Social Icons

rss feed facebook twitter google plus linkedin youtube email

Monday, September 23, 2013

Milipuko yasikika ndani ya maduka ya Westgate



Milipuko yasikika ndani ya maduka ya Westgate Sauti nzito za ufyatuaji risasi na milipuko zimesikika katika jengo la maduka ya Westgate jijini Nairobi, Kenya  wakati  vikosi vya usalama vya nchi hiyo vilipoanzisha shambulio la mwisho dhidi ya wanamgambo wanaosemekana kuwa ni wa kundi la kigaidi la as-Shabab wenye silaha walioko ndani ya jengo hilo. 
Watu walioshuhudia wameeleza kuwa sauti ya milipuko mitatu mikubwa imesikika mapema leo katika jengo hilo la maduka la Westgate jijini Nairobi.
Vikosi vya Kenya vinajaribu kupambana na wanamgambo wa as Shabab waliovamia jengo hilo la biashara juzi  Jumamosi ambalo sehemu yake moja imetajwa kumilikiwa na Israel. Katika mashambulizi hayo ya as Shabab, karibu watu 70 wameuawa na wengine wanaokaribia 200 kujeruhiwa sambamba na kushikwa mateka wengine wengi.

No comments:

Post a Comment