Wanajeshi wa Nigeria wasiopungua 40
wameuliwa na wengine 65 hawajulikani waliko katika mapambano kati yao na
wanamgambo wanaoaminika kuwa wa kundi la Boko Haram. Mapigano hayo
yalitokea Ijumaa iliyopita katika barabara ya Baga-Maiduguri kaskazini
mashariki mwa Nigeria. Uchunguzi umeanza ili kujua sababu ya kushindwa
oparesheni hiyo iliyopelekea kuuliwa wanajeshi wengi wa Nigeria. Afisa
wa jeshi la Nigeria aliyesimamia oparesheni hiyo maalumu dhidi ya
wanamgambo wa kundi la Boko Haram amefutwa kazi kufuatia kuuliwa
wanajeshi wengi. Jumapili iliyopita pia wanamgambo wanne wa Boko Haram
waliuliwa na kikosi cha oparesheni cha kiraia katika mji wa Mubi katika
jimbo la Adamawa huko mashariki mwa Nigeria.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment