Serikali ya Sudan imetishia kukata kabisa uhusiano wa
kidiplomasia na Marekani iwapo Washington itaendeleza siasa zake za
kijuba dhidi ya Khartoum. Indhari ya Sudan inafuatia hatua ya Marekani
ya kumzuia Rais Omar Hassan al-Bashir kuhudhuria mkutano wa Baraza Kuu
la Umoja wa Mataifa utakaoanza Jumapili ijayo mjini New York. Rais
Bashir alikuwa ameomba rasmi viza ya kusafiri Marekani kuhudhuria
mkutano huo lakini Washington ikalaani hatua hiyo na kusema Bashir
anapaswa kusafiri Uholanzi na kujisalimisha mbele ya mahakama ya ICC na
wala sio kwenda Umoja wa Mataifa. Sasa serikali ya Sudan kupitia Wizara
ya Mambo ya Nje imesema itamfukuza balozi wa Marekani mjini Khartoum na
pia kusimamisha biashara ya mafuta na Sudan Kusini iwapo Washington
haitobadili misimamo yake. Taarifa ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Sudan
imesema Marekani haipaswi kuzungumzia suala la haki za binadamu kwani
rekodi yake katika uwanja huo ni mbovu na yenye kutoa uvundo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment