Umoja wa Mataifa umesema kuwa mpango
wake wa kupeleka ndege ya kijasusi isiyo na rubani huko mashariki mwa
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo umecheleweshwa kwa miezi kadhaa.Ndege
hiyo itapelekwa katika eneo la Kongo lililoko karibu na mpaka wa Rwanda.
Vilevile Baraza la Usalama la Umoja wa
Mataifa limetangaza kuwa, licha ya kurejea nyuma waasi wa M23 huko
Mashariki mwa Kongo lakini bado eneo hilo halina amani na usalama. Marry
Robinson, Mwakilishi maalum wa UN katika eneo la Maziwa Makuu ameliomba
baraza hilo lizishinikize nchi za Rwanda, Kongo, Uganda na Burundi
zifanye mazungumzo ili kuimarisha amani na usalama wa kudumu kwenye eneo
hilo.
No comments:
Post a Comment