Social Icons

rss feed facebook twitter google plus linkedin youtube email

Sunday, September 29, 2013

Boko Haram yauwa makumi ya wanachuo Nigeria


Boko Haram yauwa makumi ya wanachuo Nigeria
Wanamgambo wa Boko Haram wa huko Nigeria leo asubuhi wamekishambulia chuo cha kilimo cha Yobe cha kaskazini mashariki mwa nchi hiyo na kuwauwa kwa risasi zaidi ya wanachuo 50 waliokuwa wamelala chuoni hapo.
Kundi la wanamgambo wa Boko Haram katika wiki za hivi karibuni limekuwa likiwashambulia ovyo raia wa Nigeria katika kulipiza kisasi oparesheni za mashambulizi yaliyoanzishwa na jeshi la nchi hiyo dhidi yake.
Hadi kufikia sasa miili zaidi ya 50 ya wanachuo waliouliwa na Boko Haram ambao wengi wao ni wavulana tayari imehifadhiwa katika hospitali kuu ya jimbo la Yobe.
Mbali na kuwalenga raia, wanamgambo wa Boko Haram katika miezi ya hivi karibuni wamekuwa wakizishambulia shule kadhaa likiwemo shambulio walilolifanya kwenye shule moja huko Potiskum eneo lililoko umbali wa maili zisizopungua 30 kutoka eneo palipojiri shambulio la leo na kuua  wanafunzi 27 na mwalimu mmoja.

No comments:

Post a Comment