka hatarini maisha ya watu milioni kumi wa eneo hilo.
Mratibu wa Masuala ya Kibinadamu katika nchi za kandokando
mwa jangwa la Sahara wa Umoja wa Mataifa amesema kuwa, tayari wameandaa
mpango wa kupunguza lishe duni kwa watoto wa Kiafrika milioni moja. Hii
ni katika hali ambayo, mwaka uliopita watoto laki tano wa Kiafrika
walikuwa wakisumbuliwa na tatizo la lishe duni. Friday, September 14, 2012
Hasira ya ulimwengu wa Kiislamu dhidi ya filamu inayomdhalilisha Mtume (saw)
Wimbi la malalamiko na hasira za Waislamu dhidi ya filamu
inayomdhalilisha Mtume Muhammad (saw) linazidi kuenea katika maeneo
mbalimbali ya dunia.
Baada ya mauaji ya balozi wa Marekani na wanadiplomasia wengine watatu wa nchi hiyo katika mji wa Benghazi huko Libya maelfu ya Wamisri waliokuwa na hasira wameendelea kuuzingira ubalozi wa Marekani mjini Cairo kwa siku kadhaa. Wamisri 250 walijeruhiwa baada ya polisi kuingilia kati.
Mjini Sanaa Yemen vijana waliokuwa na hasira jana Alkhamisi walivamia ubalozi wa Marekani na kupanda juu ya ukuta wa uzio wake ambako walitundika juu bendera yenye jina tukufu la Mtume wa Mwenyezi Mungu, Muhammad (saw). Askari usalama wa Yemen walishambulia maandamano hayo makubwa na kuua watu wanne kati ya waandamanaji hao.
Wananchi wa Saudi Arabia pia wamefanya maandamano katika maeneo tofauti ya nchi hiyo wakilaani filamu ya Kimarekani inayomtusi na kumvunjia heshima Mtume wa Mwenyezi Mungu. Wasaudia wametoa wito wa kufukuzwa balozi wa Marekani nchini kwao.
Maandamano makubwa kama hayo yamefanyika pia katika nchi za Lebanon, Palestina, Tunisia, Morocco, Pakistan, Afghanistan, Indonesia, Sudan na kwengineko ambako Waislamu wamelaani vikali filamu ya matusi inayomvunjia heshima Mtume Muhammad (saw) iliyotengenezwa na raia wa Marekani na Israel na kufadhiliwa na Mayahudi 100.
Hapa nchini Iran maelfu ya watu walifanya maandamano jana mbele ya ubalozi wa Uswisi unaolinda maslahi ya Marekani mjini Tehran wakitangaza hasira yao dhidi ya filamu hiyo na kutoa wito wa kufikishwa mahakamani na kuadhibiwa wale wote waliohusika kwa njia moja au nyingine katika kutayarisha na kusambaza filamu ya "Innocence of Muslims" Mamilioni ya wananchi wa Iran pia wanatazamiwa kuandamana kote nchini hii leo kabla na baada ya swala ya Ijumaa kulaani filamu hiyo ya Kimarekani.
Wakati huo huo magazeti ya serikali ya China yamelitaja tukio la kuuawa balozi wa Marekani nchini Libya kutokana na hasira za Waislamu dhidi ya filamu hiyo inayovunjia heshima matukufu yao kuwa ni tukio kubwa zaidi baina ya ulimwengu wa Kiarabu na serikali ya Washington tangu ilipoanza harakati ya mwamko wa Kiislamu Mashariki ya Kati na kaskazini mwa Afrika.
Gazeti la Watu la chama tawala huko China limezungumzia tabia ya Wamarekani ya kuvunjia heshima mara kwa mara ustaarabu na itikadi za Kiislamu na kuandika kuwa, katika miaka ya hivi karibuni Wamarekani wamekuwa wakikariri vitendo vya kuvunjia heshima itikadi na matukufu ya Waislamu ikiwa ni pamoja na kuchoma moto nakala za Qur'ani, suala ambalo lilizusha malalamiko makubwa kote duniani.
Wimbi la sasa la hasira na malalamiko ya Waislamu dhidi ya Marekani lilianza baada ya video yenye dakika 14 ambayo ni sehemu ya filamu iliyopewa jina la "Innocence of Muslims" kusambazwa katika mtandao wa kijamii wa Youtube.
Mtayarishaji wa filamu hiyo ya kudhalilisha ni Sam Bacile ambaye ni raia wa Marekani na Israel. Mzayuni huyo amesema ametayarisah filamu hiyo kwa dola milioni tano zilizotolewa na Mayahidi 100.
Mashambulizi yanayoendelea kufanywa na watu wa dini mbalimbali dhidi ya balozi za Marekani katika Mashariki ya Kati baada ya kuvunjiwa heshima Mtume wa Mwenyezi Mungu yanatoa ujumbe wa wazi kwa viongozi wa White House kwamba, tokea sasa dharau na utovu wa adabu utakaofanywa na Mmarekani mmoja dhidi ya Uislamu hautatambuliwa kuwa ni tendo la mtu binafsi bali litahusishwa na mfumo unaopanga hujuma dhidi ya Uislamu huko Marekani na katika nchi za Magharibi kwa ujumla.

Thursday, September 13, 2012
Rais mpya wa Somalia aponea chupuchupu kuuawa
Msemaji wa jeshi la Umoja wa Afrika nchini Somalia Jenerali Ali Hamiid amesema kuwa milipuko hiyo miwili ilitokea jana mbele ya Hoteli ya Mogadishu, alikokuwa Rais mpya wa Somalia. Watu alioshuhudia wamesema maiti mbili zilionekana mbele ya hoteli hiyo, moja ikidhaniwa kuwa ni ya mtu aliyejitoa mhanga.
Kundi la al Shabaab limetangaza kuwa ndilo lililopanga shambulizi hilo. Hata hivyo Rais mpya wa Somalia na Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya hawakupatwa na madhara yoyote katika shambulizi hilo.
Kundi la Shabaab limemtuhumu Rais mpya wa Somalia kuwa ni msaliti na kusisitiza kuwa litaendeleza mapambano yake dhidi ya serikali ya nchi hiyo.
Rais Hassan Sheikh Mahmoud alichaguliwa Jumatatu iliyopita na Bunge la Somalia katika uchaguzi uliotajwa kuwa ni wa kihistoria.
Israel yahofia kusambaratika Serikali ya Palestina
Mafuriko na kipindupindu vyaua watu 160 Nigeria
Duru za habari kutoka Nigeria zinaarifu kuwa, mafuriko
yaliyosababishwa na kunyesha mvua kubwa tangu mwezi Juni hadi mwezi huu
nchini humo, yamepelekea kuuawa watu 160. Ripoti iliyotolewa na ofisi
inayoshughulikia masuala ya kibinaadmu ya Umoja wa Mataifa yenye makao
yake makuu mjini Niamey, Niger imetangaza kuwa, takwimu za hivi karibuni
zinaonyesha kuwa zaidi ya watu laki tano na 27 elfu wameathiriwa na
mafuriko hayo huku watu 81 wakipoteza maisha yao. Awali viongozi Nigeria
walikuwa wametoa ripoti iliyoonyesha kuuawa watu 68 na wengine laki
nne na 85 elfu wakiathiriwa vibaya na mafuriko hayo. Aidha ripoti
iliyotolewa na ofisi inayoshughulikia masuala ya kibinaadmu ya Umoja wa
Mataifa imeashiria kuwa watu wengine 81 wamefariki dunia kwa ugonjwa wa
kipindupindu uliyoyakumba maeneo ya magharibi mwa nchi hiyo na kufanya
idadi ya watu waliopoteza maisha yao kufikia 160.
Maandamano dhidi ya Marekani huko Misri
Misri kwa mara nyingine tena imeshuhudia maandamano ya wananchi
dhidi ya Marekani. Maelfu ya Wamisri wameandamana mbele ya ubalozi wa
Marekani huko Cairo mji mkuu wa Misri na kuichoma moto bendera ya
Marekani. Wafanya maandamano wametaka pia kufungwa ubalozi wa Marekani
huko Misri na kuondoka balozi wa Marekani nchini humo. Wananchi wa Misri
wamefanya maandamano hayo wakilalamikia kutengenezwa filamu ya
Kimarekani inayomvunjia heshima Mtume Muhammad (s.a.w). Sambamba na
Misri, huko Libya pia baadhi ya waaandamanaji wameuvamia ubalozi mdogo
wa Marekani huko katika mji wa Benghazi ambapo imeelezwa kuwa,
mfanyakazi mmoja wa ubalozi huo raia wa Marekani ameuawa na mwingine
kujeruhiwa. Japokuwa hii si mara ya kwanza kwa Wamarekani kuzivunjia
heshima itikadi za Waislamu, lakini kwa kuzingatia hali maalumu ya sasa
katika eneo la Mashariki ya Kati, baadhi ya duru za kisiasa zinaamini
kuwa, kuchaguliwa kipindi hiki kwa ajili ya kutengeneza filamu hiyo
inayomvunjia heshima Mtume wa Uislamu ni jambo lililoratibiwa na
halikutokea sadfa. Kwa ibara nyingine ni kuwa watengenezaji wa filamu
hiyo inayomvunjia heshima Mtume Muhammad (s.a.w) wamefanya hivyo ili
kuzusha hitilafu na mivutano kati ya nchi za Kiarabu zilizoshuhudia
mapinduzi ya wananchi hivi karibuni. Wataalamu wengi wa masuala ya
kisiasa wanaamini kuwa kwa kuzingatia kwamba idadi kadhaa ya watu wa
kabila la Kibti la Misri wenye misimamo mikali wameshirikiana na Tery
Jones Kasisi wa Kimarekani mwenye chuki dhidi ya dini ya Kiislamu
kutengeneza filamu inayomvunjia heshima Mtume wa Uislamu, lengo la hatua
hiyo ni kuzusha vita baina ya Waislamu na kabila la Kibti la Misri.
Hasa ikizingatiwa kuwa baadhi ya Wakibti wa Misri hawajafurahishwa na
kile kinachojiri sasa katika uga wa kisiasa wa nchi hiyo yaani kuingia
madarakani wanaharakati wa Kiislamu nchini humo. Itakumbukwa kuwa Kasisi
Tery Jones huko nyuma alikabiliwa na wimbi kubwa la malalamiko ya
Waislamu kutokana na kitendo chake cha kishenzi cha kuchoma moto nakala
kadhaa za kitabu Kitukufu cha Qur'ani. Hakuna shaka kuwa, hivi sasa pia
baadhi ya pande zinafanya kila linalowezekana ili kuitumbukiza Misri
katika hali ya mchafukoge na hivyo kunufaika na hali hiyo ya kutokuweko
uthabiti nchini humo. Marekani na utawala wa Kizayuni zinafahamu vyema
kwamba Misri mpya inatofautiana sana na ile ya zama za dikteta Husni
Mubarak, zama ambazo Misri ilikuwa ikifuata kibubusa siasa za Tel Aviv
na Washington. Hii ni kwa sababu tofauti hizo zimeathiri pakubwa maslahi
ya Marekani na utawala wa Kizayuni huko Misri.
Wednesday, September 12, 2012
HARAKATI ZA UAMSHO ZAANZA RASMI
Waislamu nchini Zanzibar wamehimizwa kuwa na umoja na mshikamano katika kudai maslahi ya nchi yao. kwani umoja wa waislamu ndio utakaoleta ushindi licha ya kwamba wapo baadhi ya waislamu hawapo pamoja na wenziwao.
Hayo yameelezwa na Amir wa jumuiya ya uamsho Zanzibar {JUMIKI} wakati alipokua akiwahutubia waislamu wenye uchungu na kuchoshwa na muungano uliopo baina ya Tanganyika na Zanzibar katika muendelezo wa harakati za mihadhara ya kuamsha wananchi kuhusu matatizo mbali mbali yanayotokana na muungano.
Mhadhara huo ulifanyika katika msikiti wa Afraa kidongo chekundu ambao ulihudhuriwa na maelfu ya waislamu wanaume na wanawake kwa ajili ya kusikiliza kitu gani kipya kimejiri baada ya kuonekana kukaa kimya kwa harakati hizo kwa ajili ya mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Shekh Mselem amebainisha kuwa lengo la JUMIKI ni kutaka kurejesha heshima na hadhi ya Zanzibar kwa njia ya AMANI na utulivu bila ya kumwaga damu wala kupoteza roho za waislamu. Hivyo waislamu wasikubali kupotezewa lengo lao na baadhi ya watu wachache ambao wanapata maslahi kwa kuwakandamiza wenzawo.
Wakati huo huo naibu amiri wa JUMIKI fadhiilat shekh AZZAN amewapongeza waislamu kwa umoja wao waliouonesha katika kutii amri za viongozi wao dini hasa hasa kuhusu suala zima la sensa.
Vile vile amesisitiza ya kwamba JUMIKI hawajakaa kimya kama inavyodaiwa na baadhi ya watu amesema msimamo wake wa kudai maslahi ya zanzibar hauzimiki ingawa kuna mbinu nyingi zinaandaliwa juu yao za kutaka kuwapoteza viongozi wa harakati hizo.
Monday, September 10, 2012
Sababu 21 Za Kumfanya Muislam Asisherehekee Maulidi
Zifuatazo
ni sababu na hoja ambazo Muislam mwenye kupenda kufuata haki na mwenye
kutaka apate uongofu ili abakie katika njia iliyonyooka na ajiepushe na
mambo ya baatil. Hoja ni za wazi kutoka katika Qur-aan na Sunnah. Hoja
za kupinga jambo hili ziko nyingi sana, lakini tulizozikusanya tunatumai
kuwa zitamtosheleza Muislamu aikinaishe nafsi yake kuwa Maulidi ni
jambo la uzushi katika dini kwa hiyo ni bora kutenda amali zile
tulizopata mafundisho yake kutoka kwa Mtume صلى الله عليه وآله وسلم, Maswahaba wake na Salafus Swaalih (Watangu wema) .
SABABU YA KWANZA: Kumpenda Mola Mtukufu Aliyetuumba:
Kwanza
kabisa ni kwa sababu ya kumpenda Mola Mtukufu Aliyetuumba Ambaye
Anataka kuhakikisha kuwa mapenzi yetu Kwake ni kumfuata Mtume صلى الله عليه وآله وسلم. Naye tokea kuzaliwa kwake hadi kufa kwake hakufanyiwa wala hakusherehekea siku yake ya kuzaliwa.
Anasema Allaah سبحانه وتعالى :
((قُلْ
إِن كُنتُمْ تُحِبُّونَ اللّهَ فَاتَّبِعُونِي يُحْبِبْكُمُ اللّهُ
وَيَغْفِرْ لَكُمْ ذُنُوبَكُمْ وَاللّهُ غَفُورٌ رَّحِيمٌ))
((Sema: Ikiwa nyinyi mnampenda Allaah basi nifuateni mimi, Allaah Atakupendeni na Atakufutieni madhambi yenu. Na Allaah ni Mwenye kufuta madhambi na Mwenye kurehemu)) [Al-'Imraan: 31]
SABABU YA PILI: Kufuata amri yake Mtume صلى الله عليه وآله وسلم ya kushikamana na Sunnah Zake na Sunnah za Makhalifa wake:
((
أُوصِيكُمْ بِتَقْوى اللَّه، وَالسَّمْعِ وَالطَّاعَةِ وإِنْ تَأَمَّر
عَلَيْكُمْ عَبْدٌ حبشيٌ ، وَأَنَّهُ مَنْ يَعِشْ مِنْكُمْ فَسَيرى
اخْتِلافاً كثِيرا . فَعَلَيْكُمْ بسُنَّتي وَسُنَّةِ الْخُلُفَاءِ
الرَّاشِدِينَ الْمَهْدِيِّينَ ، عضُّوا عَلَيْهَا بالنَّواجِذِ ،
وإِيَّاكُمْ ومُحْدثَاتِ الأُمُورِ فَإِنَّ كُلَّ بِدْعَةٍ ضلالَةٌ )) رواه أبو داود ، والترمذِي وقال حديث حسن صحيح
((Nakuusieni
kumcha Allah, usikivu na twaa hata ikiwa kiongozi wenu (Au
atakayekuamrishen) ni Mtumwa wa Habash. Mtakaoishi miongoni mwenu
mtaona ikhtilafu nyingi. Kwa hiyo shikamaneni na Sunnah zangu na Sunnah
za Makhalifa waliongoka baada yangu. Ziumeni kwa magego (zikamateni kwa
nguvu wala msiziache). Na tahadharini na mambo ya uzushi kwani kila
bid'ah ni upotofu)) [Abu Daawuud, At-Trimidhiy kasema Hadiyth Hasan Swahiyh]
Kwa hiyo inamtosheleza Muislamu hoja hii pekee ya kuwa Mtume صلى الله عليه وآله وسلم wala Maswahaba zake hawakusherehekea Maulidi, kumfanya naye asisherehekee.
Na hiyo ndio sababu kubwa ya Waislamu kukhitilafiana na kugawanyika makundi makundi. Amesema Imaam Maalik رحمه الله "'Hakuna kitakachotengeneza Ummah huu wa mwisho ila kwa kile kilichotengeneza Ummah wa mwanzo". Na maadam Salafus-Swaalih (watangu wema) hawakufanya bid'ah kama hii, sisi ni lazima tuwe na khofu kubwa ya kuifanya.
SABABU YA TATU: Ametuamrisha Allaah سبحانه وتعالى tufuate aliyotuletea Mtume صلى الله عليه وآله وسلم na tujiepushe na aliyotukataza:
((وَمَا آتَاكُمُ الرَّسُولُ فَخُذُوهُ وَمَا نَهَاكُمْ عَنْهُ فَانتَهُوا))
((Na anachokupeni Mtume chukueni, na anacho kukatazeni jiepusheni nacho)) [Al-Hashr:7]
SABABU YA NNE: Kufuata amri ya Kumtii Allaah سبحانه وتعالى na Mtume Wake صلى الله عليه وآله وسلم :
Anasema Allaah سبحانه وتعالى katika Aayah nyingi kwenye Qur-aan:
((وَأَطِيعُوا اللَّهَ وَأَطِيعُوا الرَّسُولَ))
((Na mtiini Allaah na mtiini Mtume )) [At-Twaghaabun:12]
Na kumtii Mtume صلى الله عليه وآله وسلم ni kumtii Allaah سبحانه وتعالى
((مَّنْ يُطِعِ الرَّسُولَ فَقَدْ أَطَاعَ اللّهَ))
((Mwenye kumtii Mtume basi ndio amemtii Allaah)) [An-Nisaa:80]
SABABU YA TANO: Kutokufuata amri ya Mtume صلى الله عليه وآله وسلم ni kumkhalifu na kupata adhabu kali:
((فَلْيَحْذَرِ الَّذِينَ يُخَالِفُونَ عَنْ أَمْرِهِ أَن تُصِيبَهُمْ فِتْنَةٌ أَوْ يُصِيبَهُمْ عَذَابٌ أَلِيم))
((Basi nawatahadhari wanaokhalifu amri yake, usije ukawapata msiba au ikawapata adhabu chungu)) [An-Nuur:63]
SABABU YA SITA: Kumpinga Mtume صلى الله عليه وآله وسلم ni sababu ya kuingizwa motoni:
((وَمَن يُشَاقِقِ الرَّسُولَ مِن بَعْدِ مَا تَبَيَّنَ لَهُ الْهُدَى وَيَتَّبِعْ غَيْرَ سَبِيلِ الْمُؤْمِنِينَ نُوَلِّهِ مَا تَوَلَّى وَنُصْلِهِ جَهَنَّمَ وَسَاءتْ مَصِيرًا))
((Na
anayempinga Mtume baada ya kumdhihirikia uongofu, na akafuata njia
isiyo kuwa ya Waumini, tutamuelekeza alikoelekea, na tutamuingiza katika
Jahannamu. Na hayo ni marejeo maovu)) [An-Nisaa 115]
SABABU YA SABA: Kukhofu upotofu unaompeleka mtu motoni:
Mtume صلى الله عليه وآله وسلم Alikuwa akitanguliza khutba zake kwa kutoa maonyo hayo:
(( إن خير الكلام كلام الله وخير الهدي هدي محمد صلى الله علي وسلم وشر الأمور محدثاتها وكل محدثة بدعة وكل بدعة ضلالة وكل ضلالة في النار)) أخرجه مسلم في صحيحه
((Maneno bora ni kitabu cha Allah (Qur-aan) na Uongofu mbora kabisa ni uongofu wa Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم na jambo la shari kabisa ni uzushi, na kila jambo jipya (katika dini) ni bid'ah (uzushi) na kila bid'ah ni motoni)) [Muslim katika Swahiyh yake]
SABABU YA NANE: Khofu ya kuwa miongoni mwa kundi litakaloingia motoni:
Mtume صلى الله عليه وآله وسلم alipoonya katika Hadiyth ifuatayo kuwa makundi yote yanayojiita ni ya Kiislam na hali hayafuati mafunzo kama aliyokuja nayo yeye, yatakuwa motoni isipokuwa kundi moja. Maswahaba walishtuka na wakataka kujua ni kundi gani hilo moja, akawajibu kuwa ni kundi ambalo watu wake watakuwa wanafuata mwendo wake na wa Maswahaba zake.
((افترقت اليهود على إحدى وسبعين فرقة، وافترقت النصارى على اثنتين وسبعين فرقة، وستفترق هذه الأمة على ثلاث وسبعين فرقة كلها في النار إلا واحدة،)) فقال الصحابة: من هي يا رسول الله؟ قال: ((من كان على مثل ما أنا عليه وأصحابي)) الترمذي و الحاكم
((Waligawanyika
Mayahudi katika makundi sabini na moja, na waligawanyika Manaswara
katika makundi sabini na mbili, na utagawanyika Umma wangu katika
makundi sabini na tatu, yote yataingia motoni ila moja!)) Maswahaba
wakasema: 'Ni kundi lipi hilo Ee Mtume wa Allaah? Akajibu: ((Ni lile ambalo litakuwa katika mwenendo wangu hii leo na Maswahaba zangu)) [Imepokewa na Maimaam At-Tirmidhiy na Al-Haakim]
SABABU YA TISA: Kuitikia wasiya wa Allaah سبحانه وتعالى ili kubakia katika njia iliyonyooka:
Anasema Allaah سبحانه وتعالى :
((وَأَنَّ هَذَا صِرَاطِي مُسْتَقِيمًا فَاتَّبِعُوهُ وَلاَ تَتَّبِعُواْ السُّبُلَ فَتَفَرَّقَ بِكُمْ عَن سَبِيلِهِ ذَلِكُمْ وَصَّاكُم بِهِ لَعَلَّكُمْ تَتَّقُونَ))
((Na
kwa hakika hii ndiyo Njia Yangu Iliyonyooka. Basi ifuateni, wala
msifuate njia nyingine, zikakutengeni na Njia yake. Haya Amekuusieni ili
mpate kumcha Mungu)) [Al-An'aam: 153]
SABABU YA KUMI: Vitendo visivyokuwa vya Sunnah havipokelewi:
(( من عمل عملاً ليس عليه أمرنا فهو رد)) البخاري
((Atakayetenda kitendo kisichokuwa chetu (katika dini yetu) basi kitarudishwa)) [Al-Bukhaariy]
Hivyo
mtu atapoteza muda wake, labda na gharama ya kutekeleza bid'ah hii na
kumbe amali hii haina thamani yoyote mbele ya Allaah (Subhaanahu wa
Ta'ala).
SABABU YA KUMI NA MOJA: Maulidi yamezushwa karne ya nne (miaka mia nne) baada ya kufa Mtume صلى الله عليه وآله وسلم na watu wenye kufru:
Walioanzisha
Maulidi ni viongozi wa Faatwimiyyun huko Misr (hawa walikuwa ni
Rawaafidh (Mashia) katika dhehebu la Ismailiyah [Makoja] walianza
kusherehekea Maulidi ya ‘Aliy bin Abi Twaalib (Radhiya Allahu ‘anhu),
na Maulidi ya Hasan na Husayn (Radhiya Allahu ‘anhuma), na Maulidi ya
Faatwimah az-Zahraa (Radhiya Allahu ‘anha), na Maulidi ya kiongozi wao
aliye hai kwa wakati ule. Sasa kwa nini tuwafuate wao? Na kama alivyotujulisha Mtume صلى الله عليه وآله وسلم kwamba watu bora kabisa wa kuwafuata ni wa karne tatu pekee aliposema:
((خير الناس قرني ثم الذين يلونهم ثم الذين يلونهم)) متفق عليه
((Watu bora kabisa ni wa karne yangu, kisha wanaowafuatia kisha wanaowafuatia)) [Al-Bukhaariy na Muslim]
SABABU YA KUMI NA MBILI: Makafiri wanafurahi Waislamu wanapofanya Bid'ah kwani ni kuacha mafunzo sahihi ya dini na ni kuzifuta Sunnah za Mtume صلى الله عليه وآله وسلم :
Napoleon Bonaparte alimpa Shaykh Al-Bakriy Riyaal mia nane za Ufaransa (inasemekana
ni mia tatu kwenye sehemu zingine) ili arudishe bid'ah ya Maulidi naye
akahudhuria mwenyewe Maulidi. Maana makafiri wanajua kuwa Waislam
wanaposhughulishwa na vipumbazo kama hivyo, husahau matakwa yao ya msingi na muhimu.
SABABU YA KUMI NA TATU: Baadhi ya maneno katika Maulidi yana kufru ya kumpandisha Mtume صلى الله عليه وآله وسلم cheo cha usawa na Allaah سبحانه وتعالى wakati yeye ametuonya tusifanye hivyo:
((لا تطروني كما أطرت النصارى المسيح ابن مريم، إنما أنا عبد، فقولوا: عبد الله ورسوله)) متفق عليه
((Msinitukuze Kama Manaswara walivyomtukuza Masiyh mwana wa Maryam, hakika mimi na mja kwa hiyo semeni mja wa Allaah na Mjumbe Wake)) [Al-Bukhaariy na Muslim]
SABABU YA KUMI NA NNE: wanapoinuka kumswalia Mtume صلى الله عليه وآله وسلم wanaamini kwamba roho yake inahudhuria wakati huo:
Hii
ni fikra ovu kabisa, na pia yeye mwenyewe alikuwa hapendi kuinukiwa
alipokuwa hai, vipi mtu anayempenda amfanyie jambo analolichukia wakati
amekufa?
Siku moja Maswahaba walikuwa wamekaa msikitini pamoja na Abubakar رضي الله عنه
ambaye alikuwa akisoma Qur-aan. 'Abdullah ibn Ubbay ibn Saluul, mnafiki
mkubwa alikuja akaweka takia na mto wake akaketi. Alikuwa ni mwenye
sura nzuri na mwenye lugha ya ufasaha. Alisema: "Ewe Abu Bakar, muulize
Mtume صلى الله عليه وآله وسلم atuonyeshe alama ya utume wake kama walivyotuonyesha Watume wengine. Mfano, Muusa عليه السلام ametuletea Ubao (wa Tauraat), 'Iysa عليه السلام alituletea Injiyl na meza ya chakula kutoka mbinguni, Daawuud عليه السلام alituletea Zabuur, Swaalih عليه السلام alitulietea ngamia wa kike" Abu Bakar رضي الله عنه aliposikia akaanza kulia. Mara akaingia Mtume صلى الله عليه وآله وسلم na Abu Bakar رضي الله عنه akawaambia Maswahaba wengine wainuke kumpa heshima Mtume صلى الله عليه وآله وسلم na kumpa malalamiko ya mnafiki. Mtume صلى الله عليه وآله وسلم akasema: ((Sikizeni! Msiniinukie mimi bali….
وَقُومُواْ لِلّهِ قَانِتِينَ
((na simameni kwa ajili ya Allaah)) [Al-Baqarah: 238] (dalili kutoka Tafsiyr Ibnu Kathiyr]
SABABU YA KUMI NA TANO: Kuchanganyika kwa wanawake na wanaume:
Jambo ambalo limekatazwa katika dini na katika sherehe hii kumedhihirika sana hasa pande za nchi zetu za Afrika Mashariki. Na uovu huu unafikia hadi kuimba kwa pamoja na kuchezesha vichwa kama kwamba ni dansi fulani. Imefika hadi maulidi kuitwa ‘disco maulidi’
SABABU YA KUMI NA SITA: Kuwaigiza Manaswara:
Manaswara wanasherehekea siku ya kuzaliwa 'Iysa عليه السلام kama wanavyodai. Na Waislamu haitupasi kusherehekea siku ya kuzaliwa Mtume صلى الله عليه وآله وسلم kwani tumefundishwa kuwa tufanye kinyume na wao katika mambo yetu.
Vilevile Mtume صلى الله عليه وآله وسلم kasema:
((خالفوا المشركين، أحفوا الشوارب، وأوفوا اللحى)) البخاري و مسلم
((Kuweni kinyume na Washirikina, punguzeni masharubu na fugeni ndevu)) [Al-Bukhaariy na Muslim]
Na kufanya hivyo (kusherehekea Maulidi) tutakuwa tunajifananiza nao, na jambo hilo la kuwaiga na kujifananisha na mambo yao limekatazwa kama alivyosema Mtume صلى الله عليه وآله وسلم :
((من تشبه بقوم فهو منهم )) أحمد و أبو داود
Anayejishabihisha na watu basi naye ni miongoni mwao)) [Ahmad, Abu Daawuud]
SABABU YA KUMI NA SABA: Dini imekamilika hakuna tena haja ya kuleta mambo ya dini mapya:
Kuzusha mambo mapya ya dini ni kama kumtuhumu Mtume صلى الله عليه وآله وسلم kuwa ametukhini mafunzo ya dini na hakuyakamilisha, bali kuna aliyoyaficha na hakutupa yote!! Na hali aliikamilisha dini kama ilivyompasa. Aayah hii chini iliteremshwa kudhihirisha ukamilifu wa dini ya Mola Mtukufu
((الْيَوْمَ أَكْمَلْتُ لَكُمْ دِينَكُمْ وَأَتْمَمْتُ عَلَيْكُمْ نِعْمَتِي وَرَضِيتُ لَكُمُ الإِسْلاَمَ دِينً))
((Leo Nimekukamilishieni Dini yenu, na nimekutimizieni Neema Yangu, na Nimekupendeleeni UISLAMU uwe ndiyo Dini)) [Al-Maaidah:3]
Sasa vipi watu walete mafundisho ya dini mapya yasiyotokana na mafunzo kutoka kwa Allaah سبحانه وتعالى na Mtume Wake صلى الله عليه وآله وسلم ? Anauliza Allaah سبحانه وتعالى :
((أَمْ لَهُمْ شُرَكَاء شَرَعُوا لَهُم مِّنَ الدِّينِ مَا لَمْ يَأْذَن بِهِ اللَّهُ))
((Au hao wana miungu ya kishirikina waliowatungia dini asiyoitolea idhini Allaah?)) [Ash-Shuura 21]
SABABU YA KUMI NA NANE: Kudhihirisha iymaan kwa kupenda yale aliyokuja nayo Mtume صلى الله عليه وآله وسلم pekee:
عَنْ
أَبِي مُحَمَّدٍ عَبْدِ اللَّهِ بِنْ عَمْرُو بِنْ العَاصِ رَضِيَ اللَّهُ
عَنْهُمَا قَالَ : قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وآله وسلم: ((لا
يُؤْمِنُ أَحَدُكُمْ حَتَّى يَكُونَ هَوَاهُ تَبَعَاً لِمَا جِئْتُ بِهِ )) حَدِيثٌ حَسَنٌ صَحِيحٌ، رَوَيْنَاهُ فِي كِتَابِ "الْحُجَّةِ بِإِسْنَادٍ صَحِيحٍ.
Kutoka kwa Abu Muhammad Abdullah Ibn 'Amr Bin Al-'Aasw رضي الله عنه ambaye alisema: Mtume صلى الله عليه وسلم kasema: ((Hatokuwa kaamini
(kikwelikweli) mmoja wenu mpaka mapenzi yake yatakapomili (yatakapotii
au kuwafikiana) kwenye yale niliyoyaleta)) (mafundisho) [Hadiyth Hasan iliyotoka katika kitabu “Al-Hujjah” ikiwa na mtiriko mzuri wa mapokezi]
SABABU YA KUMI NA TISA: Kuacha mambo yenye shaka na kubakia katika yaliyo wazi:
عَنْ
أَبي مُحمَّدٍ الحسَنِ بْنِ عليّ بْنِ أبي طَالِب، سِبْطِ رَسُولِ اللهِ
صلى الله عليه وسلم وَرَيْحَانَتِهِ رضيَ اللهُ عنهُما، قالَ: حَفِظْتُ
مِنْ رَسُولِ الله صلى الله عليه وسلم: ((دَعْ ما يَرِيبُكَ إلى مَا لاَ
يَرِيُبكَ )) رَوَاهُ التِّرْمِذِيُّ وَالنَّسَائِيُّ وَقَالَ التِّرْمِذِيُّ: حَدِيثٌ حَسَنٌ صَحِيحٌ.
Kutoka kwa Abu Muhammad Al-Hasan Ibn ‘Aliy Ibn Abi Twaalib mjukuu wa Mtume صلى الله عليه وسلم na kipenzi chake رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُمَا alisema: "Nilihifadhi kutoka kwa Mtume صلى الله عليه وسلم maneno haya: ((Acha kile kinachokutia shaka ufuate kile kisichokutia shaka)). [Imesimuliwa na At-Tirmidhiy na An-Nasaaiy, At-Tirmidhiy akisema kuwa ni hadiyth Hasan na Swahiyh]
SABABU YA ISHIRINI: Mwezi huu wa Rabiy'ul Awwal ni mwezi alioaga dunia Mtume صلى الله عليه وآله وسلم , sasa vipi Muislamu asherehekee?
Wanachuoni wote wameafikiana kuwa siku hii ya tarehe 12 Rabiy‘ul Awwal ni siku aliyofariki Mtume صلى الله عليه وآله وسلم Vipi sasa watu watakuwa wanafurahi kwa siku kama hiyo? Anas bin Maalik رضي الله عنه anatuhadithia kuwa: "Hakuna siku ambayo watu wa Madiynah walikuwa na furaha ya hali ya juu kama siku aliyohamia Mtume صلى الله عليه وآله وسلم katika mji huo. Na hakuna siku ya huzuni kabisa kwa watu wa Madiynah kama siku aliyoaga dunia Mtume صلى الله عليه وآله وسلم ."
Inaonekana kama sisi tunakwenda kinyume na maadili ya wale watu bora waliokuwa wakimpenda Mtume صلى الله عليه وآله وسلم hata kuliko nafsi zao wenyewe.
SABABU YA ISHIRINI NA MOJA: Sababu za Waislamu wanaoshikilia Bid'ah:
1-Kufuata bila ya kupata elimu sahihi.
Ukitaka
kujua hoja za Waislamu wanaofuata bid'ah, hutopata kutoka kwao hoja
nyingi kutoka katika Qur-aan na Sunnah, bali ni hoja za kutokana na rai
zao tu, au watakwambia, 'kwani kuna ubaya gani?'. Na hata wakitoa hoja
kutoka katika Qur-aan na Sunnah basi utakuta kwamba wanazifasiri dalili
hizo isivyokusudiwa bali wanazishabihisha na matamanio yao kama Anavyosema Allaah سبحانه وتعالى :
((هُوَ الَّذِيَ أَنزَلَ عَلَيْكَ الْكِتَابَ مِنْهُ آيَاتٌ مُّحْكَمَاتٌ هُنَّ أُمُّ الْكِتَابِ وَأُخَرُ مُتَشَابِهَاتٌ فَأَمَّا الَّذِينَ في قُلُوبِهِمْ زَيْغٌ فَيَتَّبِعُونَ مَا تَشَابَهَ مِنْهُ ابْتِغَاء الْفِتْنَةِ وَابْتِغَاء تَأْوِيلِه))
((Yeye
Ndiye Aliyekuteremshia Kitabu (hiki Qur-aan). Ndani yake zimo aayah
Muhkam (nyepesi kufahamika) ambazo ndizo msingi (asili) wa Kitabu
(hiki). Na ziko nyingine Mutashaabihaat (zinababaisha kama
habari ya Akhera, za Peponi na Motoni na mengineyo ambao yamekhusika na
Roho). Wale ambao nyoyoni mwao mna upotofu wanafuata zile
zinazobabaisha kwa kutaka kuwaharibu watu na kutaka kujua hakika yake
vipi)) [Al-'Imraan:7]
Na
ukizingatia utaona kuwa Waislamu wanaofuata Bid'ah sio wenye elimu
kubwa ya juu, kwani ukilinganisha na wanaofuata Sunnah utaona kuwa kuna
tofauti kubwa sana. Na hivyo ndivyo Allaah سبحانه وتعالى
Anavyomjaalia kumpa elimu ya upeo wa juu yule mwenye kufuata haki. Na
tujiulize Maulamaa wangapi wacha Mungu wenye elimu madhubuti wanafuata
Bid'ah? Si rahisi kuwapata, bali ukiuliza wanaofuata Sunnah na wenye
elimu kubwa ambayo athari yake tunaiona leo hii na itaendelea kizazi
hadi kizazi InshaAllah, utakuta ni wengi sana,
miongoni mwao ni Maimamu wanne; Imaam Shaafi'iy, Ahmad bin Hanbali, Abu
Haniyfah, Maalik, Sufyaan Ath-Thawry. Wasimulizi wa Hadiyth kina
Al-Bukhaariy, Muslim, Abu Daawuud, At-Tirmidhiy, An-Nasaaiy, Ibn Maajah
na kadhalika. Maulamaa maarufu; Ibn Taymiyah, ibnul Qayyim, ibnul Jawzy,
ibnul Mubaarak, ibnu Hajar, ibnu Kathiyr, Imaam An-Nawawy, na waliopita
katika miaka ya karibuni kama kina: ibn 'Uthaymiyn, ibn Baaz, Shaykh
Al-Albaaniy na kadhalika. Hata katika jamii yetu kuna waliokuwa
wamejaaliwa kupewa kipaji cha elimu kama
kina Shaykh 'Abdullah Swaalih Al-Faarisy na kina Al Amiyn na Muhammad
Qaasim Mazrui, Haarith Swaalih na wengineo wengi, bila kuwataja walio
hai ambao hawana idadi kwa wingi wao.
2- Kufuata matamanio ya nafsi
Hufuata matamanio ya nafsi inavyopenda na sio kufuata haki. Wengine kutokana na unasaba wao huwa ni kwao kama utukufu kuwa nao wamo katika unasaba wa Mtume صلى الله عليه وآله وسلم
Anasema Allaah سبحانه وتعالى :
((وَلاَ تَتَّبِعِ الْهَوَى فَيُضِلَّكَ عَن سَبِيلِ اللَّهِ))
((Wala usifuate matamanio yakakupoteza kwenye Njia ya Allaah)) [Swaad:26]
3- Ugumu wa kuacha mila uliotokana na mababa na mababu
Mitume
waliopita walikuwa wakiwaita watu wao wawafuate waliyokuja nayo ya haki
walipendelea kubakia katika ujinga na mila za mababa zao. Na Waislamu
wenye kufuata mambo ya bid'ah nao ni vile vile ukiwauliza kwa nini
hamuachi mambo yasiyo katika mafundisho ya Mtume صلى الله عليه وآله وسلم
wanajibu hivyo hivyo kuwa 'vipi tuache Maulidi na hali tumekulia nayo?,
au tutaachaje kitu ambacho mababa zetu walikuwa wakifanya?? Ina maana
wao walikuwa hawajui?"
Anasema Allaah سبحانه وتعالى :
((وَإِذَا قِيلَ لَهُمْ تَعَالَوْاْ إِلَى مَا أَنزَلَ اللّهُ وَإِلَى الرَّسُولِ قَالُواْ حَسْبُنَا مَا وَجَدْنَا عَلَيْهِ آبَاءنَا أَوَلَوْ كَانَ آبَاؤُهُمْ لاَ يَعْلَمُونَ شَيْئًا وَلاَ يَهْتَدُون))
((Na
wanapoambiwa: Njooni kwenye yale Aliyoyateremsha Allaah, na kwa Mtume,
husema: Yanatutosha tuliyowakuta nayo baba zetu. Je, hata ikiwa baba zao
walikuwa hawajui kitu wala hawakuongoka?)) [Al-Maaidah: 104]
Au walikuwa wakisema:
((بَلْ قَالُوا إِنَّا وَجَدْنَا آبَاءنَا عَلَى أُمَّةٍ وَإِنَّا عَلَى آثَارِهِم مُّهْتَدُونَ))
((Bali wanasema: Hakika sisi tuliwakuta baba zetu wanashika dini makhsusi, basi na sisi tunafuata nyayo zao)) [Az-Zukhruf: 22]
4- Kukhofu kutokuungana na wengi wanaofuata bid'ah
Wengine
ukiwauliza kwa nini unafuata bid'ah ya Maulidi. Jibu ni kuwa anakhofu
kuwa yeye peke yake ataonekana kuwa hasomi Maulidi katika kundi lake, na
hii ni hatari ya kukhofu watu badala ya kumkhofu Mola Mtukufu na pia ni
kwenda na mkumbo kwa kudhani kuwa wengi ndiyo wenye haki! Haya
Anatueleza Allaah kuwa:
((وَإِن تُطِعْ أَكْثَرَ مَن فِي الأَرْضِ يُضِلُّوكَ عَن سَبِيلِ اللّهِ إِن يَتَّبِعُونَ إِلاَّ الظَّنَّ وَإِنْ هُمْ إِلاَّ يَخْرُصُونَ))
((Na
ukiwatii wengi katika hawa waliomo duniani watakupoteza na Njia ya
Allaah. Hawa hawafuati ila dhana tu, na hawakuwa ila ni wenye kusema
uwongo tu)) [Al-An'aam: 116]
5- Wengine wanasema kuwa ni kudhihirisha mapenzi ya Mtume صلى الله عليه وآله وسلم
Je, mapenzi ya Mtume صلى الله عليه وآله وسلم
yadhihirike siku moja tu? Au katika mwezi huu tu? Na si siku zote? Hayo
bila shaka ni mapenzi ya uongo. Mapenzi ya kweli ni yale ya kumkumbuka
siku zote na kumtii umpendaye. Haya ya Maulidi hayana moja kati ya
mawili hayo.
6- Hoja ya kusema ni Bid'atun-hasanah (uzushi mzuri)
Mojawapo yao ni kuwa Maulidi ni Bid'atun-hasanah. Katika dini ya Kiislamu hakuna bid'ah nzuri kwani Mtume صلى الله عليه وآله وسلم
alipotuonya alisema 'Kullu Bid'atin Dhwaalaah' (kila bid'ah ni
upotofu). Na ikiwa kauli hii wanaipinga kuwa sio KILA bid'ah, basi
wanasemaje kuhusu kauli ya Allaah سبحانه وتعالى Anaposema:
((كُلُّ نَفْسٍ ذَآئِقَةُ الْمَوْتِ))
((Kila nafsi itaonja mauti)) [Al-'Imraan:185]
Je,
tupinge pia kauli hii kuwa sio KILA nafsi? Na je, ina maana kuwa kuna
watu wengine watabakia hawatokufa na hali tunatambua kuwa hakuna
atakayebakia ila Mwenyewe Mola Mtukufu?
Subscribe to:
Posts (Atom)