
Kundi la wanamgambo la al Shabab la Somalia limetangaza kuwa ndilo lililohusika na shambulizi hilo huko Nairobi katika shopping Mall ya Westgate. Taarifa zinaeleza kuwa vikosi vya jeshi la Kenya vimeanza kumiminika katika eneo la tukio huku duru za usalama zikithibitisha kwamba milio ya kurushiana risasi inasikika kwenye eneo hilo.
Hapo jana Rais Uhuru Kenyata alisema kuwa, watu zaidi ya 40 wameuwa na wengine 150 kujeruhiwa kwenye tukio hilo na kwambaserikali yake itawasagasaga na kuwamaliza watu hao wenye silaha.
No comments:
Post a Comment