Social Icons

rss feed facebook twitter google plus linkedin youtube email

Wednesday, September 18, 2013

Russia, Marekani zatofautiana ripoti ya UN kuhusu Syria


Russia, Marekani zatofautiana ripoti ya UN kuhusu Syria
Marekani na Russia zimetofautiana kuhusu ripoti iliyotolewa na wachunguzi wa Umoja wa Taifa kuhusu matumizi ya silaha za kemikali huko Syria. Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa, Samantha Power amesema ripoti hiyo inaonyesha wazi kuwa, serikali ya Syria ndiyo iliyotumia silaha za kemikali Agosti 21 viungani mwa mji wa Damascus. Bi. Samantha amesema makombora yaliyotumiwa ni ya kitaalamu ambayo waasi hawawezi kuyapata. Naye balozi wa Russia katika umoja huo, Vitaly Churkin amesema kuwa, Ripoti hiyo ya wataalamu wa UN haijataja ni nani aliyetumia silaha hizo na hivyo madai ya Marekani hayana msingi wowote. Churkin amesema baadhi ya wapinzani wa Rais Asad ni makamanda wa zamani wa jeshi ambao waliondoka serikalini na rundo kubwa la silaha yakiwemo makombora na inawezekana walitumia makombora hayo ili ionekane kwamba serikali ndiyo iliyohusika.
Russia imesisitiza kuwa ina ushahidi wa wazi unaoonyesha wapinzani ndio waliotumia silaha za kemikali Agosti 21 dhidi ya raia ambapo zaidi ya watu 1000 waliuawa. Marekani, Uingereza na Ufaransa zinaanda rasimu ya azimio litakalopigiwa kura kwenye baraza la Usalama la Umoja wa Maraifa ingawa Russia imesema baadhi ya vipengee vya azimio hilo sharti vifutwe la sivyo italipigia kura ya veto.

No comments:

Post a Comment