Terry jones mwenye miaka 61, alikamatwa siku ya jumatano katika mji wa Mulberry, karibia na Tampa, anakabiriwa na mashtaka ya kusafirisha mafuta pamoja na bunduki waziwazi kinyume na sheria .
Taarifa za wana usalama zinasema mchungaji terry alikuwa anaendesha Pickup yenye tela lililobeba jiko la kuchomea nyama, Qurani zilizolowa mafuta ya taa, pamoja na chupa za ziada za mafuta.
kwa mujibu ya website ya Mchungaji Terry alikuwa na mpango wa kuchoma Qurani 2998, kwenye eneo hilo la Tampa bay siku ya jumatano, ambapo kila kopi moja itakuwa inawakilisha kila mtu moja aliyekufa katika tukio hilo la septemba 11.
Mchungaji huyo alikamatwa na mshirika mwenzake mchungaji Marvin Sapp, 44, dakika chache kabla hawajaanza zoezi lao.
Mwaka 2010 mchungaj huyo wa Dove World Outreach Centre, alitishia kuchoma kopi za Qurani ambapo tukio hilo lilileta mtafaruku mkubwa na vurugu ndani na nje ya marekani kabla hajaahirisha mpango huo.
2011 jumuiko lake lilichoma Quran na mwaka uliofatia wakatangaza sinema ya kuukashifu uislamu ambapo matokeo yake yalisababisha mtafaruku mkubwa katika nchi mbalimbali duniani.
mchungaji Terry Jones akiwa chini ya ulinzi |
No comments:
Post a Comment