Uchunguzi mpya wa maoni huko Marekani unaonyesha kushindwa Rais
Barack Obama wa nchi hiyo katika kupata uungaji mkono wa raia wa nchi
hiyo kuhusiana na suala la kuivamia kijeshi Syria. Uchunguzi mpya wa
maoni uliofanywa na shirika la habari ya Reuters na shirika la utafiti
la Ibson huko Marekani unaonyesha kuwa Rais Barack Obama ameshindwa
kuwashawishi Wamarekani kupitia mahojiano aliyofanya kwa njia ya
televisheni ili wamuunge mkono katika mashambulizi dhidi ya Syria.Kw amujibu wa matokeo ya uchunguzi huo wa maoni uliofanyika wiki iliyopita huko Marekani, theluthi tatu ya Wamarekani wanasisitiza kutatuliwa mgogoro wa Syria kupitia makubaliano ya kimataifa. Aidha uchunguzi huo wa maoni umeonyesha kuwa, asilimia 25 tu ya raia wa Marekani wanapinga kutatuliwa mgogoro wa Syria kwa njia za kidiplomasia.

















No comments:
Post a Comment