Social Icons

rss feed facebook twitter google plus linkedin youtube email

Saturday, September 14, 2013

Rais wa Zanzibar Dakt. Shein Amtembelea Padri Hospitali Kuu Leo.


 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Padri Joseph Monesmo Magamba, wa Kanisa la Romani Katoliki Parokia ya Machui, alipofika katika
Hospitali ya Mnazi Mmoja kumpa pole,Mjini Unguja,baada ya kumwagiwa tindikali na watu wasiojulikana katika Mtaa wa Mlandege Mkoa wa Mjini Magharibi jana jioni, Padri alimwagiwa Tindikali alipokuwa akitoka kupata huduma ya Mtandao
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akimsikiliza Padri Joseph Monesmo Magamba,wa Kanisa la Romani Katoliki Parokia ya Machui,akitoa maelezo jinsi
alivyopata mkasa wa kutiwa Tindikali jana na watu wasiojulikanwa,katika mtaa wa Mlandege Mjini Unguja, alipofika katika Hospitali ya Mnazi Mmoja kumpa pole,ambapo amelazwa na kuapatiwa matibabu.
Mmoja wa Ngugu wa Padri Joseph Monesmo Magamba,wa Kanisa la Romani Katoliki Parokia ya Machui,akimueleza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,hisia zake kwa Uchungu kutokana na kitendo hicho cha kumwagiwa Tindikali na watu wasiojulikanwa kwamba zilichukuliwe hatua za kisheria na kukomeshwa Vitendo kama hivyo.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akiwafariji jamaa na wafuasi wa Padri Joseph Monesmo Magamba,wa Kanisa la Romani Katoliki Parokia ya Machui,waliofika katika Hospitali ya Mnazi Mmoja kumpa pole Padri huyo baada ya kumwagiwa Tindikali na Watu wasiojulikanwa jana jioni Mtaa wa Mlandege Mjni Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akiwafariji jamaa na wafuasi wa Padri Joseph Monesmo Magamba,wa Kanisa la Romani Katoliki Parokia ya Machui,waliofika katika Hospitali ya Mnazi Mmoja kumpa pole Padri huyo baada ya kumwagiwa Tindikali na Watu wasiojulikana jana jioni Mtaa wa Mlandege Mjni Unguja.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]

No comments:

Post a Comment