Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Luteni mstaafu Chiku
Gallawa, amesema watu waliomuua askari mgambo Salum Mgonje na kumpiga risasi
Mkuu wa Kituo cha Polisi Songe, wilayani Kilindi Edward Lusekolo ni kikundi
kilichokuwa kinaishi msituni.
Alisema kikundi hicho kinaipinga Serikali ya Rais Jakaya Kikwete na kudai ni ya kikafiri kikiwa na mipango ya kutaka Tanzania isitawalike.Akizungumza na waandishi wa habari Mjini Handeni, Bi. Gallawa alisema kikundi hicho kiliweka kambi tatu wilayani humo kikifanya mafunzo mbalimbali yakiwemo ya kijeshi.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Luteni mstaafu Chiku Gallawa |
Alisema kikundi hicho kinaipinga Serikali ya Rais Jakaya Kikwete na kudai ni ya kikafiri kikiwa na mipango ya kutaka Tanzania isitawalike.Akizungumza na waandishi wa habari Mjini Handeni, Bi. Gallawa alisema kikundi hicho kiliweka kambi tatu wilayani humo kikifanya mafunzo mbalimbali yakiwemo ya kijeshi.
“Pia kikundi hiki ndicho kilichokuwa kikipinga mchakato wa sensa
mwaka 2012, kambi zao tatu zilikuwa katika Kata ya Lwande na Negero kwenye
Kijiji cha Madina.“Katika kambi ya Madina, wafuasi wao wawili wameuawa baada ya
kupinga kitendo cha kukamatwa na askari Oktoba 26 mwaka huu wakijiita wafuasi
wa Sunni,” alisema.
Aliwataja wafuasi waliouawa kuwa ni Ramadhan Hamis, ambaye ni
mfanyabiashara wa madini na mwingine jina lake halikufahamika
mara moja lakini inasemekana ni mwalimu wa dini ya Kiislamu (ustaadh) Kijiji
cha Lwande.
Aliongeza kuwa, kikundi hicho kimekutwa na bunduki tatu aina ya
gobore, shortgun moja, bastola mbili zilizotengenezwa kienyeji, mapanga 18 na
visu 10. Bi. Gallawa alisema wafuasi 46 wa kikundi
hicho tayari wamekamatwa lakini jambo la kushangaza wamo watumishi wa Serikali
ambao ni walimu wa shule za msingi na watafikishwa mahakamani wakati wowote.
Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa, ambayo
inaongozwa na Bi. Gallawa, imeamua kuweka kambi Kilindi kwani hivi sasa hali ya
usalama si nzuri hadi itakapotulia. Akizungumza na Majira hivi karibuni, Kamanda
wa Polisi mkoani humo, Constantine Masawe, alisema askari mgambo Salum Mgonje
aliuawa Oktoba 22 mwaka huu ambapo Edward alipigwa risasi za mbavu na mkononi
Oktoba 23, saa mbili usiku.
Kikundi hicho kinajumuisha wakazi wa vijiji
mbalimbali wilayani humo ambao wamefukuzwa na wenzao kutokana na tabia zao za
kupinga mambo mbalimbali ya maendeleo. Chanzo cha
kuanzishwa kikundi hicho ni baada ya mwenzao mmoja ambaye ni mfanyabiashara
kutakiwa kulipa ushuru katika Kijiji cha Lwande na kukataa hivyo mgambo
waliingilia kati ndipo wafuasi wao walichukua uamuzi wa kwenda kuwakata mapanga
mgambo ambao mmoja alijeruhiwa na mwingine kuuawa.
----MAJIRA
----MAJIRA