Social Icons

rss feed facebook twitter google plus linkedin youtube email

Monday, September 30, 2013

TETESI: TAARIFA INAYODAI KUWA MAGAIDI WALIOSHAMBULIA WESTGATE HUENDA WALITOROKEA NJIA YA MAJI TAKA CHINI YA JENGO...tazama picha hapa

Wakati bado kuna maswali mengi kuhusu magaidi waliohusika na shambulio la Westgate kama kweli waliuawa kama isemavyo taarifa ya serikali ya Kenya, mtandao wa Mirror umetoa taarifa kuhusu tetesi za uwezekano wa magaidi hao kutorokea njia ya maji taka kutoka katika jengo hilo.


Westgate escape route
Ripota wa Sunday Mirror Russell Myers akiwa ndani ya handaki lenye njia ya maji taka kutokea jengo la Westgate

Mtandao huo umedai kuwa baadhi ya magaidi walitoroka kupitia njia ya maji taka iliyoko chini ya jengo la Westgate inayoenda kutokea katika mto Nairobi.

Kwa mujibu wa habari hiyo njia hiyo inaanzia eneo la maegesho ya magari katika jengo la Westgate na inaenda moja kwa moja kutokea katikati ya jiji la Nairobi. Magaidi hao wanahofiwa kutumia njia hiyo ya maji taka kutoroka na kuwaacha wengine wakiendelea kushambulia.

westgate escape route-2
Hapa ndipo inapotokea njia hiyo ya maji taka kutoka Westgate hadi katikati ya jiji la Nairobi

Taarifa hiyo inaendelea kudai kuwa wana usalama wanadai kuwa magaidi wa Al-shabaab walisafiri umbali wa nusu maili kwa magoti katika njia hiyo ya chini ya ardhi katika njia ya maji taka.

Chanzo kimoja kilisema “They escaped like sewer rats. The terrorists would have been able to pass through the underground tunnels at a rapid pace and surface almost unnoticed”.

Taarifa hiyo inaendelea kusema kuwa wachunguzi wa Kenya hawakuigundua njia hiyo ya kutorokea mpaka masaa 72 kupita baada ya shambulio kutokea.

Unaweza kuisoma taarifa hiyo kwa undani hapa

Source: Mirror

KWA SABABU YA WOGA WA WAKAZI WAKE KUSILIMU, MEYA AGOMA KUTOA KIBALI CHA UJENZI WA MSIKITI

Meya wa mji wa Moscow Sergey Sobyanin  amesema mji wake hauna mpango wa kuruhusu tena ujenzi wa msikiti mpya kwani kwa kufanya hivyo kuna madhara kwa wakazi wenye asili na mji huo, aliyasema hayo wakati akihojiwa na kituo cha redio cha echo Moscow.

Alisema Wengi wa waislamu wa mji wa Moscow ni wahamiaji waliokuja kufanya kazi. Na kwamba kuna asilimia 10 tu wakazi waislamu hivyo haoni kama kuna haja ya Kuruhusu ujenzi wa msikiti mwingine mpya.

Aidha anakasirishwa na watu hao wanaozungumza lugha tofauti, tabia tofauti pamoja na tabia ya 'fujo', kuanza kuigwa na wakazi wenye asili ya mji huo na uingiaji wa kasi katika dini ya kiislamu kwa wakazi wa Moscow kuna madhara kwa baadae.

Alisema kuna wafanyakazi wahamiaji 200,000 na asilimia 35 kati yao ndio wenye ujuzi. Meya huyo alisema ni muhimu kupunguza sehemu ya wafanyakazi wasio na ujuzi.

Kulingana baadhi ya makadirio ya Moscow kuna mhamiaji mmoja haramu katika wahamiaji 10 waliosajiliwa. Hii inafanya idadi ya wafanyakazi wa kigeni waliosajiliwa katika mji huo kufikia milioni mbili. Mwaka 2012 mamlaka ya Moscow iliwafukuza wageni 16,000 kwa kosa la kufanya kazi kinyume cha sheria.

Hata hivyo Kauli ya Meya huyo imepingwa vikali na waislamu wa nchini urusi kwa kusema mahitaji ya ujenzi wa msikiti ni makubwa kulingana na wingi wa waislamu nchini humo ambapo inawalazimu kusali Barabarani.

Makamu mwenyekiti wa baraza la Mufti wa Russia Nafigulla Ashirov alisema waislamu hawakubaliani na meya huyo na kwamba wanapeleka maombi yao kwa Rais Vladimir Putin kwa msaada zaidi. Russia ni mojawapo ya nchi zinazokabiliwa na wimbi kubwa la ukuaji wa dini ya kiislamu.

OPERESHENI KIMBUNGA YAFUMUA KIJIJI HARAMU CHENYE DOLA YAO.

Imeandikwa tarehe 29 Septemba 2013 By Eric Anthony, Kigoma

KAMPENI ya kitaifa ya kuondoa wahamiaji haramu nchini iliyopewa jina la Operesheni Kimbunga, imefanikiwa kusambaratisha kijiji cha wahamiaji haramu wa Burundi waliokuwa wamejitengenezea dola yao nchini, kiasi cha
hata kutumia sarafu ya Burundi ilihali wakiwa Tanzania.


Aidha, watoto wao wanasoma shule kwa mitaala ya Burundi, ikiwa ni pamoja na kuwafundisha kwa lugha ya Kifaransa wakiwa kijijini Nyamugali, Mvugwe wilayani Kasulu, Kigoma.

Hayo yamethibitishwa na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa, Issa Machibya katika mahojiano maalumu na gazeti hili ofisini kwake mjini hapa.


Kutokana na hatua hiyo, baadhi ya wakazi wa mkoani Kigoma, wakiwemo wa Manispaa ya Kigoma Ujiji na wilaya za Kasulu na Buhigwe, wamepongeza hatua hiyo.

Wameitaka serikali kutorudi nyuma katika kuhakikisha inawaondoa nchini wahamiaji haramu ambao wametajwa kuwa tishio kwa usalama wa nchi kutokana na kujihusisha na matukio ya ujangili, biashara ya silaha zikiwemo za kivita, na matukio mengine.


Akizungumza mjini hapa, Machibya alisema mbali ya kutumia faranga (fedha za Burundi) kwa matumizi yao ya kawaida wakiwa nchini na kufundisha kwa mitaala ya nchi waliyotoka, wahamiaji hao walipeperusha pia bendera ya nchi yao katika sehemu mbalimbali za kijiji hicho.
“Lakini kwa sasa, wote wamekimbia na kuziacha nyumba zao. Huwezi kuamini kama ni nyumba za wahamiaji haramu, kwani walijijenga na kuishi watakavyo, tena bila ya hofu katika nchi ya kigeni.


“Hebu tafakari, ni dharau gani unaishi Tanzania, lakini hata pesa yao hutumii, badala yake unatumia faranga.Tunashukuru tumewasambaratisha, na tutaendelea na operesheni hii mpaka tuhakikishe Watanzania
wanaishi kwa amani katika ardhi yao,” alisema Machibya.


Inakadiriwa kuwa, idadi ya wahamiaji haramu waliokuwa wanaishi kijijini hapo, lakini sasa wakiwa wamekimbia mkono mrefu wa Operesheni Kimbunga, ni zaidi ya 600.


Mkoa wa Kigoma pekee umenasa wahamiaji haramu 4,365 wa Burundi katika awamu ya kwanza ya operesheni hiyo iliyosambaa katika mikoa mbalimbali nchini, lakini Machibya amewataka Wana-Kigoma kushiriki kikamilifu
katika vita dhidi ya wahamiaji haramu hasa katika awamu hii ya pili na nyinginezo.


“Tatizo lililopo ni usiri. Wengi wameshindwa kutoa ushirikiano, na kufanya wengi tuishi nao kana kwamba ni Watanzania wenzetu… Watanzania waelewe hawa si watu wema, wangekuwa wema wangefuata taratibu za kuishi nchini, lakini wamekuwa wakiishi kwa ujanja ujanja mno. Mshona nguo za RC “Miongoni mwao ndimo walimo mawakala wa silaha za kivita, mabomu ya kurusha kwa mkono na biashara nyingine haramu.


Hatuwezi kukubaliana na hali hii,” alisema Machibya na kutoa mfano unaoendelea kumshangaza hata yeye mwenyewe kuwa, fundi maarufu aliyekuwa anashona nguo za baadhi ya Wakuu wa Mkoa wa Kigoma, akiwemo
yeye mwenyewe na mtangulizi wake, John Simbakalia ni mtuhumiwa wa uhamiaji haramu.


“Ndiyo, hata kabla yangu ndiye aliyekuwa anashona nguo za baadhi ya ma-RC (Wakuu wa Mkoa) hapa Kigoma, Simbakalia ni miongoni mwao na mimi mwenyewe amenishonea suti mbili…nikanogewa na kutaka kushona suti
nyingine, sasa nikiwa na kitambaa changu, kila nikipita nakuta ofisi zimefungwa, zaidi ya mara nne nimepita... kuuliza naambiwa ni wale wale, wameamua kujisalimisha kabla ya kunaswa.


“Sasa mambo haya yanatokea hapa mjini, si huyo tu, kuna wengi wanaendelea kusombwa…lakini kama Serikali ya mkoa, tunasema wawe hapa mjini au mahali popote pale, operesheni hii itawanasa na tunamshukuru Rais Jakaya Kikwete kwa kuunga mkono,” alisema.


Akizungumzia hatua hiyo, Mkuu wa Kambi ya Wakimbizi ya Nyarugusu, wilayani Kasulu, Frederick Nisajile, alipongeza kazi nzuri inayofanywa na serikali, huku akishauri mianya mingine ya kuzalisha wahamiaji haramu au hata kugawa uraia kiholela kwa wakimbizi ifungwe kwa sababu za kiusalama.


“Kwa idadi hii ya wahamiaji na wakimbizi, usalama wa nchi uko hatarini. Kuna mengi ya kufanyiwa kazi ili kuhakikisha nchi haiingiliwi,” alisema Nisajile ambaye amefanya kazi na wakimbizi kwa takribani miongo miwili.
Mkazi mwingine wa mjini Kigoma, eneo la Burega ambaye hata hivyo hakuwa tayari kutajwa jina, alisema,” Kigoma imevamiwa.


Mbaya zaidi watu wanafichiana siri, lakini wahamiaji ni wengi, wakiwemo wafanyabiashara wakubwa. Nao wanaita ndugu zao na kuzidi kuijaza nchi yetu, wakiishi bila kufuata taratibu.


Naipongeza serikali kwa kuanza kukabiliana na wimbi hili la wahamiaji haramu.” Naye Kiongozi wa Timu ya Habari na Mawasiliano ya Operesheni Kimbunga, Zamaradi Kawawa, akizungumza kwa njia ya simu kutoka
Biharamulo, Kagera alisema anafarijika kuona operesheni inang’ata kila sehemu, huku akiahidi kutoa taarifa ya utekelezaji wa awamu ya pili ya operesheni inayoendelea kote nchini.


Operesheni Kimbunga ilianzishwa kwa lengo la kukabiliana na vitendo vya uhalifu vilivyokithiri vikiwemo ujambazi wa kutumia silaha, ujangili, utekaji wa magari na mauaji ya kikatili pamoja na migogoro ya ardhi inayotokana na wafugaji kutoka nchi jirani kuingiza mifugo yao kwa ajili ya malisho.


Ni utekelezaji wa agizo la Rais Jakaya Kikwete alilolitoa Julai 29, 2013 akiwa katika ziara ya kikazi mkoani Kagera, akitaka kufanyika kwa operesheni maalumu ya kuondoa uhalifu katika mikoa ya Kagera, Kigoma na
Geita ambao kwa kiasi kikubwa umechangiwa na kuwepo kwa wahamiaji haramu kutoka nchi jirani.


Operesheni Kimbunga inayoongozwa na Brigedia Jenerali Mathew Sukambi ilianza Septemba 6, 2013, baada ya kupita wiki mbili alizokuwa amezitoa Rais Kikwete kwa kuwataka wahamiaji wanaoishi nchini bila kufuata sheria kuondoka kwa hiari yao au kuhalalisha ukazi wao nchini.

MWANAMKE AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MIAKA MITANO JELA BAADA YA KUMTUPA MTOTO WAKE CHOONI


                   Mwanamke mmoja mkazi wa Manga A Jijini Mbeya amehukumiwa kifungo cha miaka 5 jela kwa kosa la kutupa mtoto wake chooni. Mwaka huu katika eneo hilo baada ya watoto waliokuwa wakicheza kugundua kuwepo kwa Mtoto katika choo cha shimo.



 

Mtuhumiwa baada ya kukamatwa amekiri kutenda kosa hilo na kwamba alifanya hivyo baada ya mzazi mwenzie kumkataa.

Ameongeza kuwa amelazimika kutupa katika choo cha jirani kwa sababu ni cha shimo tofauti na chao ambacho asingeweza kutupa mtoto huyo.

  

Rukia Haruna (31)  akitolewa nje  na Askari wa Jeshi la Polisi akitolewa nje ya  Mahakama kwenda Gerezani kutumikia kifungo cha miaka 5 Jela  

Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Archiles Mulisa mbele ya Hakimu wa Mahakama ya Wilaya ya Mbeya, Zabibu Mpangula, amemtaja Mtuhumiwa kuwa ni Rukia Haruna (31) mkazi wa Manga A Jijini Mbeya na kwamba kosa lake ni kinyume cha kifungu  218 kifungu kidogo cha 35 sura ya 16 ya mwaka 2002.

Sunday, September 29, 2013

Utanuzi wa Kina cha Maji Bandari ya Sea Link Malindi zanzibar


Kampuni ya Azam Marine ikifanya utanuzi wa bandari inayotumia meli yake ya Mv Sea Link ili kuongeza kima cha maji ya bahari katika eneo hilo lilinalotumika na meli yake kwa kupakilia abiri na mizigo katika banmdari hiyo.Kima cha maji katika eneo hilo huwa ndogo wakati wa maji kutoka na kusababashi usumbufu kwa wakati huo.

Maalim Seif: Katiba bora hutokana na mawazo ya wananchi


Baadhi ya Wazanzibari wanaoishi Tanga wakimsikiliza Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad katika ukumbi wa Tangamano jijini Tanga, leo tarehe 27/09/2013. 




Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, akizungumza na Wazanzibari wanaoishi Tanga, katika ukumbi wa Tangamano jijini Tanga.
(picha na Salmin Said, OMKR)
 Na Hassan Hamad, OMKR
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, amesema katiba bora ni ile inayotokana na mawazo ya wananchi, na sio inayotengenezwa na kikundi cha watu au chama cha siasa.
Maalim Seif ametoa kauli hiyo Mkoani Tanga, wakati akizungumza na Wazanzibari wanaoishi Tanga, ikiwa ni mfululizo wa ziara zake za kuzungumza na Wazanzibari wanaoishi nje ya Zanzibar.
Amesema ili katiba iweze kuwa ya wananchi, haina budi ipitishwe na zaidi ya theluthi mbili ya wananchi, vyenginevyo itafuata matashi ya vyama vya siasa au kikundi kinachojali maslahi yake binafsi.
Maalim Seif ametoa ufafanuzi huo baada ya kuwepo madai ya marekebisho ya sheria ya mabadiliko ya katiba yanayolenga kuidhinisha katiba kwa ushindi mdogo wa kura (simple majority).
Ametoa changamoto kuwa duniani kote hakuna katiba iliyopitishwa kwa ushindi mdogo wa kura, na kwamba haitokuwa busara kwa Tanzania kupitisha katiba kwa mfumo huo.
Mapema akizungumza katika mkutano huo, Mwakilishi wa Jimbo la Ole, Mhe. Hamad Massoud Hamad, ametoa wito kwa Wazanzibari wanaoishi Tanga ambao wametimiza masharti ya kujiandikisha, kwenda kujisajili katika daftari la kudumu la wapiga kura wakati utakapofika.
Sambamba na hilo amewatanabahisha Wazanzibari hao kufanya juhudi za kutafuta vijambulisho vya Uzanzibari Mkaazi kutokana na umuhimu waka katika maisha ya kila siku ya Wazanzibari.
Amesema iwapo Mzanzibari atakosa kitambulisho hicho, anaweza kupoteza fursa nyingi zikiwemo utambulisho wake kama Mzanzibari, masomo, hati ya kusafiria na biashara.
Hassan Hamad (OMKR)

Mlipuko waua watu 6 huko Tumbuktu Mali


Mlipuko waua watu 6 huko Tumbuktu Mali
Watu 6 wameuawa wakiwemo raia wawili na wengine kadhaa kujeruhiwa kufuatia mlipuko uliotokea karibu na kambi ya jeshi katika mji wa kihistoria wa Timbuktu nchini Mali. Afisa wa serikali katika eneo hilo ameeleza kuwa, mlipuko huo wa kutegwa garini umesababisha pia nyumba kadhaa kuporomoka na kutokea hasara kubwa.
Serikali ya Mali imelaani shambulio hilo lililotokea ikiwa zimepita siku chache tu tangu waasi wa Tuareg wanaopigana ili kulitenga eneo la Kaskazini wasimamishe mazungumzo na serikali, wakiituhumu kwamba imeshindwa kuheshimu makubaliano ya amani yaliyofikiwa kati ya pande mbili. Mwezi Juni viongozi wa kundi la Tuareg walifikia makubaliano na serikali ya mpito ya Mali yaliyopelekea kurejea jeshi kwenye mji wa Kidal na kufanyika uchaguzi wa rais.

Viongozi wa Iraq walaani mashambulizi ya Arbil


Viongozi wa Iraq walaani mashambulizi ya Arbil
Ofisi ya Waziri Mkuu wa Iraq imelaani miripuko ya mabomu iliyotokea leo katika mji wa Arbil wa kaskazini mwa nchi hiyo.
Ali al Musawi, Mshauri wa Masuala ya Habari wa Waziri Mkuu wa Iraq, Noor al Maliki, amesema leo jioni kuwa, serikali ya nchi hiyo inalaani vikali miripuko iliyotokea kwenye mji wa Arbil huko Kurdistan Iraq na kupelekea watu 6 kuuawa na wengine 38 kujeruhiwa.
Al Musawi aidha ameashiria namna mgogoro wa Syria unavyohatarisha pia usalama wa nchi jirani hasa Iraq na kusema kuwa, miripuko hiyo ya mabomu ina uhusiano na matukio ya Syria.
Leo Jumapili kumetokea miripuko mitano ya mabomu mbele ya ofisi ya usalama ya mjini Arbil, kaskazini mwa Iraq, sambamba na kutangazwa ushindi wa chama cha Democrat cha Kurdistan ya Iraq kinachoongozwa na Masoud Barzani.

Mamlaka ya Ndani Palestina haitaki Intifadha


Mamlaka ya Ndani Palestina haitaki Intifadha
Idara za usalama za Mamlaka ya Ndani ya Palestina zimetangaza kuwa zinafanya kila linalowezekana ili kuzuia kuanza Intifadha ya Tatu huko katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan. Idara za usalama za Mamlaka ya Ndani ya Palestina zimedai kuwa kuanza Intifadha ya Tatu ya Wapalestina kutazusha hali ya hofu na wasiwasi katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na kwamba idara hizo zitafanya kila ziwezalo ili kuzuia kutokea intifadha hiyo. Mji wa Quds unaokaliwa kwa mabavu na Wazayuni pamoja na msikiti mtukufu wa al Aqswa ambao ni kibla cha kwanza cha Waislamu, Ijumaa iliyopita  ilishuhudia wanajeshi wa utawala wa Kizayuni wakijenga vituo mbalimbali vya upekuzi sambamba na kujiri mapigano makali kati ya raia wa Kipalestina na wanajeshi wa Israel. Matukio hayo yalijiri baada ya harakati ya muqawama ya Palestina Hamas kutoa mwito kwa makundi mbalimbali ya wananchi wa Palestina huko katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na katika mji wa Quds wa kuunga mkono Intifadha ya Tatu ili kukabiliana na utawala wa Kizayuni. 

Boko Haram yauwa makumi ya wanachuo Nigeria


Boko Haram yauwa makumi ya wanachuo Nigeria
Wanamgambo wa Boko Haram wa huko Nigeria leo asubuhi wamekishambulia chuo cha kilimo cha Yobe cha kaskazini mashariki mwa nchi hiyo na kuwauwa kwa risasi zaidi ya wanachuo 50 waliokuwa wamelala chuoni hapo.
Kundi la wanamgambo wa Boko Haram katika wiki za hivi karibuni limekuwa likiwashambulia ovyo raia wa Nigeria katika kulipiza kisasi oparesheni za mashambulizi yaliyoanzishwa na jeshi la nchi hiyo dhidi yake.
Hadi kufikia sasa miili zaidi ya 50 ya wanachuo waliouliwa na Boko Haram ambao wengi wao ni wavulana tayari imehifadhiwa katika hospitali kuu ya jimbo la Yobe.
Mbali na kuwalenga raia, wanamgambo wa Boko Haram katika miezi ya hivi karibuni wamekuwa wakizishambulia shule kadhaa likiwemo shambulio walilolifanya kwenye shule moja huko Potiskum eneo lililoko umbali wa maili zisizopungua 30 kutoka eneo palipojiri shambulio la leo na kuua  wanafunzi 27 na mwalimu mmoja.

YABAINIKA!!! VIJANA WA AL SHABAAB WALITOROKA KUPITIA MTARO UNAOPITISHA MAJI MACHAFU,NA WANAJESHI WA KENYA HAWAKUUA GAIDI HATA MMOJA

Friday September 27, 2013 - As Kenya and foreign detectives continue to comb the Westgate debris in search of missing bodies and answers to the Westgate terror attack, shocking revelations have emerged that may catch Kenyans unaware following the 4-day horror they went through.
This is after detectives discovered a huge underground tunnel, also used as sewerage tunnel, which runs several metres from the Westgate Mall to the neighboring Nakummatt Ukay Mall.
The detectives noted that the Al-Shabaab terrorists are likely to have escaped through the tunnel, and left their explosives in the Westgate Mall, whose explosions have continued to be heard even after the Kenya Defence Forces secured the Westgate Building.
According to impeccable sources from the intelligence community, KDF did not kill any Westgate terrorist after all, because there is no sign of any of them in the debris even after combing the rubble for days now.
This comes as KDF through Interior Cabinet Secretary, Joseph Ole Lenku, insist they killed five terrorists, but have since failed to prove their assertion.

Source of the News :  credit Thechoice

Friday, September 27, 2013

AJALI MBAYA YAUA MTU MMOJA NA MAJERUHI WANNE - TABORA


Mwili wa kijana mmoja aliyefahamika kwa jina la Rashidi Seleman mkazi wa Isevya manispaa ya Tabora ambaye amepoteza maisha baada ya Lori walilokuwa wamepanda kuanguka eneo la Inala barabara ya kwenda Kigwa,Polisi wamesema chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi wa dereva ambaye amekimbia huku watu wengine wanne wakiwa wamejeruhiwa vibaya ambao wamelazwa katika hospitali ya Rufaa ya Kitete.
Tatizo la ukosefu la ukosefu wa vifaa vya kuokolea vilisababisha maiti ya mtu huyo kukaa muda mrefu akiwa amebanwa na Lori hilo ambalo ni mali ya kampuni ya mkandarasi JOSSAM
Awali jitihada za Polisi na wananchi ziligonga mwamba na kubaki wakiiangalia maiti hiyo pasipo msaada wowote ajali ambayo imetokea majira ya saa kumi jioni hapo jana.
Askari wa usalama barabarani wakiongozwa na kamanda wa Polisi kikosi cha usalama barabarani wilaya ya Tabora Bw.Swaleh Digega hatimaye wakafanikiwa kuutoa mwili wa marehemu huyo na kuupeleka hospitali ya mkoa wa Tabora Kitete kwa ajili ya kuuhifadhi....Hata hivyo Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Sumatra wanakusudia kumfikisha mahakamani mmiliki wa Lori hilo kwa kitendo cha kusafirisha mizigo na wanadamu katika gari hilo lenye nambari za usajili T 702 ACR ambalo ni ISUZU TX

MAJANGA!!! KANISA LALIPULIWA NA KUUA WAKRISTO 75 NA KUJERUHI 110...


Wauaji wawili wa kujitoa mhanga wamelipua mabomu yao nje ya kanisa la kihistoria nchini Pakistan jana na kuua watu 75 kwenye shambulio baya zaidi kuwahi kutokea kwa Wakristo walio wachache wa nchini humo.

 Taliban wa Pakistan wamekiri kuhusika na shambulio hilo lililotokea katika mji wa Peshawar, wakisema wataendelea kuwalenga wasio Waislamu hadi hapo Marekani itakapositisha mashambulizi katika mji huo wa kikabila nchini humo. 


Shambulio la hivi karibuni lilifanyika Jumapili pale makombora yalipopiga majengo mawili katika eneo la North Waziristan, na kuua watu sita wanaodhaniwa kuwa wanamgambo, maofisa wa intelijensia Pakistan walisema.
Shambulio kwenye Kanisa la All Saints, ambalo pia lilijeruhi watu 110, linatekeleza kitisho kilichotolewa na Taliban wa Pakistan wakati huku serikali ikitaka mpango wa amani na wanamgambo hao.
Shambulio hilo limetokea wakati mamia ya waumini wakiwa wanatoka nje ya kanisa hilo lililoko katika wilaya ya Kohati Gate mjini humo baada ya huduma ya kupata chakula cha bure aina ya wali.
"Kulikuwa na milipuko na kulikuwa na mateso kwetu sote," alisema Nazir John, ambaye alikuwa kanisani pamoja na takribani waumini wengine 400.
"Niliporejewa na fahamu zangu, sikuona chochote ila moshi, vumbi, damu na watu waliokuwa wakilia kwa uchungu. Niliona sehemu za miili zilizosambaratika na damu kuzunguka eneo lote."
Manusura walikumbatiana kila mmoja baada ya milipuko huko. 
Ukuta mweupe wa kanisa hilo, ambalo lilifunguliwa kwa mara ya kwanza mwishoni mwa miaka ya 1800, ulitapakaa mashimo yaliyochimbwa na vipande vya vyuma vilivyotoka katika mabomu ma kusababisha uharibifu mkubwa.
Damu ilitapakaa sakafuni na kusambaa kwenye ukutani. Sahani zenye wali zilitawanyika kila pembe za eneo hilo.
Shambulio hilo lilifanywa na watuhumiwa wawili wa kujitoa mhanga ambao walilipua mabomu yao kwa kupokezana. Mamlaka zimekuta sehemu za mwili na zilikuwa zikijaribu kutambua umri wao.
Milipuko hiyo imeua watu 75 na kujeruhi wengine 110. Waliokufa ni pamoja na wanawake na watoto.
Idadi ya majeruhi ni kubwa mno kiasi cha hospitali hiyo kuishiwa majeneza kwa ajili ya waliokufa na vitanda kwa ajili ya majeruhi, alisema Mian Iftikhar Hussain, waziri wa zamani wa habari wa jimbo la Khyber Pakhtunkhwa ambaye alikuwa katika eneo la tukio.
"Hili ni shambulio baya zaidi dhidi ya Wakristo katika nchi yetu," alisema Irfan Jamil, askofu wa mji wa mashariki wa Lahore.
Mmoja wa waliojeruhiwa, John Tariq, ambaye amepoteza baba yake katika shambulio hilo, aliwauliza washambulizi hao, "Tumewakosea nini watu hawa? Kwanini tumekuwa tukiuawa?"
Ahmad Marwat, ambaye alijitambulisha kama msemaji wa tawi la Jundullah la Taliban wa Pakistan, alidai kuhusika na shambulio hilo.
"Wote wasio Waislamu nchini Pakistan ni walengwa wetu na wataendelea kuwa hivyo kwa wakati wote Marekani inaposhindwa kusitisha mashambulizi katika nchini yetu," alisema Marwart kwa njia ya simu kutoka sehemu isiyojulikana.
Askofu wa Peshawar, Sarfarz Hemphray, ametangaza siku tatu za maombolezo kufuatia shambulio hilo na kuishutumu serikali na vyombo vya ulinzi kwa kushindwa kuwalinda Wakristo wa nchini humo.
"Endapo serikali itaonesha nia, inaweza kudhibiti ugaidi huu," alisema Hemphray. "Tumekuwa tukizitaka mamlaka kuimarisha ulinzi, lakini hazitilii maanani."
Waziri Mkuu wa Pakistani ameshutumu shambulio hilo katika taarifa iliyotumwa kwa waandishi wa habari, akisema, "Magaidi hawana dini na wanaolenga watu wasio na hatia ni kinyume cha mafundisho ya Kiislamu na dini zote."
"Matukio kama hayo ya kiwendawazimu ya ugaidi yanaakisi unyama na akili zisizo za kibinadamu za magaidi," alisema.

HIVI NDIO HALI YA JENGO LA WESTGATE BAADA LA SHAMBULIO LA AL-SHABAAB...!!


a2

Picha za nje ya jengo la Westgate hazioneshi uhalisia wa hali iliyoko ndani ya jengo baada ya shambulio la kigaidi Jumamosi iliyopita jijini Nairobi, Kenya na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 70.
a7
Picha hizi zinatoa picha halisi ya jinsi jengo hilo lilivyoharibika vibaya kwa ndani baada ya ghorofa tatu za jengo hilo kudondoka baada ya kupigwa mabomu katika mchakato wa kukabiliana na magaidi.
a6 Hivi ndivyo jengo la West gate linavyoonekana kwa nje

Picha hizi pia zinaonesha jinsi magari yaliokuwepo eneo la maegesho ya magari katika jengo hilo yakiwa yameharibiwa kiasi kwamba kuna mengine ambayo huenda hata wamiliki wanaweza kushindwa kuyatambua.
a1

a3
a4
a5
a8
a9 Picha: Nairobi Wire, Mail Online

Wataalamu watafuta miili Westgate

Jengo la Westgate ambalo ghorofa zake tatu ziliporomoka
Vikundi vya maafisa wa uchunguzi wa mauaji vinatafuta miili ya mateka waliouawa ndani ya jengo la Westgate ambao idadi yao haijulikani.
Mateka walizuiliwa na magaidi kwa siku nne kabla ya serikali kutangaza kumalizika rasmi kwa shambulizi hilo
Zaidi ya watu 65 waliuawa na mamia ya wengine kujeruhiwa.
Waziri wa usalama Joseph Ole Lenku amesema kuwa hatarajii kuwa idadi ya waliofariki itaongezeka na kusema kuwa miili ya magaidi pakee ndio itapatikana ndani ya vifusi.
Hii ni baada ya sehemu ya jengo hilo kuporomoka wakati shughuli za uokozi zilikuwa zinaendelea .
Lakini kwa mujibu wa shirika la Red Cross, watu 61 wangali hawajulikani waliko.
Wakati huohuo, Kenya inaendelea na siku tatu za maombolezi ya vifo vya raia na baadhi ya maafisa wa usalama waliofariki katika shambulizi hilo.
Mazishi ya mtangazaji mmoja wa Televisheni na Redio, Ruhila Adatia yalifanyika siku ya Alhamisi.
Bendera zingali zinapeperushwa nusu mlingoti kwa heshima ya wale waliofariki.
Walinzi walionekana wakichunguza abiria kabla ya kuabiri magari ya usafiri.
Huku wasiwasi ukiongezeka miongoni mwa wakenya kuhusu hali ya kujiandaa kwa maafisa wa usalama kuhusiana na mashambulizi kama haya, taarifa zinasema kuwa serikali inajiandaa kudurusu mikakati yake ya kupigana dhidi ya ugaidi na majanga mengine.
Kundi la kigaidi la Al Shabaab linasema limeshambuli Kenya kutokana na nchi hiyo kujihusisha na vita dhidi ya kundi hilo nchini Somalia

Kenya yamsaka Samantha Lewthwaite


Samantha anashukiwa kuwa na uhusiano na kundi la kigaidi la Al Shabaab
Polisi wa kimataifa Interpol, wamemuweka mwanamke aliyeshukiwa kuongoza mashabulizi ya kigaidi nchini Kenya raia Muingereza Samantha Lewthwaite, kwenye orodha ya watu wanaosakwa sana duniani.
Hatua hii ni kutokana na ombi la serikali ya Kenya kwa Interpol.

Bi Lewthwaite, mwenye umri wa miaka 29, ni mjane wa mlipuaji aliyefanya shambulizi la kujitoa mhanga mjini London Uingereza mwezi Julai mwaka 2005
Anajulikana kama "white widow", na amehusishwa na kundi la kigaidi la Al Shabaab nchini Somalia.
Polisi wa Interpol hata hivyo hawakuhusisha hatua ya kumsaka Samantha na shambulizi la kigaidi dhidi ya jumba la maduka la Westgate mjini Nairobi lililowaua watu 67.
Hata hivyo, hatua hii ya kumsaka Bi Lewthwaite inakuja punde baada ya shambulizi hili la kigaidi nchini Kenya.
Al-Shabab ilikiri kufanya mashambulizi hayo yaliyotokana na kutekwa kwa jengo la Westgate na kisha kutekwa kwa raia wa kawaida waliokuwa ndani ya jengo hilo kwa siku nne.
Kwa mujibu wa polisi wa Interpol, mwanamke huyo anasakwa na serikali ya Kenya kwa kumiliki mabomu na kupanga njama ya kufanya mashambulizi kuanzia Disemba mwaka 2011.
Ikiwa mwanamke huyo atakamatwa katika nchi mwanachama wa Interpol, atazuiliwa na kusibiri kupelekwa katika nchi anayotakikana kwa kesi kufunguliwa dhidi yake.
Bi Lewthwaite anajulikana kwa jina bandia la, "Natalie Webb" –na alikuwa anasakwa kwa madai ya kumiliki hati bandia ya usafiri nchini Afrika Kusini.
Ni mjane wa Germaine Lindsay, mmoja wa washambuliaji wanne waliohusika na shambulizi la kigaidi mjini London ambapo watu 52 waliuawa na mamia ya wengine kujeruhiwa.

SIMULIZI:MMOJA WA MAGAIDI WA AL SHABAAB ALIKUWA AKIONGEA KISWAHILI KIZURI KABISA

INGAWA duka la Westgate liko karibu dakika 15 tu kutoka nyumbani kwangu, nilikuwa nikienda kule kwa nadra kununua vitu. Mara kwa mara huwa kuna watu wengi katika duka hili katika siku za mwisho mwa wiki na hivyo niliona kama karaha. Jumamosi ilikuwa maalumu kwa sababu nilitaka kutumia muda wangu na mkwe yangu, Amina (si jina halisi) na baadhi ya marafiki zetu ambao watoto wao walikuwa wakishiriki katika shindano la upishi.

Tulikuwa juu ya ghorofa la mwisho saa 5.00 asubuhi. Shindano la upishi lilikuwa likiendelea. 

Baada ya muda, Amina aliamua kuelekea chini kwa ajili ya kununua vitafunwa. Sikuwa na njaa sana hivyo niliamua kubaki hapo hapo. Nilitaka kuangalia watoto wakipika.

Karibu saa saba na robo, Amina alikuwa hajarejea nilipokuwa, lakini sikuwa na hofu na nilibakia hapo hadi niliposikia sauti ya milio ya bunduki.

Nilishikwa na kihoro na kumpigia simu mwanangu. Ni ofisa usalama na nilidhani pengine angeweza kusaidia.

“Kuna milio ya risasi hapa. Naweza kusikia milio ya risasi. Tafadhari fanya unaloweza,” nilimwambia.

Niliongea naye kwa muda mfupi kwa simu kwa sababu nilitaka kuzungumza na mkwe wangu. Katika simu aliniambia kuwa alikuwa amejificha katika benki iliyo kwenye kituo hicho cha biashara. Alisisitiza kwamba yu salama na alitaka niwe mwangalifu.

Mazungumzo yetu yalihitimishwa ghafla nilipoona watu wawili wakija juu. Walikuwa na bunduki na haikunichukua muda nikaona mabomu ya kutupwa kwa mkono yakining’inia katika mikanda yao.

Nyuso zao hazikufichwa na tuliziona wazi kana kwamba walikuwa hawajali iwapo tungeweza kuwatambua baadaye. Mara moja nilianza kuwa na wasiwasi huenda nisitoke hai.

Katika kitambo hicho, hofu yangu ilikuwa kubwa. Magaidi walipoanza kurusha risasi na magurunedi holela, umati ukaangua kilio kwa kihoro. 

Watu walianza kukimbia kwa mshtuko huku mwelekeo wao ukiwa haueleweki. Nami nilikimbilia katika hema lililokuwa likitumika kama jiko la watoto na kujificha humo.

Awali nilidhani walikuwa wakifyatua risasi kwa bahati mbaya. Hata hivyo, punde nikaona kwamba wale watu waliokuwa wakikimbia huko na huko wakipiga kelele ni wale waliokuwa wamepigwa risasi. Huku kukiwa na makelele, niliwasikia magaidi wakiwaita Waislamu:

“Kama ninyi ni Waislamu, mnaweza kunyanyuka na kuondoka,” walisema.

Lakini haikuwa rahisi kama ilivyodhaniwa. Waislamu walitakiwa kuthibitisha imani yao. Walitakiwa kutaja jambo fulani kutoka aya za Korani kabla ya kuachiwa. Na hata baada ya hapo bado unaweza kupoteza maisha yako. Mwanamke mmoja ambaye alisema alikuwa Muislamu lakini hakuonekana kuwa Muislamu alipigwa risasi na kufa.

Sina uhakika kwa nini sikutumia dini yangu ili kujiokoa mapema. Pengine ilitokana na hofu. Pengine ilitokana na hali ya ukaidi.

Nikiwa nimejificha nyuma ya maboksi na meza katika hema, watu nisiowajua wakawa wa karibu nami kuliko marafiki. Magaidi lazima walijua tulipo; kulikuwa na maeneo mengi ambayo tungeweza kuyatumia kujificha.

Hata hivyo, tulitulizana wenyewe kwa wenyewe huku tukiwataka watoto wanyamaze kwa sababu sauti zingeweza kutufichua pale tulipo. 

Lakini pamoja na juhudi zetu zote za kuwatuliza wanyamaze, bado baadhi ya watoto hawa hasa wale wadogo walilia.

Tuliomba. Tuliwasilisha maombi yetu kimyakimya kwa Muumba wetu, pengine tukiona hiyo ni siku yetu ya mwisho kuwa hapa duniani.

Tulikuwa tumejificha kwa dakika 20 wakati nilipomsikia mmoja wa magaidi akipokea simu kupitia simu yake ya mkononi. Hakuzungumza kwa sauti kubwa, lakini ilikuwa sauti tulivu ya Kiswahili iliyosikika vema masikioni.

Maneno halisi ilikuwa vigumu kuyakumbuka. Lakini alisema kuwa ameua watu wengi na wengine zaidi walijeruhiwa.

Dakika chache baadaye baada ya kupokea simu, magaidi walirusha risasi ovyo juu ya paa na kuondoka. Nikadhani kwamba milio hiyo ya mwisho ililenga kutuogopesha na kutuonya tusijaribu kuondoka mahali tulipo.

Tuliokolewa muda mfupi baadaye na wakati nikitembea kutoka katia jengo hilo tuliona miili ikiwa imezagaa sakafuni, nilijisikia nisiye na msaada kwamba sikuweza kufanya lolote kuzuia hali hii. 

Nilikuwa huru lakini mkwe wangu alikuwa bado amenasa katika jengo. Nilipompigia simu alinihakikishia kuwa yu salama tena kwa sauti tulivu. Alinitaka nisiwe na wasiwasi, ombi ambalo halikuwezekana kwangu.

Amina aliokolewa saa 12 jioni. Saa kadhaa nikiwa nyumbani kwa mwanangu na kwa rafiki yangu kusubiri neno la matumaini kutoka kwake ilikuwa tete hakika.

Nilifarijika sana wakati alipompigia simu mwanangu akimtaka aende kumchukua kutoka Visa Oshwal.

Saa zaidi ya 24 baada ya ile iliyokuwa siku njema nikiwa na mkwe wangu iligeuka kuwa jinamizi, na bado ninatetemeka nikiikumbuka. Hata hivyo, nina furaha kuwa hai na ninashukuru Amina na mimi tulitoka Westgate bila majeraha.

*Hii ni simulizi ya mmoja wa watu waliookoka katika tukio la ugaidi la Westgate

POLISI WAMZOA BWANA NA BI HARUSI WAKATI WAKIFUNGA NDOA NA DIFENDA

Binti wa miaka 14, Zubeda akiwa tayari kufunga ndoa na Hamis (35).

NDOA iliyokuwa tayari kufungwa na shehe kati ya Hamis Ngaumba (35), mkazi wa Bangulo, Ulongoni, Gongo la Mboto, Dar na binti wa miaka 14 anayetajwa kwa jina moja la Zubeda, imesambaratishwa na polisi wa Kituo cha Polisi cha Sitaki-Shari, Dar kutokana na umri wa bi harusi kuwa mdogo, Amani limeidaka hiyo.
Hamis Ngaumba (35) aliyetaka kumuoa binti wa miaka 14.
Kizaazaa hicho cha aina yake kilichovuta hisia za wengi kilitokea saa 10:00 jioni, Jumapili iliyopita ambapo Shehe Bakari Mgesa wa Msikiti wa Bangulo alikuwa ameanza kutoa mawaidha ya maandalizi ya kufungisha ndoa hiyo lakini ghafla polisi na mapaparazi waliingia na shughuli kuishia hapo.
ISHU ILIKUWA HIVI
Mapema siku ya tukio, msamaria mwema ambaye hakupendezwa na kitendo hicho alitoa taarifa kwa mapaparazi ambao nao waliwataarifu polisi wa Kituo cha Polisi Sitaki-Shari na kupewa maafande kutoka dawati linaloshughulikia unyanyasaji wa kijinsia na kuambatana nao hadi eneo la tukio.
BREKI YA KWANZA KWA MJUMBE
Kabla ya kufika eneo la tukio, breki ya kwanza ilikuwa ni kwa mjumbe wa eneo hilo Shina Namba 10, Erasto Nyakiege ambaye alikiri kusikia taarifa hizo za mtoto kufungishwa ndoa lakini alizipata muda mfupi kabla polisi na waandishi hao kufika eneo hilo.
MJUMBE AUNGANA NA POLISI, MAPAPARAZI
Mapaparazi, polisi na mjumbe huyo waliambatana hadi kwenye nyumba ambayo ilikuwa na shamrashamra za ndoa hiyo na kumkuta shehe akijiandaa kufungisha huku waalikwa wakiwa wameshakaa mkao wa kula ‘mnuso’ (pilau).
MSHTUKO WATOKEA, WATU WAKIMBIA
Mshtuko mkubwa ulitokea eneo la sherehe baada ya watu kuwaona askari, wengine walikimbia kama wanafukuzwa na simba. Bi harusi yeye alikimbilia chumbani huku bwana harusi akijichanganya katikati ya wageni waalikwa lakini polisi walimweka ‘mtukati’.
SHEHE AWA WA KWANZA KUSIMULIA
Akizungumza baada ya kunaswa, Shehe Bakari alisema ndiyo kwanza alikuwa anajiandaa kwa zoezi la kuwafungisha ndoa wawili hao lakini kama angebaini kuwa mtoto huyo ana miaka isiyokidhi vigezo, asingekubali kwa vile hata dini ya Kiislamu hairuhusu mtoto kuolewa mpaka atimize miaka 18 na kuendelea.
BI HARUSI AWA WA PILI KUWEKA BAYANA
Naye bi harusi, Zubeda ambaye anaishi na bibi yake aitwaye Bibi Abuu, alieleza kuwa ndoa hiyo ilikuwa ni kama utani kwani mwanamme huyo alikuwa akimtania tangu akiwa mdogo akimwambia kuwa akikua atamuoa, hivyo akawa anamuita mchumba lakini hakuwahi hata siku moja kumtongoza.
MAHARI ILIVYOPELEKWA
Zubeda alisema cha kushangaza siku moja aliwaona wazazi wa kijana huyo wakipeleka barua ya posa na mahari na kumkabidhi mjomba na bibi yake kwani baba yake mzazi anaishi Shinyanga na mama anaishi Tabora, tangu akiwa mdogo anaishi na bibi yake huyo.
“Mimi natamani sana kusoma lakini sina uwezo kwani niliishia darasa la tatu baada ya wazazi wangu kushindwa kunisomesha ndipo bibi akaja kunichukua ndiyo maana suala la kuolewa limenitokea tu bila mwenyewe kupenda. Ilikuwa kama utani lakini wakapokea mahari,” alisema Zubeda huku akilia kwa uchungu.
BIBI AZUNGUMZA HUKU AKIWA AMELEWA TILALILA
Bibi Abuu alipoona mambo yameharibika huku akiwa  tilalila alikimbilia ndani kulala ambapo babu wa kufikia wa Zubeda, James alisema ni kweli mjukuu huyo ana miaka 14 na kuongeza kwamba waliopokea mahari ya mtoto huyo kiasi cha shilingi laki tano na nusu (550,000) ni wajomba pamoja na Bibi Abuu lakini yeye hajui chochote kuhusiana na ndoa hiyo.
KIUMENI WADAI MAHARI
Baada ya sekeseke hilo, ndugu wa upande wa mwanamme walikuja juu na kudai mahari yao huku wakitishia kwamba kama hawatarudishiwa basi wakwe hao watapelekwa polisi kwani hata wao hawakujua kama huyo anayeolewa ni mtoto wa miaka 14.
WAPELEKWA POLISI
Hata hivyo, polisi waliwazoa ndani ya difenda bwana harusi, bi harusi na wajomba wawili ambao ndiyo waliopokea mahari na kwenda kuwaweka nyuma ya nondo kusubiri taratibu za kisheria.

Tuesday, September 24, 2013

Asasi za Kiislamu zaitaka Nigeria kuchunguza mauaji

Asasi za Kiislamu zaitaka Nigeria kuchunguza mauaji

Taasisi za Kiislamu na za kutetea haki za binadamu nchini Nigeria zimeitaka serikali ya Abuja kufanya uchunguzi kuhusiana na mauaji ya makumi ya watu wanaoshukiwa kuwa wanachama wa kundi la Boko Haram. Jumuiya hizo zimeashiria mauaji ya hivi karibuni ya makumi ya watu mjini Abuja wanaoshukiwa kuwa wanachama wa Boko Haram na kusisitiza kwamba, kuna utata katika tukio hilo hivyo kuna haja ya kufanyika uchunguzi wa kina kuhusiana na mauaji hayo. Taasisi za Kiislamu na za kutetea haki za binadamu nchini Nigeria zimetangaza kuwa, kuna udharura wa kufanyika uchunguzi kuhusiana na mauaji hayo. Wakati huo huo, Taasisi ya Kitaifa ya Haki za Binadamu nchini Nigeria imetangaza kuwa, uchunguzi kuhusiana na mauaji hayo tayari umeshaanza. Kundi la Boko Haram linahusishwa na mashambulio mengi ya kigaidi nchini Nigeria. Boko Haram ni kundi lenye misimamo ya kufurutu mipaka nchini Nigeria ambalo kutokana na kuwa na ufahamu mbaya na potofu kuhusiana na Uislamu, limeitumbukiza nchi hiyo katika dimbwi la machafuko na mauaji sambamba na kuzusha hitilafu za kidini na kikabila nchini humo

Kadhaa wakombolewa kwenye jengo la Westgate


Kadhaa wakombolewa kwenye jengo la WestgateKamanda wa Polisi wa Nairobi ametangaza kukombolewa idadi ya watu kadhaa waliokuwa wakishikiliwa mateka na wanamgambo wa al Shabab ndani ya jumba la kibiashara la Westgate lililoko kwenye mtaa wa Westland jijini Nairobi nchini Kenya. David Kimaiyo amesema kuwa, kikosi cha usalama cha Kenya kimefanikiwa kutekeleza operesheni hiyo ya kuwaokoa baadhi ya watu waliokuwa wakishikiliwa na wanamgambo wa al Shabab na kusisitiza kwamba operesheni hiyo ya uokozi inaendelea kwa kasi. Wakati huohuo, Polisi ya Kenya imeeleza kwamba inadhibiti ghorofa zote za jengo la kituo hicho cha biashara. Taarifa hiyo imeeleza kuwa, baada ya masaa machache itafanyika operesheni ya kumaliza kabisa tukio hilo lililodumu kwa siku tatu. Hadi sasa inaelezwa kuwa, watu wasiopungua 69 wameuawa na wengine wasiopungua 200 kujeruhiwa.

Kenya: Tunaidhibiti Westgate, operesheni iko ukingoni


Kenya: Tunaidhibiti Westgate, operesheni iko ukingoniSerikali ya Kenya imetangaza kuwa, vikosi vya usalama vya nchi hiyo vinadhibiti jengo la madula la Wesgate lililokuwa likidhibitiwa na magaidi wa kundi la wanamgambo wa al-Shabab. Taarifa ya serikali ya Kenya imesema kuwa, kwa sasa vikosi vya usalama vinapambana na gaidi mmoja au wawili ambao wamebakia katika jengo hilo. Manoah Esipisu, Msemaji wa serikali ya Kenya ametangaza kwamba, vikosi maalumu vya usalama vilivyoko katika eneo hilo vinaendelea kusonga mbele bila upinzani mkubwa. Aidha amesema kuwa, mateka wote waliokuwa wakishikiwa na magaidi hao wamekombolewa na kwa sasa inafanyika operesheni ya kumaliza kabisa tukio hilo lililodumu kwa siku tatu. Hadi sasa inaelezwa kuwa, watu wasiopungua 69 wameuawa na wengine wasiopungua 200 kujeruhiwa.

Monday, September 23, 2013

MAHOJIANO KWA LUGHA YA KISWAHILI KATI YA MWANDISHI WA HABARI NA MSEMAJI WA AL-SHABAAB JUU YA MAUAJI YA ZAIDI YA WATU 59 JIJINI NAIROBI...!!



Mwandishi Jamal Osman amefanya mahojiano exclusive na msemaji wa kundi la kigaidi la Al-Shabaab kuhusiana na sababu za kuishambulia mall ya Westgate. 


Hii ni tafsiri ya Kiswahili ya mahojiano hayo yaliyofanywa kwa Kiingereza kwenye mtandao wa Channel4


Jamal Osman: Kwanini mmefanya shambulio?
 
Msemaji wa Al-Shabaab: Sababu ya kufanya shambulio ni kuwalinda watu wetu na nchi yetu sababu Kenya ilitushambulia, bado wanaendelea kushikilia sehemu ya ardhi yetu. Tumekuwa majirani wenye amani, lakini wao ndio walitushambulia na tunajilinda. 

Haijalishi kama wewe ni Muislamu ama Mkristo, sheria inasema unatakiwa kujilinda mwenyewe dhidi ya yule aliyekushambulia.
 
JO: Mmeua watu wa mataifa mengi wakiwemo Waingereza, hamuogopi mataifa makubwa yatawatafuta?
 
Msemaji wa Al-Shabaab: Tumewaambia Wakenya na wale wanaoenda Kenya kwamba hatuwezi kuvumilia kile Kenya inatufanyia. Tuliwaambia tutajilinda wenyewe na tuliwaonya kuhusu kwenda Kenya. 

Wakenya wana damu yetu mikononi mwao. Mtu yeyote aliyejiandaa kwenda Kenya lazima ajiandae na kukabiliana na ukweli huo, na hatuwaogopi watu wa Ulaya ama Wamarekani sababu sisi si wadhaifu.
 Na tunasema hili kwa watu wa Ulaya na Wamarekani ambao wamekuwa wakiwasaidia wale wanaotushambulia, muwaambie Wakenya waache uonevu wao kama mnataka kuwa salama.
 
JO: Kwanini mliilenga mall ya Westgate?
 
Msemaji wa Al-Shabaab: Sababu ya kwanini tuliilenga mall ya Westgate, ni kwakuwa Wakenya na serikali yao wametumia majeshi dhidi yetu, ni maadui wetu. Wamewatuma watu wao Somalia, wameiunga mkono serikali yao kuishambulia nchi yetu. Kwetu, popote pale Kenya ni sawa, tutawapiga popote tuwezapo.
 Sababu tulilenga Westgate ni kwamba tunajua ni sehemu ambayo wanajisikia maumivu zaidi. Ni kwasababu inaingiza hela nyingi na ipo katikati ya jiji. 

Ni sehemu wanasikia maumivu na kwasababu tulitaka kutuma ujumbe na hatukutaka kuupoteza ujumbe wetu. Tulitaka ujumbe wetu umfikia kile Mkenya.
 
JO: Wapiganaji wenu ndani ya mall bado wanapigana?

Msemaji:
 Ni zaidi ya saa 27 sasa, wapo ndani na bado wameshika hatamu.
 
JO: Nasikia kuna mpiganaji mwanamke ndani pia?
 
Msemaji: Hatupeleki wanawake wetu kwenye uwanja wa vita.
 
JO: Kitu gani mnategemea kitatokea sasa? Nini litakuwa tokeo la hili?
 
Msemaji: Kama Mungu akipenda, tunategemea Wakenya watapata ujumbe kwamba kama ukimwaga damu, damu yako itamwagika pia. Kwao kujua kuwa hawawezi kushikilia Kismayu, Dhobley na Afmadow na wategemee waishi kwa amani Nairobi. Huo ni ujumbe tunataka kuutuma kwao.
 
JO. Kwenye jumbe zenu kupitia Twitter mnasema huu ni mwanzo tu na mtaendelea, ama mmeshafikia malengo yenu?
 
Msemaji: Tunasema kwa Kenya, iacheni nchi yetu. Huo ni ujumbe wa kwanza. Na kama wakikataa kuiacha nchi yetu basi tutaanzisha vita yenyewe.
 
JO: Hivyo matakwa yenu kwa Wakenya, ni kuiacha nchi yenu kama wanataka amani?

Msemaji:
 Kama Wakenya wanataka amani, wanatakiwa kuiacha nchi yetu.
 
JO: Kwanini mnawalenga watu wasio na hatia?
 
Msemaji: Raia wa kigeni, wanatakiwa kuondoka kwenye nchi hiyo (Kenya) kwasababu Wakenya na Al-Shabaab wapo kwenye mgogoro na tunamwambia kila mtu – Kenya ni eneo la vita.
 
JO: Kwakuwa unasema raia wa kigeni na Waingereza wana maslahi makubwa nchini Kenya, mna ujumbe gani kwao?

Msemaji: Tunasema kwa Waingereza, kwakuwa tunaamini wanawasaidia Wakenyan na Wakenya ni watumwa wao, wao (Waingereza) wanatakiwa kuwaambia Wakenya, walitoe jeshi lao Somalia.


 Na Waingereza wanajua Wasomali hawataka tamaa. Tuliwakatalia Waingereza mwanzoni, ambao wana nguvu kuliko Wakenya