Wizara hiyo imesema itaimarisha ushirikiano na taasisi za serikali na jumuiya zisizo za serikali kwa ajili ya kuzuia mipango ya watu au makundi yanayowahamasisha wanawake kwenda Syria kwa ajili ya kutoa huduma ya ngono kwa makundi ya Kiwahabi. Wizara hiyo imesema inatayarisha mpango wa kutoa elimu na mafunzo ya kuzitahadharisha familia na wanawake wanaopelekwa Syria.
Alkhamisi iliyopita Waziri wa Mambo ya Ndani wa Tunsia Lotfi ben Jeddou alisema kuwa, wanawake wa Kitunisia wanaopelekwa Syria wamekuwa wakitumiwa kingono na wapiganaji wa kigeni wanaoungwa mkono na nchi za Magharibi dhidi ya serikali ya Damascus. Jeddou amesema wanawake hao hutumiwa na wanaume kadhaa wa Kisalafi na wengi wao hurejeshwa nchini wakiwa na mimba.
Wizara ya Afya ya Tunisia pia ilitangza jana kuwa idadi ya wasichana wa Kitunisia wanaopelekwa Syria kwa ajili ya kutumiwa na wapiganaji wa kisalafi imeongezeka. Wanawake hao wanapelekwa Syria kutoa huduma ya ngono kwa wapiganaji hao wa Kisalafu kufuatia fatuwa zinazotolewa na baadhi ya maulama wa Saudia Arabia wanaohalalisha suala hiyo linalopingana na mafundisho ya Kiislamu.
No comments:
Post a Comment