Rais Hassan Sheikh Mahmoud wa Somalia amenusurika kuuawa leo katika shambulizi lililodaiwa kufanywa na wanamgambo wenye uhusiano na mtandao wa al Qaida dhidi ya msafara wake uliokuwa ukisindikizwa na vikosi vya jeshi. Rais wa Somalia alikuwa akikaribia kuwasili katika mji wa bandari wa Marka kusini mwa Mogadishu mji mkuu wa Somalia wakati wanagambo wa al Shabab walipourushia msafara wake maguruneti. Abdikadir Mohamed, Kamanda wa polisi ya Somalia amethibitisha kutokea shambulio hilo na kueleza kuwa Rais Hassan Sheikh Mahmoud amewasili salama salimini humo Marka umbali wa kilomita 90 kutoka Mogadishu.
Wanamgambo wa al Shabab wamesema wamewaua wanajeshi kadhaa na kuharibu magari mawili ya kijeshi yaliyokuwa kwenye msafara wa Rais wa Somalia ambao ulikuwa ukisindikizwa na askari jeshi wa kulinda amani wa Umoja wa Afrika na wa serikali ya nchi hiyo
No comments:
Post a Comment