Mpango wa ujenzi wa msikiti umekuwa unakabiliwa na vikwazo vya utawala na ukosefu wa utashi wa kisiasa katika nchi hiyo yenye wakatoliki milioni mbili, ambapo idadi ya waislamu ni 50,000 tu.
Takribani watu 10,000 walihudhuria sherehe za uwekaji jiwe la msingi la msikiti, akiwemo waziri mkuu wa Slovenia bi Alenka Bratusek, waziri wa serikali ya Qatar ambayo inafadhili mradi huo na Meya wa Ljubljana, Zoran Jankovic, ambao kwa pamoja walisaidia kuweka jiwe la msingi. Wanawake wachache waliovaa hijabu walihudhuria katika uzinduzi wa msikiti huo.
Waziri mkuu huyo wa Slovenia aliuambia umati uliohudhuria kwamba ni ishara ya ushindi wa kila aina ya uvumilivu uliooneshwa na waislamu katika kipindi chote cha kukosa msikiti na kuongeza kwamba ulaya bila kuwa na uislamu haiwezi kuwa tajiri.
"Hii ina maana dunia ni yangu ," alisema Sahra Kacar , 44, ambaye alizaliwa mwaka ambao yalipelekwa maombi ya kwanza rasmi ya kujenga msikiti katika Ljubljana. "Tutakuwa na mahali sahihi pakufanyia ibada, badala ya kutumia kumbi mbalimbali za umma ." Alisema
Ombi
la ujenzi wa msikiti lilikuwa linashikiliwa na maafisa wa mitaa, ambao
baadhi yao walijaribu kulazimisha kura ya maoni juu ya suala hilo mwaka
2004. Watu 12,000 walisaini ombi la wito wa kura ya maoni ili pasi
jengwe msikiti, lakini Mahakama ya Katiba ya Slovenia ilikataa kwa
kusema itakuwa ni kinyume na katiba kwa misingi ya uhuru wa dini.
"
Tunafuraha kwa kuanza ujenzi huu Ljubljana , ambao utakuwa bora na
utakaojulikana na mji zaidi," Mufti Nedzad Grabus , Kiongozi wa juu wa
jamii ya Kiislamu ya Slovenia , aliiambia sherehe.
Ujenzi
wa msikiti unatarajiwa kuanza kwa kasi Novemba mwaka huu na unatarajiwa
kuchukua miaka mitatu kwa gharama ya dollar milioni 12. Asilimia 70 ya
fedha zitatolewa na serikali ya Qatar.
Mradi
huo umekuja wakati Slovenia ipo katika hali mbaya ya kifedha tangu
uhuru wa mwaka 1991, ambapo unatishia taifa kutafuta fedha kutoka EU na
Shirika la Fedha Duniani .Mradi wa ujenzi wa msikiti huo umewafanya
baadhi ya wasio kuwa waislamu kukasirika na kulaumu maamuzi ya kukubali
kujengwa.
No comments:
Post a Comment