Mtu mmoja ameuawa na wengine 14 kujeruhiwa baada ya kutokea
mripuko wa guruneti, Kigali mji mkuu wa Rwanda. Mripuko huo umetokea
zikiwa zimesalia siku tatu kabla ya kufanyika uchaguzi wa bunge nchini
humo. ACP Damas Gatare Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini Rwanda amesema
kuwa, watu watatu wanashikiliwa na jeshi la polisi kwa tuhuma za
kuhusika na mripuko huo. Hadi sasa hakuna mtu au kikundi chochote
kilichojitangaza kuhusika na mripuko huo. Viongozi wa Rwanda wametangaza
kuwa, miezi ya Julai na Agosti ilijiri miripuko miwili ya maguruneti
mjini Kigali, na kulituhumu kundi la waasi wa FDRL walioko Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Kongo kwa kutekeleza shambulio hilo. Uchaguzi wa Rwanda
umepangwa kufanyika siku ya Jumatatu, huku chama tawala cha Rwanda
Patriotic Front (RPF) kinachoongozwa na Rais Paul Kagame kinatarajiwa
kuibuka na ushindi wa kishindo kwenye uchaguzi huo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment