Mahakama ya jinai ya Misri imekubaliana na suala la
kuzuiwa mali za baadhi ya viongozi wa ngazi za juu wa harakati ya
Ikhwanul Muslimin ya nchini humo kwa tuhuma za mauaji na kuchochea
machafuko.
Mahakama ya jinai ya Misri Jumanne hii imeafiki ombi
lililokuwa limewasilishwa na mwendesha mashtaka mkuu wa nchi hiyo kwa
ajili ya kuzuiwa mali za viongozi na maafisa wa ngazi ya juu wa Ikhwanul
Muslimin.
Hisham Barakat mwendesha mashtaka wa Misri, awali aliiomba
mahakama ya jinai ya nchi hiyo ikubali kuzuiwa mali za viongozi kadhaa
wa ngazi za juu wa harakati ya Ikhwanul Muslimin kutokana na tuhuma hizo
wakiwemo Muhammad Badie kiongozi wa kundi hilo, naibu wake Khairat
Shater, Mahmud Izzat Ibrahim, Mahdi Akef, Mohamed Saad al Katatni,
Rashad al Bayumi, Issam al Aryan na viongozi wengine kadhaa wa ngazi ya
juu wa harakati hiyo.
Viongozi wengi wa Ikhwanul Muslimin wametiwa mbaroni katika
maeneo mbalimbali ya Misri baada ya wanajeshi wa nchi hiyo kumpindua
madarakani Muhammad Morsi, Rais halali wa nchi hiyo.
No comments:
Post a Comment