skip to main |
skip to sidebar
Asasi za Kiislamu zaitaka Nigeria kuchunguza mauaji
Taasisi za Kiislamu na za kutetea haki za binadamu nchini Nigeria
zimeitaka serikali ya Abuja kufanya uchunguzi kuhusiana na mauaji ya
makumi ya watu wanaoshukiwa kuwa wanachama wa kundi la Boko Haram.
Jumuiya hizo zimeashiria mauaji ya hivi karibuni ya makumi ya watu mjini
Abuja wanaoshukiwa kuwa wanachama wa Boko Haram na kusisitiza kwamba,
kuna utata katika tukio hilo hivyo kuna haja ya kufanyika uchunguzi wa
kina kuhusiana na mauaji hayo. Taasisi za Kiislamu na za kutetea haki za
binadamu nchini Nigeria zimetangaza kuwa, kuna udharura wa kufanyika
uchunguzi kuhusiana na mauaji hayo. Wakati huo huo, Taasisi ya Kitaifa
ya Haki za Binadamu nchini Nigeria imetangaza kuwa, uchunguzi kuhusiana
na mauaji hayo tayari umeshaanza. Kundi la Boko Haram linahusishwa na
mashambulio mengi ya kigaidi nchini Nigeria. Boko Haram ni kundi lenye
misimamo ya kufurutu mipaka nchini Nigeria ambalo kutokana na kuwa na
ufahamu mbaya na potofu kuhusiana na Uislamu, limeitumbukiza nchi hiyo
katika dimbwi la machafuko na mauaji sambamba na kuzusha hitilafu za
kidini na kikabila nchini humo
No comments:
Post a Comment