Kamanda wa Polisi wa Nairobi
ametangaza kukombolewa idadi ya watu kadhaa waliokuwa wakishikiliwa
mateka na wanamgambo wa al Shabab ndani ya jumba la kibiashara la
Westgate lililoko kwenye mtaa wa Westland jijini Nairobi nchini Kenya.
David Kimaiyo amesema kuwa, kikosi cha usalama cha Kenya kimefanikiwa
kutekeleza operesheni hiyo ya kuwaokoa baadhi ya watu waliokuwa
wakishikiliwa na wanamgambo wa al Shabab na kusisitiza kwamba operesheni
hiyo ya uokozi inaendelea kwa kasi. Wakati huohuo, Polisi ya Kenya
imeeleza kwamba inadhibiti ghorofa zote za jengo la kituo hicho cha
biashara. Taarifa hiyo imeeleza kuwa, baada ya masaa machache itafanyika
operesheni ya kumaliza kabisa tukio hilo lililodumu kwa siku tatu. Hadi
sasa inaelezwa kuwa, watu wasiopungua 69 wameuawa na wengine
wasiopungua 200 kujeruhiwa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment