Mazungumzo mapya ya amani kati ya serikali ya Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Kngo na waasi wa M23 mjini Kampala Uganda yanatarajiwa
kujadili mambo mengi lakini kubwa zaidi ni msamaha kwa waasi hao. Waziri
wa Ulinzi wa Uganda, Crispus Kyonga ambaye alifungua upya mazungumzo
hayo hapo jana amesema makubaliano ya mwisho yatafikiwa karibuni hivi.
Ajenda za mazungumzo hayo ni namna ya kuwarudisha waasi wa M23 jeshini
sanjari na kuhakikisha kwamba wakimbizi waliotoroka kufuatia machafuko
wanarudi katika maeneo yao. Dkt. Kyonga ambaye ndiye mpatanishi wa
mgogoro huo amesema serikali ya Kinshasa na waasi wana azma ya kufikia
mapatano na kusitisha machafuko na uasi mashariki mwa nchi. Mazungumzo
ya Kampala yalivunjika miezi kadhaa iliyopita baada ya Umoja wa Mataifa
kuidhinisha kikosi maalumu cha kikanda kuenda mashariki mwa DRC kwa
lengo la kupambana na makundi ya waasi hususan waasi wa M23 ambao mwaka
uliopita waliuvamia na kuuteka mji wa kistratejia wa Goma.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment