Social Icons

rss feed facebook twitter google plus linkedin youtube email

Sunday, September 29, 2013

Mlipuko waua watu 6 huko Tumbuktu Mali


Mlipuko waua watu 6 huko Tumbuktu Mali
Watu 6 wameuawa wakiwemo raia wawili na wengine kadhaa kujeruhiwa kufuatia mlipuko uliotokea karibu na kambi ya jeshi katika mji wa kihistoria wa Timbuktu nchini Mali. Afisa wa serikali katika eneo hilo ameeleza kuwa, mlipuko huo wa kutegwa garini umesababisha pia nyumba kadhaa kuporomoka na kutokea hasara kubwa.
Serikali ya Mali imelaani shambulio hilo lililotokea ikiwa zimepita siku chache tu tangu waasi wa Tuareg wanaopigana ili kulitenga eneo la Kaskazini wasimamishe mazungumzo na serikali, wakiituhumu kwamba imeshindwa kuheshimu makubaliano ya amani yaliyofikiwa kati ya pande mbili. Mwezi Juni viongozi wa kundi la Tuareg walifikia makubaliano na serikali ya mpito ya Mali yaliyopelekea kurejea jeshi kwenye mji wa Kidal na kufanyika uchaguzi wa rais.

No comments:

Post a Comment