Sheikh
Ponda Akishuka kwenye basi la Magereza tayari kuingia Mahakamani
Kusikiliza kesi yake inayomkabili katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoani
Morogoro.
Sheikh Ponda
akiwa Chini ya Ulinzi Mkali wakati akiingia Mahakamani kusikiliza kesi
yake inayomkabili katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoani Morogoro.
Sheikh Issa Ponda akiingia Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoani Morogoro leo kusikiliza kesi yakeShekh Issa Ponda akiteta jambo na wakili wake Abdallah Nassoro
kundi
la waislam wakiwa mahakamani leo kusikiliza kesi ya Shekh Ponda
iliyokuwa imetajwa mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Morogoro.Shekh Issa Ponda alishtakiwa katika Mahakama Hiyo akikabiliwa na Mashtaka Matatu Ambayo inadaiwa aliyatenda Mkoani Morogoro katika Mkutano wa Hadhara mwezi uliopita.Kesi hiyo imearishwa tena Mpaka Tarehe 01.10.2013.Shekh Ponda amenyimwa dhamana hivyo Amerudishwa Rumande.Hata hivyo wakati wa kesi hiyo,wakili wa Shekh Ponda aliwasili ombi la kesi hiyo kuhamishiwa kisutu kutokana na jinsi mashtaka yalivyo.
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII HAPO CHINI
No comments:
Post a Comment