Msahafu wa kihistoria
ulioandikwa kwa mkono umeonekana katika msikiti wa zamani ulioko Bodrum katika
mji wa bandari wa Mugla, huko nchini Uturuki.
Yüksel Kılınçarslan imam wa msikiti mkongwe uliojengwa mwaka 1737 wa Tepecik
ulioko Neyzen Tevfik Avenue, umebainika msahafu huo una umri wa miaka 1200, na
uligunduliwa katika chumba cha imamu katika msikiti huo wa zamani ulioko Bodrum. Msahafu huo
umekabidhiwa idara ya makumbusho ya mji wa Bodrum.
Msahafu huo utapelekwa maktaba ya mji wa İzmir baada ya kufanyiwa baadhi ya matengenezo.Imam
Kılınçarslan alisema kwamba uligunduliwa msahafu huo ukiwa umezungushiwa kitambaa.
“hatukutoa umuhimu wowote kwamba ilikuwa ni Qurani tunayoijua, lakini
nikagundua kuwa ni Qurani iliyoandikwa kwa mkono."
Utafiti uliofanywa na wanahistoria kuhusu msahafu huo unaonesha
kwamba ni wa miaka 1000 iliyopita. “Nilikwenda Ankara kuzungumza na viongozi na
walinambia niutoe kwa taasisi husika,” alisema Imam.
Msahafu huo ulioandikwa
mkono umepatikana katika msikiti huko Aegean ambako kuna misikiti mingi
iliyojengwa tangu kipindi cha utawala wa Khalifa sayyidna Uthman bin Afan
Aidha msahafu huo umepatikana na baadhi ya vitabu vya tafsiri
ya Qurani.
No comments:
Post a Comment