Habari kutoka Mali zinasema kuwa, mapambano makali yameshuhudiwa
kati ya wanajeshi wa serikali na waasi wa Tuareg katika mji wa Lere
katikati mwa nchi hiyo. Duru za habari zinaripoti kuwa, waasi hao ndio
walioanza kuwashambulia wanajeshi wa serikali kuanzia jana Jumatano
ingawa wao wamedai jeshi ndilo lililoanza kuwafyatulia risasi na
makombora ya mizinga. Makabiliano hayo yamepelekea waasi kadhaa kuuawa
huku wanajeshi 3 wa serikali wakijeruhiwa vibaya. Hii ni mara ya kwanza
kwa vita kama hivyo kutokea tangu pande mbili hizo kusaini makubaliano
ya amani mwezi Juni mwaka huu. Vita hivyo aidha vinatokea ikiwa imepita
wiki moja tu tangu rais mpya, Ibrahim Keita ashike rasmi hatamu za
uongozi wa nchi hiyo ya mgharibi mwa Afrika; jambo linaloashiria kibarua
kigumu kinachomsubiri kiongozi huyo katika juhudi zake za kutafuta
maridhiano ya kitaifa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment