Umoja wa Mataifa umesema kuwa watu elfu sita wanaikimbia Syria
kila siku kutokana na kushadidi mapigano nchini humo. Hayo yalisemwa
jana katika kikao cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa mjini New
York Marekani. Antonio Guterres, Kamishna Mkuu wa Masuala ya Wakimbizi
wa Umoja wa Mataifa amesema katika kikao hicho kuwa kamisheni yake
haijawahi kuona idadi ya wakimbizi ikiongezeka kwa kiwango cha kutisha
namna yote hiyo tangu miaka 20 iliyopita. Ivan Simonovic, Naibu wa
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anayehusika na masuala ya haki za
binadamu amedai kuwa, watu wasiopungua 92,901 waliuawa huko Syria kati
ya mwezi Machi mwaka juzi hadi mwishoni mwa mwezi Aprili mwaka huu,
miongoni mwao wakiwemo watoto zaidi ya 6,500. Amesema, inakadiriwa kuwa
watu elfu tano wanauawa huko Syria kila mwezi. Serikali ya Damascus
inasema kuwa, madola ya kigeni ambayo hayaitakii kheri Syria yamepeleka
makundi ya kigaidi na kuyasaidia kwa kila hali ili yafanye mauaji ya
raia na maafisa wa serikali nchini humo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment