Idara za usalama za Mamlaka ya Ndani ya Palestina zimetangaza
kuwa zinafanya kila linalowezekana ili kuzuia kuanza Intifadha ya Tatu
huko katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan. Idara za usalama za
Mamlaka ya Ndani ya Palestina zimedai kuwa kuanza Intifadha ya Tatu ya
Wapalestina kutazusha hali ya hofu na wasiwasi katika Ukingo wa
Magharibi wa Mto Jordan na kwamba idara hizo zitafanya kila ziwezalo ili
kuzuia kutokea intifadha hiyo. Mji wa Quds unaokaliwa kwa mabavu na
Wazayuni pamoja na msikiti mtukufu wa al Aqswa ambao ni kibla cha kwanza
cha Waislamu, Ijumaa iliyopita ilishuhudia wanajeshi wa utawala wa
Kizayuni wakijenga vituo mbalimbali vya upekuzi sambamba na kujiri
mapigano makali kati ya raia wa Kipalestina na wanajeshi wa Israel.
Matukio hayo yalijiri baada ya harakati ya muqawama ya Palestina Hamas
kutoa mwito kwa makundi mbalimbali ya wananchi wa Palestina huko katika
Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na katika mji wa Quds wa kuunga mkono
Intifadha ya Tatu ili kukabiliana na utawala wa Kizayuni.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment