Social Icons

rss feed facebook twitter google plus linkedin youtube email

Monday, September 23, 2013

Kuanza zoezi la kukusanywa silaha Sudan


Kuanza zoezi la kukusanywa silaha Sudan
Serikali ya Sudan imeanza kukusanya silaha na kuziwekea alama ili kuzuia ukosefu wa amani na machafuko nchini humo. Abdallah Hamdan Mkuu wa kamati inayosimamia mpango wa kukusanya silaha katika jimbo la Darfur magharibi mwa Sudan amesema kuwa hadi kufikia sasa silaha 135 zimekwishakusanya na kuwekwa alama katika maeneo manne ya Darfur. Hamdan ameongeza kuwa katika awamu ya kwanza, kamati hiyo imeazimia kukusanya na kuziwekea alama silaha elfu tatu.
Naye Salafuddin Saleh mkuu wa kituo cha upokonyaji silaha cha Sudan ametangaza kuanza zoezi la kukusanya na kuziwekea alama silaha katika majimbo ya Darfur ya Kusini na ya Magharibi na kwamba mpango huo utaendelea pia katika majimbo mengine ya Darfur na baadaye kuelekea katika maeneo mengine ya Sudan. Serikali ya Sudan inafanya juhudi za kurejesha amani na utulivu na pia kuzuia mapigano ya kikabila nchini humo kwa kukusanya silaha zilizokuwa zimetapakaa miongoni mwa baadhi ya watu.

No comments:

Post a Comment