Social Icons

rss feed facebook twitter google plus linkedin youtube email

Tuesday, January 29, 2013

Vikosi maalumu Tunisia katika viwanda vya mafuta


Askari wa Jeshi la Tunisia
Askari wa Jeshi la Tunisia
Kufuatia utekaji nyara wa hivi karibuni dhidi ya wafanyakazi wa kiwanda cha gesi huko nchini Algeria, Tunisia imetangaza kuwa imeweka askari wake maalumu kwenye taasisi zake za mafuta na gesi zilizopo kusini mwa nchi hiyo karibu na mipaka ya Libya na Algeria. Kamanda mmoja wa jeshi la Tuniasia ambaye hakutaka jina lake litajwe amenukuliwa akisema kuwa, hatua hiyo imechukuliwa tangu mwanzoni mwa wiki hii katika fremu ya kuimarisha vikozi vilivyoko katika maeneo ya jangwani kwa ajili ya kulinda usalama katika taasisi hizo. Kwa mujibu wa kamanda huyo, askari hao na zana kadhaa za kijeshi wamepelekwa kuimarisha doria katika maeneo ya Ramada na Dahabiya yaliyopo mpakani kati ya Libya na Algeria. Tangu Ufaransa ilipoanzisha mashambulizi yake huko nchini Mali makundi ya kigaidi ya eneo hilo yameanzisha mashambulizi ya kuyalenga maeneo nyeti kama vile viwanda,

Watu sita wauawa, Waziri Mkuu Somalia anusurika


Mwanajeshi wa serikali ya Somalia katika eneo la mlipuko wa huko nyuma mjini Mogadishu Mwanajeshi wa serikali ya Somalia katika eneo la mlipuko wa huko nyuma mjini Mogadishu
Watu wasiopungua sita wameuawa kufuatia mlipuko wa bomu nje kidogo ya ofisi ya Waziri Mkuu wa Somalia mjini Mogadishu.
Hujuma hiyo imejiri leo Jumanne mchana ambapo kati ya waliouawa ni maafisa wa usalama. Imearifiwa kuwa mtu aliyekuwa amejifunga mshipi wa bomu alijiripua karibu na ofiisi ya Waziri Mkuu Abdi Farah Shirdon katika eneo la kati kati mwa Mogadishu. Maafisa wa usalama wanasema waziri mkuu alikuwa ofisi wakati wa tukio hilo lakini hakujeruhiwa.

Saturday, January 26, 2013

Dk. Amani Abeid Karume adai hati halisi ya muungano



Amani_Karume Salma Said,
Rais Mstaafu wa Zanzibar, Dk. Amani Abeid Karume, ameomba kupatiwa hati halisi (Original) ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ambayo imetiwa saini na Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Mzee Abeid Amani Karume.
Ombi hilo la Karume limekuja kufuatia utoaji wake wa maoni mbele ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba iliyoongozwa na Mwenyekiti wa tume hiyo, Jaji Joseph Warioba, makamo Mwenyekiti Assa Rashid na wajumbe wnegine aliyokutana nayo juzi nyumbani kwake Mjini Unguja.
Karume alisema yeye hana hati ya Muungano na hajawahi kuiona na iwapo Tume hiyo inayo hati hiyo basi angeomba kupatiwa kwani ni wazanzibari wengi wanahitaji kuiona hati hiyo ambayo ni mkataba kati ya nchi mbili zenye mamlaka kamili kila moja na zilizoungana mnamo mwaka 1964 kila nchi ikiwa huru.

Tuesday, January 22, 2013

Waliokataa sensa wameitia hasara serikali

Na Salma Said
SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar imesema kitendo cha baadhi ya wananchi kususia sensa kilisababisha serikali kuingia gharama kubwa katika kuendelea kuhamasisha umma kukubali zoezi hilo kwa maendeleo ya Taifa
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Fedha Uchumi na Mipango ya Maendeleo Zanzibar, Omar Yusuf Mzee ameyasema hayo alipokuwa akijibu suala la msingi katika ukumbi wa baraza la wawakilishi linaloendelea huko Chukwani nje kidogo ya Mji wa Zanziba lililoulizwa na mwakilishi wa Kiwani (CUF) Hija Hasan Hija .
Hija aliyetaka kujua ni kiasi gani serikali imepata hasa na imejifunza nini kutokana na mamuzi wa wananchi, je ni sheria gani iliyovunjwa na wananchi na je sheria hiyo ilipitishwa au kuridhiwa na baraza la wawakilishi.
Aidha Hija alitaka kujua iwapo sheria ipo na inafanya kazi ni kwa nini vyombo va Dola vikaaamua kuwapiga na kuwasumbua wananchi badala ya sheria kuchukua mkondo wake wakati wa zoezi la sensa lililofanyika mwishoni mwa mwaka jana.
Waziri alisema hasa pale serikali ilipoongeza wiki moja zaidi kwa ajili ya kuendelea na kazi ya kuhesabu watu sio rahisi kupata tathmini ya fedha zilizotumika kughaamia kazi za ziada zilizofanywa na makundi ya watu mbali mbali walihamasisha na kuelimisha watu washiriki katika zoezi la sensa ya watu na makazi baada ya kugomea kuhesabiwa kwa wiki ya kwanza.
Alisema sheria iliyovunjwa ni sheria ya takwimu ya Zanzibar Namba 9 ya mwaka 2007 sehemu ya tano kifungu cha 14 (2) na (3) na sheria hii ilipitishwa na Baraza la wawakilishi
Mzee alisema serikali haina taarifa kuwa wananchi waliosusia sensa walipigwa na kusumbuliwa na vyombo vya dola na hakuna mwananchi aliyewasilisha madai ya aina hii katika chombo chochote cha kisheria hapa Zanzibar kinyume chake ni baadhi ya wananchi waliosusia zoezi hilo ndio waliofanya fujo.
“Serikali haina taarifa ya kuwa kuna watu waliyanyaswa kuhusu suala la sensa lakini tunajua kuwa maafisa wa sensa ndio walionyanyaswa, kupingwa na kuharibiwa mali ya serikali ilipokuwa ikifanya hiyo kazi” alisema Waziri.
Waliwapiga na kuwatukana makasaa wa sensa kuwanyananya maafisa vifaa vyao vyakufnayia kazi ni wananchi ambao hawakuwa wakitaka kuhojiwa kuhusiana na zoezi hilo la sensa ambapo mbali ya kuhatarisha usalama wa maafisa hao lakini pia wamehatarisha usalama wa wananchi wenzao katika maeneo ya makaazi yao.
Alisema muda wote huo serikali ilichukua busara na hekma kubwa na ilijiepusha na vitendo va kutumia nguvu na iliunda timu ya viongozi wa dini na watu mashuhui kwa leno la kuwaelimisha zaidi wananchi badala ya kuwachukulia hatua.
Naye Mwakilishi wa Jimbo la Chonga Abdallah Juma Abdallah (CUF) alisema sensa imeshindwa kufanikiwa kutokana na tabia ya masheha kukataa kuwatambua wananchi katika maeneo yao wakati wa uchaguzi na ndio wananchi wamejenga uadui kati yao na masheha.
“Mheshimiwa Spika Masheha wamekuwa na tabia ya kukataa kuwatambua wananchi wa maeneo yao katika shehia zao hata kama wanawajua lakini ikifika wakati wa uchaguzi wanasema hawawatambui jee serikali haioni kwamba kittendo cha Masheha ndio kilichochangia wananchi kukataa kutoa ushirikiano kwa Masheha wakilipiza kutotambuliwa kwako na Masheha?” alihoji Abdallah.

Jeshi la Uganda lamuuwa mlinzi mkuu wa Kony


Jeshi la Uganda lamuuwa mlinzi mkuu wa KonyJeshi la Uganda limethibitisha kumuuwa mlinzi mkuu wa Joseph Kony kiongozi wa kundi la waasi wa Lord's Resistance Army (LRA).
Msemaji wa Jeshi la Uganda Kanali Felix Kulayigye amesema kuwa, Brigedia Binani ameuawa katika mapigano makali yaliyojiri katika eneo la mashariki mwa Jamhuri ya Afrika ya Kati karibu na mpaka na serikali ya Sudan Kusini. Kanali Kulayigye ameongeza kuwa mapigano makali yanaendelea kati ya majeshi ya Uganda na waasi wa LRA katika eneo lililoko umbali wa kilomita 280 kaskazini mwa Diema.
Brigedia Binani anatuhumiwa kwa kutorosha watoto na kuwapeleka kwenye kundi hilo na wengine wakitumikishwa katika kukusanya chakula kwa ajili ya wapiganaji wa LRA. Inasemakana kuwa, nguvu za kijeshi za Kony zinazidi kupungua baada ya wapiganaji wake kupungua sana huku akijaribu kuhama kutoka sehemu moja hadi nyingine akikwepa mashambulizi ya majeshi ya Uganda katika maeneo ya mpakani ya nchi za Jamhuri ya Afrika ya Kati, Sudan Kusini na Sudan.

Sitta: Katiba ijayo ya Tanzania iwabane mafisadi


Samuel John Sitta, Waziri wa Afrika Mashariki wa Tanzania.
Samuel John Sitta, Waziri wa Afrika Mashariki wa Tanzania.Waziri wa Afrika Mashariki wa Tanzania Samuel Sitta amependekeza kuwa, Katiba mpya ya Tanzania itaje moja ya sifa za wagombea Urais kuwa ni uadilifu ili kuwabana watu ambao wamejilimbikizia mali na wezi kuongoza nchi.  Samuel Sitta amependekeza pia kuwa, Katiba mpya ijayo iweke idadi ya wabunge badala ya kugawa majimbo kila baada ya uchaguzi, jambo ambalo alisema ni kuwaongezea ulaji baadhi ya watu. Mwanasiasa huyo ambaye amewahi kuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amesisitiza kuwa,

Utulivu warejea Eritrea baada ya uasi jeshini


Rais Issaias Afeworki wa EritreaSerikali ya Eritrea imesema kuwa, hali katika mji mkuu Asmara ni tulivu baada ya kushindwa nguvu wanajeshi waasi waliokuwa wamechukua udhibiti wa jengo la Wizara ya Habari.
Yemane Gebremeskel, mkurugenzi wa ofisi ya Rais Issaias Afeworki wa Eritrea amethibitisha kutulia hali ya mambo.
Kundi moja la askari waasi katika Jeshi la Eritrea walizingira Wizara ya Habari Jumatatu na kulazimisha Shirika la Utangazaji la Taifa kutangaza kuachiliwa huru wafungwa wote wa kisiasa.
Wanajeshi hao waasi walimlazimisha mkuu wa televisheni ya serikali kusoma tangazo hilo.

WAZIRI WASHERIA NA KIBARAKA WA KANISA...........AISHITUMU UAMSHO... ASEMA KIKUNDI CHA KUANZISHA FUJO......VIONGOZI WAKE LAZIMA WADHIBITIWEE..



Wazir wa Sheria na Katiba Zanzibar Abubakar Khamis .Amesema nchi sasa imetulia naimerudi katikahali ya Amani kama ilivokuwa awali baada ya viongozi wa UAMSHO kuwa ndani.
Akisema hayo katika uzinduzi wa Baraza la Maulamaa wa zanzibar.Akisisitiza kuwa Uamshioni kikundicha Fujo lazima wadhibitiwe wao pamoja viongozi wao.
Kwa maana hiyo Abubakar anaungana na Kanisa na Maskofu walivoishutumu serikali kuwa wanaiwachia uamsho kwani ni kikundi cha Fujo na wanavunja Amani.

Friday, January 18, 2013

Tunisia yaonya kuathiri vibaya mgogoro wa Mali



Rais Muncef Marzouki wa Tunisia
Rais Muncef Marzouki wa TunisiaSerikali ya Tunisia imeonya kuhusiana na taathira mbaya zinazoweza kulikumba eneo zima la Sahel na nchi za magharibi mwa Bara Arabu kutokana na uingiliaji kijeshi nchini Mali. Hayo yalisemwa jana na Rais Moncef Marzouki wa Tunisia ambaye amesisitizia pia udharura wa kuimarishwa mawasiliano na mshikamano kwa ajili ya kuitafutia ufumbuzi kadhia ya Mali. Katika ripoti hiyo iliyotolewa baada ya kikao cha mawaziri wa ulinzi na wa mambo ya nje wa nchi hiyo, imeelezwa kwamba,

Sudan Kusini yaanza kuondoka mpakani




Sudan Kusini yaanza kuondoka mpakaniSerikali ya Sudan Kusini imetangaza kuwa, imeanza kuondoa askari wake katika maeneo ya mpaka wake na Sudan, kwa ajili ya kuanzisha eneo huru kati ya nchi mbili hizo jirani. Ripoti iliyotolewa jana na serikali ya Juba ilibainisha kuwa, mwisho wa kuondoka vikosi vya nchi hiyo katika maeneo hayo ya mpakani ni tarehe 4 mwezi ujao wa Februari na kwamba, Sudan Kusini inatarajia kuona Khartoum nayo inachukua hatua mithili ya hiyo kama njia ya kutekeleza makubaliano yaliyotiwa saini na viongozi wa nchi mbili mjini Addis Abba, Ethiopia. Mwezi Septemba mwaka jana na chini ya mashinikizo ya kimataifa, Sudan na Sudan Kusini zilikubaliana kuondoa vikosi vyao katika maeneo yanayogombaniwa na pande mbili. Aidha viongozi wa nchi hizo Omar Hassan al-Bashir wa Sudan na Salva Kiir wa Sudan Kusini, walikubaliana kuanzisha eneo huru lisilo na askari wa upande wowote,

Askari wa Umoja wa Afrika waua watoto 5 Somalia



Askari wa Kenya akihudumu chini ya mwavuli wa Umoja wa Afrika nchini Somalia
Askari wa Kenya akihudumu chini ya mwavuli wa Umoja wa Afrika nchini Somalia
Duru za habari kutoka Somalia zinaarifu kuwa, askari wa kulinda amani wa Umoja wa Afrika, wamewaua kwa kuwapiga risasi raia saba wa nchi hiyo kwa bahati mbaya. Duru za habari zinaarifu kuwa, mauaji hayo yalitokea jana katika operesheni za kuwasaka wanamgambo wa ash-Shabab waliodhaniwa kwamba walikuwa wamekimbilia katika shule moja na hivyo kupelekea raia saba kuuawa wakiwamo watoto watano. Dhahir Amin Jisu mmoja wa wabunge wa Somalia amenukuliwa akisema kuwa, wahanga wa mauaji hayo ni watoto walio chini ya umri wa miaka 10 na kwamba tukio hilo lilitokea katika mji wa Liju ulioko umbali wa kilomita 120 kutoka mji mkuu wa Somalia, Mogadishu.

25 wauawa katika miripuko ya mabomu Iraq



25 wauawa katika miripuko ya mabomu Iraq
Duru za habari kutoka nchini Iraq zimearifu kuwa, zaidi ya watu 25 wameripotiwa kuuawa katika maeneo tofauti nchini humo. Habari zinasema kuwa, mauaji hayo yalitokea jana katika mfululizo wa miripuko ya mabomu iliyotokea katika maeneo tofauti nchini Iraq. Mauaji hayo yanajiri baada ya mfululizo wa mauaji yaliyosababishwa na mashambulizi ya kigaidi yaliyotokea katika siku tatu zilizopita kwenye maeneo kadhaa ya nchi hiyo, na kupelekea kuuawa zaidi ya watu 81 na kujeruhiwa mamia ya wengine. Hadi sasa hakuna kundi lolote lililotangaza kuhusika na mauaji hayo. Viongozi wa Iraq wamekuwa wakizituhumu nchi za Saudia na Qatar kuwa, zinayaunga mkono makundi ya kigaidi yanayofanya mauaji nchini humo, kama njia ya kutekeleza siasa za Marekani kwenye eneo la Mashariki ya Kati. Wakati huo huo serikali ya Baghdad imetangaza kuwa, polisi ya nchi hiyo imefanikiwa kuwaangamiza magaidi 10 katika mkoa wa Al-Anbar nchini humo.

Thursday, January 17, 2013

Wanamgambo Algeria wazima oparesheni ya jeshi




Kiwanda cha kusafisha gesi asilia walikotekwa nyara wageni Algeria
Wanamgambo nchini Algeria wanasema wamefanikiwa kuzima shambulizi la Jeshi la Algeria lililokuwa na lengo la kuwanusuru makumi ya raia wa kigeni waliotekwa nyara jana wakiwemo raia wa Ufaransa, Uingereza na Marekani.
Imearifiwa kuwa, Jumatano usiku wanajeshi wa Algeria walijaribu kuingia katika kiwanda cha kusafisha gesi asilia katika mji wa In Amenas mashariki mwa nchi hiyo ambako wanamgamabo hao wanawashikilia makumi ya raia wa kigeni.
Mapema jana Jumatano alfajiri wanamgambo 20 waliokuwa na silaha nzito nzito walishambulia basi ambalo lilikuwa limewabeba raia wa kigeni wafanyao kazi katika kiwanda cha gesi. Katika tukio hilo raia mmoja wa Uingereza na mwingine wa Ufaransa waliuawa na wengine 41 kutekwa nyara. Raia wengine wa kigeni waliotekwa nyara katika tukio hilo ni kutoka Ireland, Japan na Norway. Wanamgambo hao wanasema kwamba watawaachilia huru mateka hao salama salimini kwa sharti la Ufaransa kusitisha mashambulizi yake ya kijeshi nchini Mali.

Iran kutuma meli za kivita Bahari ya Mediterranean




Manowari za kivita za Jeshi la Wanamaji la Iran
Kamanda wa Jeshi la Wanamaji la Iran Admeli Habibollah Sayyari amesema msafara wa 24 wa manowari za kivita za Jamhuri ya Kiislamu utaelekea katika Bahari ya Mediterranean hivi karibuni.
Akizungumza Jumatano, Admeli Sayyari amesema msafara huo wa meli za kivita utalinda doria eneo la kaskazini mwa Bahari ya Hindi, Ghuba ya Aden, Bab-el-Mandeb, Bahari ya Sham, Mfereji wa Suez na Bahari ya Mediterranean kwa muda wa miezi mitatu.
Kamanda huyo ameongeza kuwa msafara wa 23 wa manowari za kivita za Jamhuri ya Kiislamu utarejea nchini wiki ijayo.
Akiashiria mazoezi ya hivi karibuni ya jeshi la wanamaji, Admeli Sayyari amesema maneva hiyo ilionyesha uwezo mkubwa wa jeshi la wanamaji la Iran katika kukabilina na tishio lolote dhidi ya maslahi ya Jamhuri ya Kiislamu.

Friday, January 11, 2013

MITAMBO YA KURUSHIA MATANGAZO YA REDIO YA MASAFA YA KATI YAZINDULIWA HUKO BUNGI ZANZIBAR


 
Waziri wa Mawasiliano,Sayansi na Teknolojia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Prof.Makame M,Mbarawa wapili kushoto akisalimiana na Waziri wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Said Ali mbarouk mara alipowasili katika ufunguzi wa Kituo cha Kurushia Matangazo ya Redio masafa ya kati(MIDIUM F)huko Bungi Wilaya ya Kati Unguja.
 
Waziri wa Mawasiliano,Sayansi na Teknolojia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Prof.Makame M,Mbarawa akikunjuwa Kitambaa kuashiria ufunguzi wa Kituo cha Kurushia Matangazo ya Redio masafa ya kati(MIDIUM F)huko Bungi Wilaya ya Kati Unguja.ikiwa ni shamra shamra za Maadhimisho ya miaka 49 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
 
Waziri wa Mawasiliano,Sayansi na Teknolojia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Prof.Makame M,Mbarawa akitoa hotuba katika sherehe za  ufunguzi wa Mitambo ya Matangazo ya Redio masafa ya kati(MIDIUM F)huko Bungi Wilaya ya Kati Unguja.ikiwa ni shamra shamra za Maadhimisho ya miaka 49 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
 
Waziri wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Said Ali mbarouk akitoa hotuba ya  kumkaribisha Waziri wa Mawasiliano,Sayansi na Teknolojia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Prof.Makame M,Mbarawa katika sherehe za ufunguzi wa  Mitambo ya Matangazo ya Redio masafa ya kati(MIDIUM F)huko Bungi Wilaya ya Kati Unguja.

Thursday, January 10, 2013

Mshukiwa wa mauaji Rwanda awakataa majaji



Mshukiwa wa mauaji Rwanda awakataa majaji
Mshukiwa wa mauaji ya kimbari nchini Rwanda Leon Mugesera amefungua kesi akitaka majaji wawili kati ya watatu wanaosikiliza kesi yake waondolewe.
Mugesera alifikishwa kizimbani katika Mahakama Kuu ya Rwanda lakini punde baada ya kuwasili hapo alifungua kesi akitaka majaji Athanase Bakuzakundi na Eugene Ndagijimana wazuiwe kusikiliza kesi yake. Amesema kwa mujibu wa sheria ya taratibu za mahakama, majaji hao hawana haki ya kusikiliza kesi yake kwani waliwahi kusikiliza kesi zake ambazo alishindwa.
Mahakama inatazamiwa kutoa uamuzi wake leo Alkhamisi kuhusu pingamizi hiyo ya Mugesera ambaye alirejeshwa Rwanda kutoka katika maficho yake nchini Canada.
Mugesera anakabiliwa na mashtaka ya kushiriki katika mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 nchini Rwanda.

Drone’ ya Marekani yaua watu wanne Pakistan



‘Drone’ ya Marekani yaua watu wanne Pakistan
Watu wanne wameuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa kufuatia hujuma ya ndege isiyo na rubani ya Marekani yaani Drone katika eneo la Waziristan Kaskazini nchini Pakistan.
Duru zinaarifu kuwa ndege hiyo imevurumisha makombora manne katika nyumba moja na kusababisha maafa na hasara mapema leo asubuhi.
Mara kwa mara ndege zisizo na rubani za Marekani hutekeleza mashambulizi katika maeneo kadhaa ya Pakistan kwa kisingizio cha kupambana na magaidi. Hata hivyo wahanga wakuu wa hujuma hizo za Marekani ni raia wakiwemo wanawake na watoto wasio na hatia.
Marekani inatekeleza hujuma za ndege zisizio na rubani katika nchi kadhaa za Kiislamu kama vile Afghanistan, Yemen na Somalia kwa kisingizio hicho hicho cha kupambana na ugaidi lakini wahanga wakuu huwa ni raia.

Rais Farole wa Puntland ajiongezea muhula


Rais Farole wa Puntland ajiongezea muhula
Rais wa eneo la Puntland lenye mamlaka ya ndani kaskazini mashariki mwa Somalia amejiongezea muda wa kutawala hadi Januari mwaka ujao wa 2014.
Akizungumza mjini Bodsaso, Rais Abdulrahman Mohammad Farole wa Puntland amesema ataendelea kutawala baada ya muhula wake kumalizika mwezi huu.
Farole amesema katiba inamruhusu kuongeza muhula wake kwa muda wa mwaka mmoja.
Wapinzani wanamlaumu rais huyo wa Puntland kuwa amekiuka sheria.
Eneo la Puntland lilijitangazia mamlaka ya ndani mwaka 1998 na limekuwa likishuhudia amani pamoja na kuwepo vita katika maeneo ya kati na kusini mwa Somalia.
Eneo la Somaliland lililoko kaskazini mwa Somalia tayari limeshajitangazia uhuru kamili ingawa bado halijatambuliwa na Umoja wa Mataifa.

Mapigano makali yajiri katikati mwa Mali

Mapigano makali yajiri katikati mwa Mali
Wanajeshi wa Mali wamepambana vikali na wanamgambo wanaokalia eneo la kaskazini katika mji wa Konna ulioko katika eneo la katikati mwa nchi hiyo.
Wakaazi wa Konna wanasema siku ya Jumatano kulikuwa na ufyatulianaji risasi wa masaa kadhaa kati ya waasi na wanajeshi wa serikali.
Mapigano hayo yamejiri masaa 48 baada ya vikosi vya serikali kujaribu kuudhibti mji huo.
Duru mpya ya mashambulizi ya waasi inajiri baada ya mazungumzo ya amani kati ya pande hasimu kuakhirishwa. Mazungumzo hayo yalikuwa yaanze leo katika mji mkuu wa Burkina Faso, Ouagadougou.

Wafanyakazi wa majumbani TZ wakabiliwa na matatizo


Wafanyakazi wa majumbani TZ wakabiliwa na matatizoWafanyakazi wa majumbani nchini Tanzania wanakabiliwa na changamoto kubwa ya kuweza kuwakomboa dhidi ya matatizo yanayowakabili licha ya kwamba sheria za kazi zinawatambua. Hayo yamedokezwa na Ofisi ya Shirika la Kazi la Umoja wa Mataifa –ILO- nchini Tanzania. Mratibu wa mpango wa misaada ya maendeleo katika ofisi ya ILO nchini Tanzania, Anne-Marie Kiaga amesema changamoto hizo ni za pande tatu yaani usimamizi wa sheria, waajiriwa wenyewe pamoja na waajiri.

Wednesday, January 9, 2013

Waasi wa Seleka wazungumza na wakuu wa CAR


Waasi wa Seleka wazungumza na wakuu wa CAR
Mazungumzo kati ya muungano wa waasi wa Seleka na wawakilishi wa serikali ya Jamhuri ya Afrika ya Kati yameanza leo huko Libreville mji mkuu wa Gabon. Mazungumzo hayo yanafanyika chini ya upatanishi wa nchi za eneo la katikati mwa bara la Afrika. Imeelezwa kuwa, ajenda kuu ya mazungumzo hayo ni kujadili kwa kina makubaliano yaliyofikiwa hapo awali kati ya pande hizo mbili katika miaka ya 2007 na 2011. Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Jamhuri ya Congo Brazzaville Basile Ikouébé ambaye ni Mwenyekiti wa mazungumzo hayo amezitaka pande mbili kuheshimu sheria za Umoja wa Afrika zinazopiga marufuku kuondoshwa kiholela tawala zilizopo madarakani.

Watoto walemavu waongezeka Marekani



Watoto walemavu waongezeka MarekaniViongozi wa Idara ya Afya ya Marekani wametangaza kuwa, mtoto mmoja mwenye ulemavu na upungufu wa viungo huzaliwa kila baada ya dakika tano nchini humo.
Coleen A. Boyle Mkurugenzi wa National Center on Birth Defects and Delevopmental Disabilities (NCBDDD) huko Atlanta Marekani amesema kuwa, kila dakika nne na nusu huzaliwa mtoto mwenye ulemavu na tatizo hilo huchangia asilimia ishirini ya vifo vya watoto wachanga nchini humo. Coleen Boyle ameongeza kuwa, watoto wanaozaliwa wakiwa na ulemavu na upungufu wa viungo wanakabiliwa na hatari zaidi ya kupatwa na maradhi. Amesema kuwa, mmoja kati ya kila watoto wachanga 35 wanaozaliwa nchini Marekani, huzaliwa akiwa kilema.

Polisi Afrika Kusini washambulia waandamanaji


Polisi Afrika Kusini washambulia waandamanaji
Polisi nchini Afrika Kusini wametumia risasi za plastiki kujaribu kuwatawanya wafanyakazi wa mashamba ambao wameitisha mgomo kutokana na mishahara duni katika mashamba ya zabibu huko mkoa wa Cape Magharibi.
Jumatano hii mamia ya wafanyakazi wa mashamba hayo waliwarushia mawe polisi na kufunga barabara kadhaa kwa kuchoma moto matairi katika eneo hilo lililo kilomita 100 kutoka mji wa Cape Town.
Wafanyakazi hao wanataka mshahara wao wa dola nane kwa siku uongezwe maradufu. Vibarua hao ambao hufanya kazi kwa msimu kila mwaka hubakia bila ajira kwa miezi kadhaa baada ya kumaliza kazi zao.
Mwaka uliopita wa 2012 Afrika Kusini ilikumbwa na migomo kadhaa ya wafanyakazi waliokuwa wakidai nyongeza ya mishahara.

Shughuli za kukusanya maoni ya katiba TZ zachafuka


Shughuli za kukusanya maoni ya katiba TZ zachafukaMwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba nchini Tanzania amejikuta mashakani baada ya kutoa agizo la kupinga kutolewa baadhi ya maoni na wananchi. Jaji Mustaafu Joseph Warioba anayeongoza tume hiyo yenye dhima ya kukusanya maoni kuhusu katiba mpya ameagiza maafisa kutopokea maoni ya makundi maalumu. Warioba amesema watu watoe maoni yao binafsi bila kufungamana na makundi yoyote. Hatua hiyo imemuweka pabaya jaji huyo mustaafu baada ya makundi ya kutetea haki za binadamu kusema kuwa, agizo hilo ni ukiukaji wa haki ya kujieleza.

Sakata ya Polisi Feki Kenya yalitikisa jeshi la polisi


Sakata ya Polisi Feki Kenya yalitikisa jeshi la polisi
Sakata ya kuweko afisa bandia wa polisi, Joshua Karianjahi Waiganjo aliyehudumu kwa takriban miaka mitano kama afisa wa ngazi za juu mkoani Rift Valley katika jeshila polisi huko nchini Kenya imeendelea kuwaandama wakuu wa polisi katika mikoa kadhaa ya nchi hiyo. Hapo jana Inspekta Mkuu wa Polisi David Kimaiyo aliwafuta kazi maafisa kadhaa wa ngazi za juu katika jeshi la polisi akiwemo Mkuu wa polisi katika mkoa wa Rift Valley, John Mbijiwe. Shoka hilo pia limemuangukia afisa mkuu wa kitengo cha kupambana na wizi wa mifugo Remi Ngungi. Imedaiwa kuwa,

Tuesday, January 8, 2013

Mkutano wa Madhehebu za Kiislamu kufanyikaTehran


Ayatullah Mohsen Araki
Ayatullah Mohsen Araki
Mkutano wa Kukurubisha Pamoja Madhehebu za Kiislamu unatarajiwa kufanyika hivi karibuni hapa mjini Tehran. Ayatullah Mohsen Araki Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kukurubisha Pamoja Madhehebu za Kiislamu ambaye yuko safarini mjini London Uingereza amesema kuwa, mkutano huo utafanyika tarehe 28 na 29 za  mwezi huu wa Januari hapa mjini Tehran. Ayatullah Araki amesema kuwa, wageni kutoka nchi 100 duniani wanatarajiwa kushiriki katika mkutano huo. Ameongeza kuwa, mkutano huo utafuatilia mikakati na maazimio yaliyopasishwa katika mkutano uliopita. Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kukurubisha Pamoja Madhehebu za Kiislamu ameashiria mwamko wa Kiislamu katika ulimwengu wa Kiarabu na kusema kuwa, Wamagharibi wanafanya njama za kuzusha fitina na mifarakano baina ya Waislamu hivyo Waislamu wanapaswa kuwa macho na njama hizo.

Jeshi la Israel lashambulia Ukingo wa Magharibi



Jeshi la Israel lashambulia Ukingo wa Magharibi Kwa mara nyingine askari wa utawala wa Kizayuni umefanya mashambulizi dhidi ya maeneo tofauti ya Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na kuwatia mbaroni Wapalestina wasiopungua 4. Duru za habari za Palestina zinaarifu kuwa, jana pia askari hao walivamia mji huo na kuwatia mbaroni Wapalestina 13 na kufanya idadi ya Wapalestina waliotiwa mbaroni ndani ya kipindi cha siku mbili kuwa 17. Hii ni katika hali ambayo, karibu kila siku askari hao huyavamia maeneo tofauti ya raia wa Palestina na kuwatia mbaroni raia hao wa maeneo hayo. Ni vyema kuashiria hapa kwamba,

Wakimbizi wa Somalia waanza kurejea



Wakimbizi wa Somalia waanza kurejeaWakimbizi wa Somalia waliopata hifadhi katika nchi jirani sasa wameanza kurejea makwao baada ya hali ya usalama kuboreka.
Hayo yamedokezwa na Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa huko Somalia, Balozi Augustine Mahiga.
Balozi Mahiga amesema kuwa wakimbizi hao wa Somalia wanarejea katika nchi yao kwa hiari yao wenyewe kutokana na kuimarika kwa hali ya usalama.
Hata hivyo Balozi Mahiga amesema kuwa, kurejea wakimbizi hao ni changamoto kwa serikali ya Somalia kwa sababu haijajiandaa ipasavyo.

Thursday, January 3, 2013

22 wauawa katika mapigano huko Darfur, Sudan



22 wauawa  katika mapigano huko Darfur, SudanWatu 22 wameuawa na wengine 25 kujeruhiwa katika mapigano kati ya raia na watu wenye silaha katika jimbo la Darfur magharibi mwa Sudan. Duru za habari zimemnukuu msaidizi wa gavana wa jimbo la Darfur Sediq Abdel-Nabi kuwa, wapiganaji wa waasi wa Harakati ya Ukombozi wanaoendesha shughuli zao za uasi nchini Sudan, walifanya mashambulizi dhidi ya eneo la Zureiqat magharibi mwa wilaya ya Samaha katika jimbo hilo na kuwateka nyara watoto watatu na wanawake 6. Kiongozi huyo amesema kuwa, kufuatia tukio hilo, wakazi wa eneo hilo walijaribu kuwakomboa mateka hao, hali iliyopelekea kuzuka kwa mapigano makali kati yao na wapiganaji wa Harakati ya Ukombozi na kupelekea watu 22 kuuawa na  wengine 25 kujeruhiwa.

Maandamano Makka dhidi ya Aal Saud



Maandamano Makka dhidi ya Aal SaudIdadi kubwa ya watu wamefanya maandamano katika Mji Mtakatifu wa Makka kupinga utawala wa kifalme nchini Saudi Arabia.
Aidha maandamano sawa na hayo yameripotiwa kufanyika katika mji wa Buraidah kaskazini kati mwa nchi hiyo.
Katika maandamano hayo yaliyofanyika Jumanne katika miji miwili, wananchi walitoa nara za kutaka upinduliwe utawala wa ukoo wa Aal Saud. Halikadhalika waandamanaji wametaka wafungwa wote wa kisiasa waachiliwe huru. Maandamano yameshadidi katika siku za hivi karibuni nchini Saudia hasa katika Mkoa wa Mashariki wenye utajiri wa mafuta ambapo kijana aliyekuwa akiandamana aliuawa shahidi Desemba 31.

Maandamano Makka dhidi ya Aal Saud


Maandamano Makka dhidi ya Aal SaudIdadi kubwa ya watu wamefanya maandamano katika Mji Mtakatifu wa Makka kupinga utawala wa kifalme nchini Saudi Arabia.
Aidha maandamano sawa na hayo yameripotiwa kufanyika katika mji wa Buraidah kaskazini kati mwa nchi hiyo.
Katika maandamano hayo yaliyofanyika Jumanne katika miji miwili, wananchi walitoa nara za kutaka upinduliwe utawala wa ukoo wa Aal Saud. Halikadhalika waandamanaji wametaka wafungwa wote wa kisiasa waachiliwe huru. Maandamano yameshadidi katika siku za hivi karibuni nchini Saudia hasa katika Mkoa wa Mashariki wenye utajiri wa mafuta ambapo kijana aliyekuwa akiandamana aliuawa shahidi Desemba 31.

Mabeberu wanakosea kutathimini uwezo wa Hizbullah


Mabeberu wanakosea kutathimini uwezo wa Hizbullah
Katibu Mkuu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Lebanon Hizbullah Sayyid Hassa Nasrullah amesema kuwa, mabeberu wakiongozwa na Marekani na utawala haramu wa Kizayuni, wanakosea kutathmini uwezo wa harakati hiyo. Amesema wapiganaji shupavu wa Harakati ya Hizbullah hawategemei uwezo wao wa makombora pekee, bali wanategemea imani yao kwa Mwenyezi Mungu, Mtume Muhammad (SAW) na kumpenda na kumuenzi mjukuu wa Mtume Imam Hussein (as). Katibu Mkuu wa Hizbullah ameyasema hayo leo katika maombolezo ya siku ya Arobaini ya Imam Hussein (as),

Waislamu washambuliwa na kuteswa Marekani


Waislamu washambuliwa na kuteswa  MarekaniVitendo vya ukandamizaji, utesaji na ushambuliaji dhidi ya Waislamu vimeongezeka kwa kasi kubwa nchini Marekani. Televisheni ya Russia Today imeinukuu Polisi ya Marekani FBI ikisema kuwa, mashambulizi yanayosababishwa na chuki dhidi ya Waislamu nchini Marekani yaliongezeka kwa asilimia 50 mwaka 2010. Maisha ya Waislamu yamekuwa hatarini zaidi nchini humo tokea lilipotokea shambulio la Septemba 11, na Waislamu wa Marekani na wahajiri walioko nchini humo wamekuwa wakikabiliwa na vitendo vya kibaguzi, ukandamizaji, utesaji na wengine kupigwa bila ya hatia yoyote,

Tuesday, January 1, 2013

Mai Mai walia na mazungumzo Congo


Mai Mai walia na mazungumzo Congo Wanamgambo wa Mai Mai katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wametoa wito wa kujumuishwa katika mazungumzo ya amani baina ya serikali na waasi wa M23. Joseph Assanda mmoja wa viongozi wa wanamgambo wa Mai Mai katika Jimbo la Kivu Kusini amesema kuwa, kundi lao linapaswa kujumuishwa katika mazungumzo ya amani baina ya serikali na M23. Hayo yanajiri katika hali ambayo, mazungumzo ya waasi wa M23 na serikali ya Kinshasa yaliyokuwa yakifanyika mjini Kampala Uganda, yameendelea kukosolewa na wapinzani ambao wanataka makundi mengine ya upinzani yajumuishwe katika mazungumzo hayo. Wakati huo huo,

Waandishi wa habari 121 waliuawa mwaka 2012


Waandishi wa habari 121 waliuawa mwaka 2012
Jim Boumelha Mkuu wa Muungano wa Kimataifa wa Waandishi wa Habari amesema kuwa, jumla ya waandishi wa habari 121 waliuawa kwenye matukio mbalimbali yaliyojiri katika pembe zote za dunia mwaka 2012. Akitoa taarifa hiyo hapo jana nchini Ubelgiji, Boumelha amesema kuwa, waandishi hao wa habari waliuawa kwenye machafuko au matukio mbalimbali wakati wa kutekeleza majukumu yao ya kikazi.
Mkuu wa Muungano wa Kimataifa wa Waandishi wa Habari amezitaka serikali zote ulimwenguni kuchukua hatua za kivitendo za kuzuia mauaji dhidi ya waandishi wa habari ambao amesema wana jukumu muhimu la kufichua na kueleza uhakika wa mambo na kuufikisha mbele ya fikra za walio wengi.
Kwa mujibu wa taarifa ya Jim Boumelha nchi za Somalia, Pakistan na Mexico zilikuwa hatari zaidi katika shughuli za waandishi wa habari mwaka 2012.

Waasi wa Seleka watakiwa kufanya mazungumzo



Waasi wa Seleka watakiwa kufanya mazungumzo
Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Ufaransa amewataka viongozi wa Jamhuri ya Afrika ya Kati na Muungano wa Waasi wa Seleka wahitimishe mapigano na kukaa katika meza ya mazungumzo. Laurent Fabius ametoa wito pia wa kuundwa serikali ya muungano katika nchi hiyo ya Afrika ya Kati. Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Ufaransa amenukuliwa na mtandao wa Intaneti wa wizara hiyo akisema kwamba, kwa sasa kufanyika mazungumzo baina ya waasi wa Seleka na serikali ya Rais Francois Bozize wa nchi hiyo ndio njia bora kabisa ya kuupatia ufumbuzi mgogoro wa nchi hiyo.

Kikwete: Hatua ya kwanza ya katiba mpya imekamilika


Kikwete: Hatua ya kwanza ya katiba mpya imekamilika
Rais Jakaya Kikwete wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amesema kuwa, Tume ya Mabadiliko ya Katiba imekamilisha hatua ya kwanza ya kukusanya maoni ya mtu mmoja mmoja nchi nzima na kwamba, hatua inayofuata ni ya kukusanya maoni ya makundi maalumu. Akizungumza kwa mnasaba wa kuwadia mwaka mpya wa 2013 Miladia, Rais Kikwete amesema, Bunge la Katiba, litakaa Novemba mwaka huu kupitisha mapendekezo ya Katiba Mpya. Rais Kikwete amesisitiza kwamba, kama kila kitu kitakwenda kama inavyotarajiwa, Katiba Mpya iliyotokana na maoni na matakwa ya wananchi itapatikana ifikapo mwaka 2014.