Social Icons

rss feed facebook twitter google plus linkedin youtube email

Friday, September 13, 2013

MWANAMKE ARUHUSIWA KUPANDA MAHAKAMANI NA NIQABU, BAADA YA MSUGUANO HAKIMU AWA MPOLE

Mwanamke wa mmoja wa kiislamu ameruhusiwa kupanda kizimbani katika mahakama ya kifalme ya blackfriars  bila ya kutoa Niqabu wakati wa uendeshwaji wa kesi yake, imeripotiwa na vyombo mbalimbali vya habari nchini Uingereza.

Inaelezwa alipoingia mahakamani hapo mwanamke huyo, alitakiwa aweke wazi sura yake na hakimu Peter Murphy aliyekuwa akiendesha kesi, lakini alikataa kufanya hivyo kwa kusema asingeweza kuweka sura yake wazi mbele ya wanaume.

Alipoombwa zaidi kufanya hivyo na hakimu, mwanamke huyo alisimamia msimamo wake kwamba hataondoa Niqabu kwa sababu za kidini. Mwanamke huyo ambaye hakutajwa jina lake kwa sababu za kisheria, ametajwa kuwa ni mkazi wa mji wa London. 

Baada ya msuguano mkali ilibidi hakimu  awe mpole na kumuamuru askari wa kike aliyewahi kumuona sura yake wakati alipopigwa picha baada ya kukakamatwa kwenda kumtambua mwanamke huyo.Zoezi la kwenda kumtambua sura yake lilifanyika katika chumba cha falagha katika mahakama hiyo ya blackfriars.Baadae afisa huyo wa polisi alirudi mahakamani na kutoa kiapo kwamba mtu aliyekuwepo ni sahihi.Mwanamke huyo aliyepanda kizimbani kutoa ushahidi, kesi hiyo imeahirishwa Jumatatu ijayo.

Akizungumzia kadhia hiyo mwanasheria Suzan Meek, anasema ni haki kuvaa Niqabu kwa mujibu wa mkataba wa nchi za ulaya wa haki za binadamu inayohusiana na mambo ya dini. "Ana haki kuvaa Niqabu sehemu ya wazi na falagha,na haki pia kuvaa mahakamani.hakuna sheria katika nchi hii inayopinga kuvaa Niqabu" alisema Suzan Meek.

Tukio hili limekuja baada ya chuo cha Birmingham Metropolitan College kupiga marufuku wanafunzi wa kike Kutovaa Niqabu wawapo ndani ya chuo hicho,kitendo ambacho kimesababisha malumbano makubwa na kupelekea waislamu kuandaa maandamano kushinikiza kuondolewa kwa sera hiyo chuoni hapo
mahakama ya kifalme ya blackfriars

No comments:

Post a Comment