Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la
Umoja wa Mataifa limesema kuwa maelfu ya Warundi waliokuwa wakiishi
katika nchi jirani ya Tanzania wamerejeshwa nchi kwao kwa nguvu katika
siku 30 zilizopita. Catherine Huck, Kamishna wa UNHCR amesema kwamba, ni
vigumu kujua idadi ya Warundi waliofukuzwa kutoka Tanzania lakini kwa
uchache ni watu kati ya elfu 20 hadi elfu 30.
Karibu Warundi milioni moja walivuka
mpaka na kuingia Tanzania wakati wa vita vya ndani vya mwaka 1993.
Ingawa wakimbizi wengi wa Burundi walirejea nchini kwao baada ya vita
hivyo kuisha mwaka 2006 lakini baadhi yao bado wanaishi nje ya nchi
ikiwemo Tanzania.
No comments:
Post a Comment