Na Mohammed Mhina, wa Jeshi la Polisi Zanzibar
Mahakama Kuu ya Vuga mjini
Zanzibar imetoa ushauri kwa Viongozi wa Jumuiya mbili za Kiislam
Zanzibar wanaotuhumiwa kwa makosa ya kuhatarisha usalama wa Taifa ya
kutotendewa haki wakiwa Gerezani wafungue kesi ya madai.
Ushauri huo umetolewa na Mrajisi
wa Mahakama Kuu ya Zanzibar Mh. George Kazi mara baada ya kupitia kwa
makini maombi ya watuhumiwa hao yaliyofikishwa mbele yake Novemba 8,
mwaka huu kupitia kwa mawakili wa watuhumiwa hao.
Kesi hiyo inawakabili watu wanane akiwemo Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maimamu Zanzibar
na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Uamsho Sheikhe Mselem Ali Mselem.
Wengine katika kesi hiyo ni Mussa
Juma Issa, Suleiman Juma Suleiman, Azan Khalid Hamdan, Khamis Ali
Suleiman, Hassan Bakar Suleiman na Ghalib Ahmada Omar.
Akitoa uwamuzi huo, Mh. Kazi
amesema watuhumiwa wana haki ya kufungua kesi mahakama kuu ya kile
wanachokilalamikia na kwamba mahakama kuu itakuwa na uwamuzi wa
kuyasikiliza madai yao tofauti na kesi ya msingi kwa watuhumiwa.