Serikali ya Kenya imetangaza kuwa, vikosi vya usalama vya nchi
hiyo vinadhibiti jengo la madula la Wesgate lililokuwa likidhibitiwa na
magaidi wa kundi la wanamgambo wa al-Shabab. Taarifa ya serikali ya
Kenya imesema kuwa, kwa sasa vikosi vya usalama vinapambana na gaidi
mmoja au wawili ambao wamebakia katika jengo hilo. Manoah Esipisu,
Msemaji wa serikali ya Kenya ametangaza kwamba, vikosi maalumu vya
usalama vilivyoko katika eneo hilo vinaendelea kusonga mbele bila
upinzani mkubwa. Aidha amesema kuwa, mateka wote waliokuwa wakishikiwa
na magaidi hao wamekombolewa na kwa sasa inafanyika operesheni ya
kumaliza kabisa tukio hilo lililodumu kwa siku tatu. Hadi sasa inaelezwa
kuwa, watu wasiopungua 69 wameuawa na wengine wasiopungua 200
kujeruhiwa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment