Binti
wa kinigeria Obabiyi Aishah Ajibola mwenye umri wa miaka 21, jana
ametangazwa kuwa mshindi wa shindano la Miss World Muslimah wa mwaka
2013 lililofanyika mjini Jakarta,Indonesia.
Mabinti
20 kutoka nchi sita ndio waliofanikiwa kuingia fainali ambapo washiriki
wote walivaa hijabu na mavazi yaliyostiri maungo yao. Baada ya kuonesha
watazamaji na wasomi wa kiislamu, jopo la majaji lilimchagua Obabiyi
Aishah Ajibola kutoka Nigeria kuwa mshindi. Vigezo vilivyotumika kumpata
mshindi ni Ufasaha wa kusoma Qurani na Maoni yao juu ya Uislamu katika
Dunia ya kisasa.
Baada ya kusikia jina lake kama mshindi Obabiyi Aishah Ajibola, alilia
kwa furaha na kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa yeye kuwa mshindi. “Jambo
hili hasa si kushindana bali sisi tunajaribu tu kuonesha Dunia kwamba
Uislamu ni mzuri” alisema Aishah.
Eka
Shanti ambaye ndiye aliyeanzisha shindano hili miaka mitatu iliyopita,
baada ya kupoteza kazi yake ya utangazaji wa Televisheni kwa kukataa
kuvua Hijabu akiwa anatangaza, anasema, "Mwaka huu tumefanya makusudi
lianze shindano letu kabla ya Miss World ili kuonesha kwamba kuna jambo
mbadala na mfano wa kuigwa kwa wanawake wa kiislamu.”
Shindano
hili lilianza mwaka 2011 likiwa na jina tofauti lilishirikisha
waindonesia peke yake. Shanti anasema baada vyombo vya habari
kulinganisha na Miss World tulibadilisha jina na tulikubali kuweka
wagombea wa kigeni mwaka huu. Washiriki wa nje ya Indonesia, walitoka
nchi za Iran, Malaysia, Bangladesh, Brunei, na Nigeria.
Obabiyi Aishah Ajibola |
Akivishwa Taji |
Akivishwa beji ya Miss world Muslimah |
Akishangilia kwa kushukuru baada ya kuangazwa mshindi |
Washiriki wa Miss World Muslimah |
No comments:
Post a Comment