ZANZIBAR
ZANZIBAR
IMEZINDUA SAFARI ZA NDEGE MOJA KWA MOJA KUTOKA JOHANNESBURG AFRIKA YA KUSINI
HADI ZANZIBAR.
AKIZUNGUMZA
KATIKA UZINDUZI HUO ULIOFANYIKA HOTELI YA LAGEMA NUNGWI, MAKAMU WA KWANZA WA
RAIS WA ZANZIBAR MHE. MAALIM SEIF SHARIF HAMAD, AMELIPONGEZA SHIRIKA LA NDEGE
LA MANGO KUTOKA NCHINI HUMO KWA KUAMUA KUANZISHA SAFARI HIZO.
AMESEMA
SAFARI HIZO ZITASAIDIA KUONGEZA IDADI YA WATALII KUTOKA AFRIKA YA KUSINI, HASA
IKIZINGATIWA KUWA WATALII WA NCHI HIYO TAYARI WAMERUHUSIWA KUINGIA NCHINI BILA
YA KUWA NA VIZA.
AMEFAHAMISHA
KUWA ZANZIBAR INATEGEMEA SANA SEKTA YA UTALII KATIKA KUKUZA UCHUMI WAKE, NA
KWAMBA KWA SASA NDIO SEKTA KIONGOZI INAYOCHANGIA UPATIKANAJI WA FEDHA ZA KIGENI
KWA ASILIMIA 72.
AMESEMA
SERIKALI KWA UPANDE WAKE ITAFANYA KILA JUHUDI KUSHIRIKIANA NA SHIRIKA HILO
PAMOJA NA WAWEKEZAJI WENGINE, ILI KUHAKIKISHA KUWA SEKTA YA UTALII NA
UWEKEZAJI ZINAPATA MAENDELEO MAKUBWA.
AIDHA MAKAMU
WA KWANZA WA RAIS AMEWATAKA WATEMBEZAJI WATALII PAMOJA NA VYOMBO VYA HABARI KUWA
MABALOZI WAZURI WA KUITANGAZA ZANZIBAR KWA WAGENI, ILI KUVUTIA WATALII NA
WAWEKEZAJI WENGI ZAIDI.
AMEONGEZA
KUWA LENGO LA SERIKALI NI KUONA KUWA INAFANYA KAZI KWA KARIBU ZAIDI NA WENZAO
WA AFRIKA YA KUSINI KATIKA SEKTA ZOTE ZA MAENDELEO, ILI KUNYANYUA HALI ZA
MAISHA KWA WANANCHI WA PANDE HIZO MBILI.
KWA UPANDE
WAKE BALOZI WA AFRIKA YA KUSINI NCHINI TANZANIA BW. THAMDUYCSE CHILLIZA AMESEMA
WANANCHI WA AFRIKA YA KUSINI MARA ZOTE WAMEKUWA WAKIJISIFIA UKARIMU WANAOUPATA
KUTOKA KWA NDUGU ZAO WA TANZANIA, NA KWAMBA HALI HIYO IMEKUWA IKIWAVUTIA
WAWEKEZAJI WENGI KUTOKA NCHI HIYO.
AMESEMA
UZINDUZI WA SAFARI HIZO ZA MOJA KWA MOJA UTARAHISISHA SAFARI ZA WATALII NA
WAWEKEZAJI WENGINE, SAMBAMBA NA KUKUZA UHUSIANO WA MUDA MREFU ULIOPO KATI YA
NCHI HIYO NA ZANZIBAR.
AMESEMA
TANZANIA IMEENDELEA KUWA NCHI MUHIMU BARANI AFRIKA KUTOKANA NA UWEPO WA AMANI
NA USALAMA, TOFAUTI NA ILIVYO KWA NCHI NYINGI ZA AFRIKA, HALI INAYOIPA NAFASI
KUBWA ZAIDI YA KUVUTIA WAWEKEZAJI KUTOKA NCHI MBALI MBALI DUNIANI.
NAE WAZIRI WA
HABARI, UTAMADUNI, UTALII NA MICHEZO MHE. SAID ALI MBAROUK, AMEPONGEZA JUHUDI
ZINAZOCHUKULIWA NA AFRIKA YA KUSINI KATIKA KUIMARISHA VITEGA UCHUMI VYAKE
ZANZIBAR.
AMESEMA HATUA
HIYO INADHIHIRISHA UKWELI KUWA ZANZIBAR NI MAHALI PAZURI NA SALAMA KWA
UWEKEZAJI NA WAGENI, NA KULITAKIA SHIRIKA HILO LA NDEGE MAFANIKIO MAKUBWA
KATIKA KUTEKELEZA MAJUKUMU YAKE YA KUTOA HUDUMA ZA USAFIRI WA NDEGE NCHINI.